NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, July 28, 2011

NI KWELI DAWA YA BABU HAIFANYI NA HAIJAFANYA KAZI ???

 • Hata kama ni kweli kwamba dawa hii haitibu, kisiasa ilikuwa ni "tiba" tosha katika kipindi ambacho taifa lilikuwa linapita katika vuguvugu la kashfa mbalimbali zikiwemo DOWANS na RICHMOND. Badala ya kuripoti kuhusu mambo haya muhimu kisiasa, vyombo vya habari vilitupia hasa macho yao Loliondo na sehemu zingine nchini ambako watoa vikombe walikuwa wakiibuka kila siku. Moto huu uliendelea kuchochewa na viongozi wa serikali na chama waliokuwa wakimiminika huko Loliondo kupata hiyo tiba ingawa wengine walidai kwamba walikuwa wanakwenda huko kwa ajili ya "curiosity" tu na si vinginevyo. Viongozi kadhaa wa upinzani walilalamikia jambo hili na kusema kwamba serikali ilikuwa inashabikia tiba hizi za kiimani ili kujaribu kupoteza mwelekeo wa kesi na kashfa mbalimbali za kifisadi zilizokuwa zikiiandama.
 • Kama madai haya ni kweli basi si kweli kudai kwamba eti tiba hii ya babu haitibu. Ilikuwa tiba tosha kisiasa na imeshafanya kazi yake; na sasa babu anaweza kuendelea na shughuli zake nyingine. Kuna anayejua sakata la DOWANS lilikoishia? RICHMOND je?

5 comments:

 1. Profesa, maoni yangu hayahusiani na chapisho la leo ila ninataka kukamata -attention- yako kukusihi usome ujumbe kwenye -inbox- yako kupitia anwani profesamatondo at gmail.com maana nimekuandikia mara 2 lakini sijapata majibu (naogopa mie).

  ReplyDelete
 2. Ilikuwa ni mbinu tu ya kutuliza moto wa mapambano dhidi ya ufisadi.

  ReplyDelete
 3. Kisiasa sasa hivi ni wakati muafaka kujitenga nayo!

  Mie kwa kawaida ni Tomaso ! Nisiposhuhudia uponyaji siamini DAWA!:-(

  Na mpaka sasa hivi sijashuhudia uponyaji wa SERIKALI yetu katika ugonjwa uikabilio TANZANIA kama NCHI ambayo naamini haistahili kuwa ilipo sasa hivi katika karne hii!:-(

  ReplyDelete
 4. Da Subi - niko salama. E-mail yangu ilikuwa na matatizo. Google walifuta inbox yote. Nitakupigia!

  Matiya - Pengine ilitokea kwa bahati tu kwamba Loliondo ikafumuka wakati kashfa zile zimepamba moto na ikafanikiwa kuzifunika kabisa.

  Mtakatifu - Sidhani kama serikali ina uponyaji. Pengine inataka kujua kwanza hatua anazochukua mgonjwa katika kujaribu kujiponyesha mwenyewe. Kama mganga hajigangi, swali ni kwamba, mgonjwa aweza kujiponyesha mwenyewe?

  ReplyDelete
 5. Eh, pole Profesa.
  Nimesoma ujumbe wa mbeleni uliotupasha masaibu yaliyokukumba, basi nakutakia mafanikio mema katika kusubiri google wakurejeshes barua zako.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU