NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, May 8, 2011

KWA MAMA YANGU MPENDWA, MKE WANGU MWEMA NA AKINA MAMA WOTE DUNIANI: HONGERENI. LEO NI SIKU YENU. TUNAWAENZI !!!

Mamangu mpendwa nami mwaka jana nyumbani Bariadi. 
 • Kama nilivyokwisha kusema HAPA na HAPA kumhusu mamangu mpendwa, leo tena ni sikukuu ya Akina Mama hapa Marekani. Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza tena mamangu mzazi, mke wangu mpendwa pamoja na akina mama wote popote mlipo hapa duniani bila kuwasahau mashujaa wanablogu wenzetu kama mlivyorejelewa kiufundi sana na Mzee wa Changamoto  HAPA. Akina mama, ninyi ndiyo nguzo ya jamii na mchango wenu kamwe haupimiki wala kuelezeka. Tunawaenzi !!!
*******************
Kama picha hizi zinavyoonyesha, ni nani kama mama ???

imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com

7 comments:

 1. Hongera zenu akina MAMA! Mbarikiwe sana!

  ReplyDelete
 2. Honera sana akina MAMA. Hakuna kama mama.

  ReplyDelete
 3. Mama is always a heroine!Mama ni kila kitu!

  ReplyDelete
 4. Tuanze basi CAMPAIGN kila serikali duniani kwa siku kama hii iwachilie angalau akinamama 8 wafungwa. Kwani tunapofurahia siku kama hii, tunakuwa tunasahau mama waliokuwa jela, sehemu za vita na hali nyingi tu isiekuwa na ustaarabu wowote kutokana na upumbavu wetu sisi wanaume wenye kutawaliwa na jazba za hovyo kutokana na TESTOSTERONE.

  Asante sana, Mkuu Matondo, kwa kuwaorodhesha wote akinamama mhimu maishani mwako bila kujali umri. Wote ni muhimu sawa tu hasa ukizingatia kwamba mtoto wakike anazaliwa na mama yake akiwa tayari tumboni mwake keshabeba watoto wake wote atakaewazaa atakapokua...ni mama tayari!

  ReplyDelete
 5. Nimependa taswira.
  Lakini pia ninapenda namna ambavyo HUWA UNAJISHUSHA kuwa nasi. Kuwa na wale ambao wengine wa hadhi yako wasingeweka picha zao hapa. Kueleza yale ambayo kwa wengine ingekuwa balaa.
  Na UMEKUWA AKISI YA MALEZI YA MAMA.
  Namshukuru na kumuombea Mama

  ReplyDelete
 6. Wapendwa - asanteni. Ni kweli hakuna kama mama. Bila mama hakuna jamii na familia nyingi zitaparaganyika. Mama....


  Goodman: Wanaume sisi kweli ndiyo chanzo cha matatizo mengi hapa duniani. Tunaanzisha vita ambavyo mara nyingi waathirika wake wakuu ni wanawake na watoto. Wanaume siye....


  Mzee wa Changamoto: Asante kwa dua zako kwa mama yangu. Bila shaka Mungu Amezisikia.

  Kuhusu kujishusha, hata sina la kusema; na hata sina uhakika kama nafahamu unachokirejelea. Bila shaka unanifahamu vyema sasa kupitia mabandiko mbalimbali katika blogu yangu; na kwingineko. Mtu hata kama ungesoma namna gani, hata kama ungekuwa tajiri namna gani, hata kama ungekuwa mzuri namna gani, hata kama ungekuwa na madaraka makubwa namna gani, hata kama ungekuwa....ukweli ni kwamba bado tu wewe ni mnyama mwenye mapungufu na siku moja pumzi yako itakoma na utatoweka. Sote tungelikumbuka hili tungejinyenyekeza na kuwatendea binadamu wenzetu kwa heshima na haki.

  Asante Mzee wa Changamoto. Daima huwa kuna jipya la kujifunza katika blogu yako. Wewe ni uthibitisho tosha kwamba HEKIMA HAIPATIKANI KWENYE MVI TU !!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU