NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, June 26, 2011

UTAJIRI WA KUTISHA WA WATUMISHI WA MUNGU

 • Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwasha moto kwa kudai kwamba baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, utajiri wa kutisha wa baadhi ya viongozi hawa wa dini umeanza kutiliwa mashaka. 
 • Habari hizi zinakuja wakati ambapo injili ya utajirisho imepamba moto duniani kote. Injili hii inasisitiza kuhusu upokeaji wa mibaraka ya Mungu kama ilivyoahidiwa katika Biblia. Mara nyingi, hata hivyo, kabla hujapokea mibaraka hii ni lazima "upande mbegu" kwa kutoa - mbali na sadaka ya kawaida iliyoamriwa ya fungu la kumi - kiasi cha fedha kanisani ili kuendeleza shughuli za injili. Kwa hapa Marekani wachungaji wengi wanapendelea upande mbegu ya kuanzia  dola 1,000 na hapo mibaraka ya Mungu itakushukia kama mvua - "guaranteed" !
 • Wapo wanaodai kwamba injili hii ya utajirisho imeweza kutumiwa vibaya na baadhi ya watumishi wa Mungu waroho ambao kwa kutumia bashasha na "miujiza" yao wameweza kuwashawishi waumini wao kuuza kila kitu walichonacho na kutoa sadaka kanisani. Na kwa kufanya hivi, watumishi hawa wa Mungu wameweza kuwa matajiri wa kutupwa wakati waumini wao wakiishi katika umasikini. Watumishi hawa wa Mungu wana majumba ya kifalme, madege binafsi ya kusafiria, helikopita na wanaendesha magari ya gharama kubwa. Hivi karibuni shirika la BBC lilichapisha makala juu ya utajiri wa kutisha wa wahubiri wa Nigeria ambao unazidi hata utajiri wa wafanyabiashara wa mafuta. 
 • Sina ugomvi na watumishi hawa wa Mungu kutajirika lakini kama kweli wanajitajirisha kwa kupitia njia za mkato kama vile kuuza madawa ya kulevya na kuwanyonya waumini wao basi ni wazi kwamba wamesahau lengo lao la kueneza injili na kuwaleta kondoo kwa Bwana. Na kwa maoni yangu, watumishi wa Mungu wa aina hii hawana tofauti na mafisadi wanaoiangamiza jamii. Kila mtu na ashike sana alichonacho!
 • Hebu tumsikilize Mchungaji Munishi na wimbo wake huu niupendao sana wa "Wanamwabudu Nani". 

Kwa picha na habari zaidi bofya HAPA. Tamko la Maaskofu kuhusu sakata la madawa ya kulevya lipo HAPA

8 comments:

 1. Dini ni bonge la Biashara!

  Ukifuatilia hata historia ya kanisa mpaka akina Martin Luther wanafukuzwa kanisa Katoliki , unaweza kustukia Biashara Kanisani ilianza zamani na labda mapaka leo hakuna waendesha dini waliowahi kufanya biashara kama MAPAPA wa kanisa la Katoliki wa enzi hizo ambapo waliweza mpaka kuuza kusamehewa dhambi na kukuhakikishia mahali mbinguni kama utalipia.

  Yakinishinda sijui nami nianzishe kanisa?

  Nawaza tu kwa sauti!:-(

  ReplyDelete
 2. Dini ni njia ya kumnyonya mnyonge maana tukiangalia nyuma kidogo kipindi cha ukoloni dini ilikuwa moja ya njia za kumlainisha masikini ili aweze kutawalika kirahisi hivyo mimi binafsi sishangai kuona haya yakitokea,biblia inasema kwa tajiri ni vigumu kulithi ufalme wa mbingu sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano sasa hawa jamaa wao hawataki kwenda mbinguni?mbona wanaipenda sana dunia?kuna uwalakini na hizi huduma zao aiseee

  ReplyDelete
 3. TUPO KTK WAKATI WA NEW GENERATION MOVEMENT. USISHANGAE NI LAZIMA HAYO YAWEPO ILI HATMAYE UKWELI UBAINIKE...

  JE, UNATAARIFA KUWA HAO VIONGOZI WA DINI HUDUMA YAO INAHUSISHWA NA NGUVU ZA KICHAWI?

  TAFITI UTABAINI SIRI NZITO NYEUSI. NA KWELI NI NI SIRI NZITO AISEE.

  KWA WAMAREKANI WANA KITU INAITWA BLACK BADGET, UNAFAHAMU DHUMUNI LA HII BLACK BADGET? HILO NALO NI SOMO JINGINE GUMU PANA.

  SOMA KITABU KINACHOITWA THE LOST SYMBOL UTAFAHAMU MENGI.

  ReplyDelete
 4. Afrika tunatakiwa tubadilike kifikra, hizi si nyakati za kuwaita viongozi waheshimiwa na wachungaji na mapadre, bwana asifiwe sana. Hizi heshima za kinafiki zimepitwa na wakati na huwa zinawapa kiburi. Viongozi wengi wamekuwa wakifanya maovu kwa vile wanaabudiwa kama miungu.

  ReplyDelete
 5. Bahati mbaya sana dini zimevamiwa na matapeli tena vihiyo wanaokula kwa mikono na miguu bila kunawa wakitapika humo humo walamo. Kimsingi ujambazi huu unalindwa na tawala jambazi zilizomo kitanda kimoja nao. Ni wakati muafaka kuwabana akina Rwakatare waeleze walikochuma utajiri wao wa kutisha zaidi ya kuiba sadaka na kuuza mihadarati. Tuwe macho na hawa wanaodai wana roho mtakatifu wakati ukweli wana roho mtakakitu.

  ReplyDelete
 6. hii dini ashara, wanatajirika sana watoto wao wanasoma shule nzuri mtoto wa muumini yuko shule ya kata .mama mchungaji anavaa kiatu cha elf arobain muumini muumin yebo lakini hawashituk sijui wanawaroga hawa watu?

  ReplyDelete
 7. yaani kama kijana wako amejiingiza huko ujue umempoteza kwani mchungaji ndiye atajifanya baba na mke wa mchungaji ni mama watamn'gan'gania hasa akiwa na kamshahara utafikiria wamesomesha wao i hate them so much

  ReplyDelete
 8. jaribu kufanya utafiti uone kama kuna kijana wa kilokole anamiliki pikipiki aukama ana maendeleo yoyote yale, kwanza hana muda wa kutafuta ili ajiongezee kipato. pia wachungaji hawataki kijana aoe au aolewe na mtu tofauti na wa zehebu lao yaani utafikiri wao ndio wazazi wa vijana hao

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU