NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, July 9, 2011

MBUNGE WANGU AZIDI KUBANWA. SASA NAPE ADAI NI LAZIMA AJIVUE GAMBA...


Sakata la Mbunge wangu (Bwn. Chenge) kuhusu ununuzi wa rada ambalo nilianza kulijadili jana linazidi kuchukua sura mpya. Hata baada ya "kusafishwa" rasmi na serikali pamoja na TAKURURU, wakuu wa chama chake bado wanamtaka ajivue gamba

Dr. Slaa naye tayari ameshawasilisha serikalini uchambuzi wa ushahidi utakaosaidia kumtia hatiani Chenge. Sijui mbunge wangu huyu kama safari hii atasalimika.

Sakata hili pia inaibua swali jingine: Ati, ni kwa nini wanasiasa wa Afrika ni wagumu sana kuwajibika na kujiuzuru hata kama tayari ni matajiri wa kutupwa? Kwa nini wanasiasa wa nchi za Magharibi wakiguswa na ka kashfa tu kadogo basi wanawajibika na kuachia ngazi mara moja?

3 comments:

 1. Hili ni swali muhimu sana. Kwa nini viongozi wetu hawapendi kuwajibika? Busara ambayo ingemtosha bwana AC ni kubwaga manyanga aendelee na maisha mengine.

  Si yeye tu, hata waziri ambaye suala la umeme limemshinda, pengine busara ishindayo busara zote ni kukaa kando yaje mawazo mapya.

  ReplyDelete
 2. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 3. Ndiyo Bwana Fadhy. Kidogo inashangaza. Ungedhani kwamba kwa mapesa yote haya basi mtu kama AC pengine angeamua kuachia ngazi na kujipumzisha na kufaidi mapesa yake lakini wapi.

  Huyo waziri wa umeme ni yale yale. Nchi ipo gizani, kashfa za rushwa na ufisadi zinamwandama lakini wapi. Pengine akitoka hapo utasikia amehamishiwa wizara nyingine. Huko nako akilianzisha basi anahamishiwa wizara nyingine. Mzunguko wa kushangaza...

  Mimi nadhani pengine AC hizi bilioni sio zake peke yake. Pengine ni za ushirika na akijiuzulu pengine anaogopa kutoswa.

  Yupo mshtakiwa mmoja kwenye kesi inayowakabili akina Mramba ananishangaza. Mke wake yuko huku Marekani na anaishi maisha magumu kidogo na inashangaza kama kweli mumewe ana mapesa yote yale anayodaiwa kuiba, kayaweka wapi? Mbona asimnunulie mkewe na watoto angalau nyumba wakaishi kwa raha. Au kaficha hayo mabilioni katika benki za nje?

  Suala hili linahitaji mada nzima kwani ni zito.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU