NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, May 6, 2011

Fikra ya Ijumaa: Hebu Tutafakari Haya Maswali Mawili Kuhusu Kifo.

Watu wakishangilia kuuawa kwa Osama Bin Laden Washington D.C

(1) Swali la Kwanza
 • Kuna mantiki au faida yo yote kweli kwa binadamu kushangilia kifo cha binadamu mwenzake (hata kama ni mbaya namna gani) wakati akijua kuwa naye anaweza kufa wakati wo wote ule? 
(2) Swali la Pili
 • Hivi kuna tofauti yo yote marehemu akizikwa na maelfu ya watu au akizikwa na mtu mmoja? Umati wa watu (au mtu mmoja) katika mazishi unamsaidiaje marehemu? Ati, mafarao wa Misri waliojijingea makaburi ya kifahari na kuzikwa na vito vingi vya thamani walikuwa na unafuu au tofauti yo yote na masikini waliozikwa katika makaburi ya kawaida yasiyo na mapambo wala ishara zo zote za utajiri? Kuna Matabaka hata baada ya kufa? Binadamu!
Picha ya Osama iliyochorwa mchangani na mchoraji wa India. 
Picha zote ni kutoka Reuters

Kwa maoni ya wanafalsafa mbalimbali kuhusu kifo bofya HAPA.

3 comments:

 1. Kwani hivi MAREHEMU anajisikia kuwa kafa?

  ReplyDelete
 2. mhhh maweee

  ukifa wewe utafanyiwa sherehe kubwa na utazikwa ndani ya nyumba

  ReplyDelete
 3. Kuna maneno matakatifu yanasema kuwa `kila nafsi itaonja umauti...' its just a matter of time...ni swala la muda tu, leoo yeye, kesho yule...hata huyo aliyemuua, au aliyetangaza kifo chake kuwa `died or alive, ipo siku naye ataonja umauti.
  Kwahiyo kushangilia ni kujipa moyo tu kuwa `keshakufa' lakini tunasahau kuwa nasi ni maiti watarajiwa.
  Labda kitu cha kuwaza hapa ni `namna ya kifo'...kwasababu kila kifo lazima kiwe na sababu au sio?
  Unajua hata `izraili' mtoa roho naye atakufa?!!!
  Ni hilo tuu mkuu!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU