NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, June 23, 2011

ATI, ITAKUWAJE SIKU JUA LA KIFIKRA LITAKAPOWAPAMBAZUKIA WALALAHOI ???

  • Wakati masikini walalahoi wanabanikana kama ndafu kwa kukwapuliana simu za mkononi, mikufu, hereni na saa, mafisadi wanaokwapua mabilioni ya shilingi na kudidimiza maendeleo yetu wanafanywa au wanafanyiana nini?
  • Ati, inakuwaje mtu anayekwapua simu anachomwa moto mpaka kufa na yule anayeiba mabilioni ya pesa za umma na kulitia taifa hasara kubwa hafanywi cho chote? Haki iko wapi? Ni kweli vyombo vya dola haviwezi kuikomesha hali hii ya walalahoi kupeana hukumu ya papo kwa papo namna hii? Au vinaiachia hali hii iendelee kwa makusudi kwa vile wanaobanikana ni walalahoi wenyewe kwa wenyewe? Vipi ingetokea siku moja mtu wa tabaka la juu akabanikwa? Vyombo vya dola kweli vingekaa kimya tu na kuacha hali iendelee?
  • Ati itakuwaje siku jua litakapowapambazukia walalahoi hawa na wakaamua kuanza kuwabanika mafisadi badala ya kubanikana wao kwa wao?
  • Japo kwa sasa jambo hili laweza kuonekana kama kichekesho lakini historia imejaa mifano tele ya aina hii; na kujipambanua kwa matabaka kati ya matajiri wa kupindukia kwa upande mmoja na walalahoi kwa upande mwingine tunakokushuhudia kwa sasa hakutoi picha ya kupendeza. Na ishara zote zimeshaanza kuonyesha kwamba walalahoi wa Tanzania tayari wameshaanza kuamka kutoka katika usingizi wao mrefu wa kifikra. 
  • Natumaini kwamba viongozi wetu hawako katika kunguku na wanaliona hili. Kushughulikia kero za walalahoi na kuinua hali zao za maisha (na hivyo kupunguza ufa kati ya matajiri na masikini) ndiyo suluhu pekee ya kukwepa misukosuko mikubwa ya kijamii kama hii.

Kwa habari zaidi kuhusu picha hii bofya HAPA

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU