NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, June 23, 2011

WATUNGA SHERIA WETU NA POSHO ZAO NONO !!!

  • Mjadala wa kufutwa kwa posho nono za wabunge uliowashwa na Mh. Freeman Mbowe unafurahisha na pengine unaakisi mwelekeo hasa wa jamii tunayotaka kuijenga na kuiimarisha, jamii ambayo kupitia kwayo mustakabali wetu mzima kama taifa unategemea. Mbowe ameonyesha azma yake ya kiungwana kwa kurudisha shangingi lake (japo ofisi ya bunge inakana na kutoa masharti), jambo ambalo limepokelewa vyema (kikejeli?) na mpiga mbiu mkuu wa Chama tawala. Kwingineko, mtendaji mkuu wa serikali naye ameonekana kuunga mkono harakati hizi kwa kuamua kuacha kutumia gari lake ghali aina ya Mercedes Benz.
  • Inafurahisha kuona kwamba angalau kwa sasa kuna chama cha upinzani ambacho kusema kweli kinatoa mchango mkubwa katika kuwaamsha Watanzania na kuhakikisha kuwa kinasikilizwa na Watanzania hasa wale wa tabala la chini (ambao ndiyo wengi). Hii inakifanya chama kilichopo madarakani kufungua masikio na kusikiliza (na hata kujivua gamba). Na hili ni jambo jema katika jitihada zetu za kujiletea maendeleo. Jambo la muhimu tu ni kwamba tuendeshe harakati hizi za kuamshana na kupigania maendeleo ya Watanzania wote kwa njia za amani. Tunaelekea kwema !!!

2 comments:

  1. Najaribu kuwaza kama kila chama kingekuwa angalau na wawakilishi watano bungeni, na kila chama kikatoa michango yake, na chama tawala kikawa radhi kuchukua hiyo michango...tungekuwa mbali...TUPO PAMOJA DAIMA

    ReplyDelete
  2. Chadema - mbali na matatizo yake yote kitaingia katika historia ya nchi yetu kama ambacho kilitoa mkubwa katika kuleta mwamko wa kisiasa nchi mwetu. Hakuna chama kilichowaamsha CCM kama Chadema.

    Kama nilivyosema - tufanye harakati hizi za kisiasa kwa njia za amani. Pamoja !

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU