NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, May 10, 2011

NAPE NNAUYE KUUANIKA UFISADI UNAOFANYWA NA DR. SLAA NDANI YA CHADEMA !!!

 • Baada ya kujivua magamba, inaonekana CCM wamezinduka na sasa wako tayari kujibu hoja na malumbano ya CHADEMA majukwaani badala ya kukaa na kulalamika kwamba wanazushiwa mambo na kuomba msaada wa vyombo vya dola. Hivi ndivyo demokrasia inavyoendeshwa na hili ni jambo jema. CCM kama chama kingine cho chote cha kisiasa inabidi nao wataabike kwa kwenda kwa wananchi na kuwaeleza mafanikio na changamoto zao. Vinginevyo wapinzani watawafanyia kazi hiyo. 
 • Nape amefikia hatua hii baada ya Dr. Slaa kudai kwamba ameunasa waraka wa siri wa CCM ambao unaeleza sababu za chama hicho kushuka umaarufu. Kwa habari zaidi kuhusu waraka huu wa siri wa Dr. Slaa soma HAPA. Tunaomba tu kwamba majibizano haya yasiwe ya ki-Ad Hominem
**************** 

Nape Nnauye  akihutubia mkutano wa hadhara viwanja 
vya Ushirika Ikungi nje ya mji wa Singida LEO


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo atamwaga hadharani jinsi Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa anavyofanya ufisadi wa kutisha ndani ya chama hicho. Nape alisema ataeleza ufusadi huo, katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye Stendi Kuu ya Mabasi mjini Singida mjini, ukiwa ni mkutano wa pili, katika ziara ya viongozi wa Sektretarieti ya Halimashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM waliyoianza jana mkoani hapa.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya jengo la Ushirika Ikungi nje ya mji wa Singida, Nape alisema, anazo nyaraka zinazoonyesha Dk. Slaa na baadhi ya viongozi wa Chadema wanavyojinufaaisha na fedha za chama hicho huku wanachama wenyewe wakiendelea kumpigia makofi.


Katika ziara hiyo ya kujitambulisha msafara wa Sekretarieti hiyo ya CCM, unaoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Kapteni Mstaafu, John Chiligati Nape amefuatana pia na Katibu wa Uchumi na Fedha, Mchumi Mwigulu Nchemba na Katibu wa Oganaizesheni Asha Juma Abdallah.

Katika mikutano iliyofanyika jana, Ikungi na Ligwa, Nape alikanusha vikali kuwepo wa waraka wa siri wa Sekretarieti mpya ya  CCM ambao Dk. Slaa anadai kuwa nao. Amesema, kwa kujitapa kwenye majukwaa juzi mjini Sumbawanga, kwamba anazo nyaraka za siri za Sekretarieti hiyo, kwanza inadhimhirisha kwamba hajui nini maana ya siri  na dhahiri.Nape alisema, anachokiita Dk. Slaa kuwa siri ni udhanifu wa kupuuzwa kwa sababu yote yaliyoainishwa kwa ajili ya kutekelezwa na sekretarieti ya CCM baada ya kikao cha mjini Dodoma, hakuna hata moja ambalo ni siri hadi sasa.

Alisema, baada tu ya sekretarieti kukabidhiwa mikoba, imefanya mikutano ya hadhara zaidi ya kumi katika mikoa mbalimbali na kuelezwa kwa kinaga ubaga nini hasa kilichotokea Dodoma hadi kupatikana kwa sekretarieti mpya.Nape alisema, pamoja na mambo kadhaa wamekuwa wakieleza wazi kwamba kilichofanyika ni CCM kujifanyia tathmini kuona kama kweli hali ilimo sasa na inatosha kuipigisha hatua ya kuongoza sasa na baadaye.


Alisema, baada ya tathmini hiyo, kama chama komavu kiliyakubali mapungufu kiliyobaini na kuamua kwamba ili kuondokana na mapungufu yaliyobainika, lazima uongozi wa juu uliopo uwajibike, jambo ambalo hakuna chama kingine kinachoeweza kuthubu kikabaki salama."Jamani tilichofanya Dodoma ni kuwasha Mwenge kwa ajili ya kuongeza matumaini pale yalipoanza kufifia, kuongeza imani kwa chama pale ilipoanza kudorora, jambo ambalo kwa chama chenye umri mkubwa kama CCM lilikuwa la lazima", alisema Nape.


Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, Chiligati alisema, anachodai kuwa nacho Dk. Slaa na kukiona kuwa ni waraka wa siri, kama kweli anacho ni gamba ililotupa CCM ambalo linamyima usingizi.


Chiligati alisema, kwa kawaida kitu kinapokuwepo muda mrefu sana kisipojitazama upya kuendelea kuwepo kuwa kwa mashaka makubwa, na ndiyo maana CCM imeona umuhimu wa kujitathmini na kuamua bila kusita kujivua gamba.


Alifafanua kwamba, gamba ililojivua CCM si ngozi ila ni yale matendo maovu ambayo baadhi ya viongozi walianza kuyakumbatia kama ufisadi, na kutokifanya chama kuwa cha wanachama badala yake kuonekana cha wenye fedha. Chiligati alisema, kimsingi ufisadi na hali hiyo ya kutokifanya chama kuwa cha wanachama ndilo gamba lililovuliwa toka CCM amabalo sasa Dk. Slaa anataka kutamba nalo wakati CCM walishaachana nalo tangu mkutano ule mzito wa Dodoma.

Kwa upande wake, Nchemba alisema, kwa kujivua gamba sasa CCM ni mpya, wale waliokuwa wamekimbia kutokana na kero za baadhi ya viongozi, sasa warejee kwa sababu yale hayawezi kujirudia tena.

Alisema, sasa CCM itaendesha mambo yake kisasa na kisayansi zaidi kuliko ubabaishaji, ambapo mali na miradi ya chama popote ilipo haitaweza kutafunwa na mbadhirifu yeyote bali rasilimali hizo zitakuwa kwa manufaa ya wanachama wote.Miongoni mwa viongozi wa 

Sekretarieti hiyo mpya ambao hawapo kwenye ziara hiyo mkoani Singida ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambaye ana majukumu mengine.

Chanzo: H@ki Ngowi

6 comments:

 1. Dr. Slaa ni Mzee wa Udaku tu hana jipya.

  Mzee wa Udaku hongera kwa waraka na mabomu hewa!! Tathmini ni kuwa kiza kikizidi saaana ni karibu ya kupambazuka na dalili za kufa CDM ziko wazi maana data zenu hazina macho ni za kutunga kila kikicha, ni njia mliochaguwa na mbinu ya kuhadaa ili mukubalike, itafika kikomo na spidi ya kushuka ni kali kuliko hiyo mliopandia maana itakuwa sawa na gari lisilo na breki linavuja hovyo!!

  Kila kukicha mabomu hewa mbona yanaishia ktk mikutano na magazetini tuu? wakati una wanasheria na mawakili kibao ktk chama chako hamchukui hatua za mbele tukajiridhisha kuwa haya mambo na maneno yana ukweli?Blabla ndizo zinafikia ukomo na Mtoto usie funzwa unataka kuwavua nguo wazee wako ni utovu wa adabu!!jifanye kinyozi ikifika zamu yako utaona panchungu usitafute mchawi

  Nauye mwanike tuone madudu yake huyu padri mzinzi !!!

  ReplyDelete
 2. Naona Single ya kuwavua magamba mapacha matatu haijauza ya kutosha, Dogo sasa anakuja na single mpya, wasiwasi wangu sina hakika kama anauwezo wa kujenga na kupangua hoja kama slaa. NAAMNI AMEJIPANGA NA ANAWASILIANA NA VIONGOZI WENZAKE WA CHAMA, wasije wakapingana kama ya magamba

  ReplyDelete
 3. Siasa bwana, mmmmh, nakumbuka lile swali `siasa ni ukweli wenye uwongo ndani yake...jadili

  ReplyDelete
 4. nape kumlipua Slaa ni ndoto. bora amalizie kufukuzana na wenye chama (magamba).

  kumsema Dr slaa ni kujifanya kuwa mdaku

  ReplyDelete
 5. NAPE UMECHEMKA, NILIVUTIWA NA KASI YAKO YA KUZUNGUMZIA MAGAMBA MMEWAPA SIKU 90 WATOKE KATIKA CHAMA THEN KATIBU WAKO MKUU ALIKUPINGA HADHARANI KUWA KATIKA NEC HAKUKUWA NA AJENDA YA KUWAPA MAFISADI SIKU 90, KUMBE ULIZUSHA?, AU ZILIKUWA CHUKI ZAKO KWA LOWASA?, AU WAKUU WA CHAMA CHAKO WANAWAOGOPA MAGAMBA COZ WATAMWAGA MBOGA?, KATIKA HILI MMEPWAYA, MNAPINGANA HADHARANI, HUYU ANASEMA HIVI, YULE KESHO ANAKANUSHA, KAMA ISHU YA DOWANS, SITTA NA NGELEJA, NA WEREMA HUYU TULIPE,HUYU MKILIPA PATACHIMBIKA. MMETUONGOZA KWA HADAA NA WAZAZI WENU KWA MUDA MREFU, MOLA AMETUONEA HURUMA JUU YA MATESO YENU CCM KWETU WANANCHI, AMETULETEA DK WILBROAD PITER SLAA, HAMUNG'UNYI MANENO WALA HARUDI NYUMA KAMA NYINYI MAGAMBA,MAFISADI,NA WEZI. HAUNA CHA KUONGEA NAPE MBELE YA MPIGANAJI DK SLAA NA WATZ WA SASA WAKAKUELEWA, CCM MMECHAFUKA NA MNALEA UFISADI. AM DONE!.

  ReplyDelete
 6. Nape tulikuamini sana wakati unaanza mbio zako dhidi ya mafisadi wa nchi hii. Lakini nadhani umeshindwa kujua ni kwa nini chadema wanapata cha kuzungumza. Kwa kukusaidia tu kijana mwenzetu ni kwamba kaza buti kupambana na mafisadi kama ulivyotuhakikishia mwanzo, hapo utakuwa umewamaliza CHADEMA. Lakini ukijiingiza kwenye malumbano hakuna utakachoshinda la zaidi utapoteza na utapwaya sana. Epuka kuongeza maadui. endelea na mafisadi ukimaliza anza na Dr. slaa kama utakuwa na muda na uwezo.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU