NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, May 17, 2011

Ati, Uraia wa Marekani wa Waziri Huyu Ndiyo Chanzo cha "Uvivu" Wake ???

 • Japo mimi si mwanasheria lakini pengine sitakosea nikisema kwamba Waziri huyu, kama kweli ana uraia wa Marekani atakuwa amevunja sheria kwani ninavyojua mimi Tanzania bado haijaruhusu uraia wa nchi mbili; na sina uhakika kama raia wa nchi nyingine anaweza kuwa waziri nchini Tanzania. Wanasheria mnajua.
 • Kilichonivutia katika habari hii ni lile dai kwamba waziri huyu anaonekana kuwa mvivu kutokana na ukweli kwamba eti anajali masuala ya Marekani zaidi kuliko ya Tanzania kutokana na ukweli kwamba yeye ni raia wa Marekani. 
 • Katika mijadala mingi kuhusu suala la uraia wa nchi mbili, hoja mojawapo ya msingi iliyotolewa na wale wanaopinga ni kuhusu wasiwasi wa kutokuwa na uzalendo kwa Watanzania watakaokuwa na uraia wa nchi mbili. Ni vigumu kuwatumikia mabwana wawili ati! 
 • Mimi nadhani "uvivu" wa mawaziri na watendaji wengine wakuu wa serikali ni tatizo la kimfumo zaidi kama bosi wao alivyowalalamikia kwa uchungu hivi karibuni HAPA na HAPA. Ni mawaziri wangapi ambao wanatazamwa vizuri na umma kuwa ni wachapa kazi, mawaziri ambao wanaweza kusimama na kusema kwamba wizara zao zimefanikiwa katika kutatua matatizo yanayowakabili wananchi? Wizara nyingi zinakumbwa na matatizo ya kiutendaji yakiwemo tuhuma za ufisadi. Hawa nao wana uraia wa nchi gani? Tunaweza kusema kwa uhakika kwamba "uvivu" wa Waziri huyu ni matokeo ya kuwa na uraia wa nchi mbili?
 • Unaweza kusoma mijadala mbalimbali kuhusu suala hili HAPAHAPA, HAPA na HAPA kuhusu suala hili.
**************

Pichani kushoto ni Waziri Cyril Chami na kulia ni 
Naibu wake Lazaro Nyalandu

Kufuatia sakata lililoibuliwa na gazeti la Dira ambalo liko mtaani leo lililoripoti kuwa kuna waziri mmoja kutoka wizara ya viwanda na biashara mwenye uraia wa Marekani, habari hiyo inaweka wazi kuwa waziri huyo amekuwa na tabia ya kipuuzi ya kumpeleka mkewe kujifungulia Marekani mara tu mkewe anapobakiza wiki mbili kabla ya kujifungua hali inayofanya watoto wake wawili kuwa na uraia wa taifa hilo tajiri zaidi duniani.

Waziri huyo kijana ana uraia wa Marekani hali inayodaiwa imeathiri uwajibikaji wake kwani amekuwa na uvivu wa kupindukia huku akili na moyo wake akielekeza Marekani. Blog yako hii ya kisiasa imefanya mahojiano na wasomi mbalimbali katika eneo la Mlimani la chuo kikuu cha Tanzania ambapo wasomi hao wamemtaka rais Jakaya Kikwete kumtimua kazi mara moja waziri huyo ambaye wamedai kuwa kwa tabia hiyo maana yake haipendi Tanzania, hana uzalendo, hafai kuwa kiongozi hivyo ang'olewe maramoja.

Chanzo: Nova Kambota

9 comments:

 1. Hii sasa kali, ina maana hata mawaziri tunahitaji 'maexpatriate'....oh isije ikawa ile ya `u-dunia' aliyeambiwa kuwa sio Mtanzania...!
  Hapo niwekeni sawa!

  ReplyDelete
 2. Stori ya vutia sana! Lakini, kwani serikali yenyewe itakuwa imelaza damu kiasi cha kwamba itamruhusu mwanasiasa mwenye utambulisho wasiwasi ajiunge nayo? Labda amekuwa Mmerikani hapo baadaye tu lakini analo kwao kabisa TZ (Kama mnavyojuwa, Amerika inautembeza na kuutangaza sana uraia wanchi yao kwa karibu kila mtu hapa duniani nami nimeona matangazo mengi sana katika INTERNET ya kusema: "Je, ungependa kuwa Mmerikani?")

  ReplyDelete
 3. kaazi kweli kweli....ndo sababu arusi yake ilikuwa matata sana!

  ReplyDelete
 4. kaka si kawaida yako kuwa kimya hivi,nikwema au box limebana?kila la kheri na familia!.

  ReplyDelete
 5. NCHI IMESHAKUWA YA KISANII
  SI AJABU HATA MKUU WA POLISI ANA URAIA WA AFGHANISTAN,NDIYO MAANA ANARUHUSU MAUAJI HOLELA YA RAIA WA UKWELI KWELI.

  ReplyDelete
 6. mimi kwa akili ya kawaida kabisa nahisi namjua huyo waliye mtarajia,ingawa hawakumtaja,kwani kati ya chami na nyarandu nani ana watoto wawili? kama wote wanao kuazia wawili rudi nani mkewe alijifungulia marekani angalau mtoto mmoja

  ReplyDelete
 7. Mwenyekiti, upo? Kunani? Umekua kimya sana!
  Arrah

  ReplyDelete
 8. Uko wapi Mwl. Masangu Matondo!

  ReplyDelete
 9. NAUNGA MKONO HOJA YA MALKIORY. UMEPOTEA BILA KUAGA

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU