NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, July 9, 2011

MAFITHADI THUGU.......

Mimi naendelea kuuliza tena na tena, hili zoezi la kujivua magamba litamalizika lini? Tusipokuwa makini nyoka wetu huyu atabakia na mabakamabaka kila mahali - hapa ngozi mpya na pale kuukuu tena iliyokakawana. Kama kujivua kumeshindikana, pengine tujaribu kuvulishana - hata kama ni kwa "kumwagiana tindikali". Mkanganyiko!

5 comments:

 1. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 2. Katika utetezi KIMSEMO usemekanao ni wa kiafrika:
  ``HARAKAHARAKA sio MWENDO na haina BARAKA!´´

  Si yasemekana Fisadi akijivua haraka gamba atachekwa mtaani alichokula kiko wapi na gamba hana?

  SI nasikia kama ukatoka ofisi yenye ulaji HARAKAHARAKA bila ulaji ni mpaka ndugu na jamaa wanawezakukutenga kisa si MJANJA na hufai kuwa mwenyekiti wa kikao cha harusi ya ndugu?:-(

  Labda wanajivua taratibu ! Na taratibu inafanya kazi katika jamii ya KITANZANIA kwakuwa katika JAMII yetu kidogo tu tunasahau kuwa WAZIRI wa KILIMO aliamishwa tu wizara baada ya kuharibu wizara ya FEDHA tokea enzi za NYERER!:-(

  ReplyDelete
 3. Mtakatifu: Kweli tupu. Umenikumbusha swali moja la Kiswahili katika mtihani mmojawapo niliowahi kuufanya: Eleza faida na hasara za methali zifuatazo:

  (1) Haraka haraka haina baraka

  (2) Mvumilivu hula mbivu

  (3) Ukiona mwanzako anayolewa wewe tia maji.

  Katika hili la kujivua gamba, methali ya haraka haraka haifanyi kazi kwani tunaambiwa kwamba wakati wa nyoka kujivua gamba ukifika ni lazima afanye hivyo vinginevyo kemikali zinazotolewa kwa ajili ya kazi hiyo zisipotumika zinaweza kumdhuru.

  Halafu umegusia jambo la muhimu. Ukijivua gamba wakati hujameza windo la kutosha basi jamii inakucheka. Na huu ni mkanganyiko ambao kidogo unashangaza: Jamii inapiga makelele kupinga ufisadi wakati inawashabikia mafisadi na kuwaita "wanaume". Ukiwa waziri halafu ujivue/uvulishwe gamba na uwe hujafisadika vya kutosha basi jamii itakucheka sana.

  Jamii ingekuwa kweli inawachukia mafisadi, mambo yasingekuwa kama yalivyo. Kumbuka hii ni jamii ambayo inawachoma vibaka wanaokwapua simu, saa au hereni mitaani!

  ReplyDelete
 4. Kwanza umesema `nyoka' ...hivi kweli ukifuga nyoka una amani...hapana, hata awe na gamba jesui livuliwe liwe jeupe bado ni nyoka, na nyoka anaogopewa wakati wote...huyu aliyetoa msemo huu kaweka tungo tata...kwani `mfuga nyoka, mwisho wa siku ataumwa mwenyewe...!

  ReplyDelete
 5. Zoezi Limeanza.. Na muheshimiwa Rostam.. Nadhani Mbunge wako Mzee wa Visenti atafuata... HAWA JAMAA WANA HELA NYINGI, KAMA MZEE WA VISENTI ACCOUNT MOJA TU ZAIDI YA DOLA MILIONI MOJA. kwanini anabanana na wakina mnyika kwa mshahara wa dola 4,500 kwa mwezi, tena za kusimangiwa...

  kweli watu wana-ngozi ngumu

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU