NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, June 17, 2011

WADAU, SAMAHANI KWA KUPOTEA BILA KUAGA. SASA NIMERUDI RASMI...

Wadau wa blogu hii. Mbali na hekaheka za kubeba maboksi, nilikuwa pia na misukosuko midogo ya kiafya. Ndiyo maana kuonekana kwangu hapa bloguni kulikuwa ni kwa kusuasua sana kwa siku za hivi karibuni.

Napenda kutoa shukrani zangu kwa wote mlioniulizia (Dada Rachel, Mpiganaji Matiya, Mchungaji Arrah, Mchambuzi Meghji, Da Subi na wengineo wengi ambao sikuwataja hapa). Asanteni sana. Tupo pamoja na sasa mtaanza tena kuniona katika blogu zenu. Tuwemo...

4 comments:

 1. Nilikua nasikitika sana kila nikifungua blog nakuta hola,this is my fave blog,welcome back

  ReplyDelete
 2. Pole Matondo kwa majukumu na misukosuko kidogo ya afya uliyokumbana nayo. Mungu ayaeupeshe mbali, maana mchango wangu ni muhimu katika ujenzi wa taifa letu la Tanzania japo bado watu wengine hawajatambua umuhimu wa watanzania waishio nje ya nchi.

  ReplyDelete
 3. Karibu tena Prof. Matondo.
  Pole kwa yaliyokuwa yanakusibu (narejea maoni ya Malkiory hapo juu, sikufahamu ulikuwa katika hali hati hati).
  Karibu tena kilingeni Mwalimu!

  ReplyDelete
 4. Asanteni jamani. Kuhusu afya ni mambo ya kawaida tu. Unajua tena siye binadamu...Nipo salama kabisa!

  Anony - asante kwa kunifuatilia na pole kwa kunikosa. Nimerudi sasa na naahidi kuandika kwa kina zaidi safari hii bila kujali kama kuna wasomaji wengi ama la. Hata kama wewe pekee ni mfuatiliaji wa blogu hii basi inatosha. Tuendelee na libeneke..

  Matiya - Nimeyaona mabadiliko makubwa katika tovuti yako mpya. Ni hatua nzuri na ni wazi kwamba umepania kuendelea na harakati zako.

  Kuhusu kutotambuliwa kwa umuhimu wa watanzania waishio nje ya nchi sijui. Nadhani wanatambua umuhimu wetu lakini pengine hawafurahii tunapoandika na kuweka mitazamo yetu wazi - hata kama inakinza tabaka lililo madarakani. Pia kumbuka kwamba ile dhana ya kwamba tulioko nje ni wasaliti bado ipo. Ndiyo maana akina Nyalandu wanafikia hata kusema kwamba Watanzania walioko nje ni walalamikaji tu wasio na mchango wa maana. Hili si jambo la kukatisha tamaa. Kwa watu wenye mtazamo mpana na wenye kuelewa mambo bila shaka wanathamini mchango wetu...Tusikate tamaa tafadhali.

  Da Subi - Asante. Mambo yalikuwa mushkeli kidogo. Nitaweka bandiko hapa kesho kuhusu ugumu wetu wanaume kwenda hospitalini kuchunguzwa. Nilikwenda kufanya "annual checkup" ya kawaida tu na daktari akakuta kuna mushkeli fulani. Mambo yamesharekebishika na sasa niko salama. Sasa utaniona kule wavuti mara kwa mara...

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU