NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, July 29, 2011

TANGAZO: TATIZO KUHUSU E-MAIL YANGU YA GMAIL (NA MENGINEYO)

 • Wapendwa: Inbox na Sentbox ya Email yangu ya gmail (profesamatondo@gmail.com) zilifutwa na pengine zilijifuta (kama google walivyodai) na imenichukua muda kupata usaidizi wa Google kuzirudisha japo sina uhakika kama meseji zote zimerudishwa. Kwa sasa najibu e-mail za watu polepole hasa zile za muhimu.
 • Kwa hivyo kama uliniandikia na hukupata jibu, naomba radhi. Naahidi kwamba nitajibu meseji zote za kibinafsi......
 • Kuhusu kutoonekana hapa kibarazani kwangu na katika vibaraza vya wanablogu wenzangu mara kwa mara ni kutokana na hekaheka za safari na mabadiliko makubwa ya kimaisha na kifamilia ninayokabiliana nayo kwa sasa. Naamini mambo yatatulia na kurudi katika hali yake ya kawaida. Tuko pamoja na kamwe sitakaa niache kublogu na kusoma blogu za wanablogu wenzangu. Kublogu ni mojawapo ya mambo ya muhimu kabisa ambayo nimeshawahi kufanya katika maisha yangu.

5 comments:

 1. Prof pole sana kwa hayo. Mie siku hizi nimekuwa na tatizo zile following up comments kwenye post nazotoa maoni haziji tena kwenye email yangu ya gmail. Kumbe napaswa wasiliana na Google!

  Ila mkuu sijakuelewa unavyosema unapitia mabadiliko makubwa kimaisha na kifamilia. Sentensi inaacha gepu kubwa kweli. Eniwei, nakutakia kila la kheri.

  Nashukuru umerejea maana blog hii ni moja ya blog ambazo hupita kila niamkapo kabla ya kuendelea na ratiba zingine. Na kutwa nzima hupita nichote maarifa.

  Ahsante kwa kusema hutoacha kublog. Ni kauli ya kutia moyo kwa kiasi kikubwa. Mungu akutangulie.

  ReplyDelete
 2. Bwana Fadhy - Asante sana kwa maneno yako ya kutia moyo; na kwa kuwa mdau wa kutegemewa wa blogu hii. Wewe ni mmoja ya watu wenye mtazamo mpana sana kuhusu mambo mbalimbali na nimefarijika kuona kwamba unavutiwa na blogu hii. Muda ni wa kuiba na pengine nikitulia safari hii nitajaribu kuandika kwa kina zaidi. Sitaacha kublogu!

  Google walikumbwa na kigugumizi (glitch) katika mitambo yao na wakafuta kabisa inbox za watu kibao. Nadhani e-mail yangu pia ilikumbwa na kigugumizi hicho. Uzuri ni kwamba waliweza kuzirudisha ingawa ni mrundikano hasa.

  Hilo tatizo lako inawezekana ni matatizo ya settings tu. Angalia vizuri hiyo email uliyotegeshea huko kama bado ni ile unayodhani. Jaribu kutafuta majibu mtandaoni na ukikwamba kabisa basi muulize mtaalamu wetu Da Subi. Google inategemea - wakati mwingine wanajibu na wakati mwingine wanakaa kimya tu.

  Mabadiliko ninayoyarejelea hapa ni ya kawaida tu. Niko salama na maisha ni lazima yaendelee. Tuko pamoja!

  ReplyDelete
 3. Ndugu yangu, katika mila yetu ya kisukuma kuaga ni muhimu sana na nilitegemea kwa vile wewe ni mmoja wa watu wanao enzi vilivyo ingekuwa ni bora zaidi ukawa unafanya hivyo ili kutuondelea simanzi.
  Wasukuma pia wanaamini, ukiondoka bila kuaga inamaanisha kule uendako hakujulikani na kama kunajulikana basi kile ukiendeacho unakuwa huna uhakika kama utakipata, Kwa hili unanilejesha kwenye sentensi yako unaposema kuwa unapitia mabadiliko makubwa kimaisha na kifamilia.
  Sina budi kukuombea baraka za Mola ili mapitio hayo yawe ya mafanikio makubwa.
  Kumbuka blog hii ni kisima cha mawazo endelevu na hekima. kwa sisi tunaofuatilia blog hii, tunafedheheka tunapokumbana na maswali yasiyo na majibu.
  Cha muhimu kabisa umetueleza kuwa blog itaendelea kama Samora Machel alivyopenda kusema ''A luta continua''

  ReplyDelete
 4. Ng'wanaMwamapalala:

  Asante kwa kunikumbusha kuhusu mila zetu. Siku nyingine "nikisafiri" na kutoonekana hapa basi nitahakikisha kuwa naaga.

  Kuhusu mabadiliko niliyoyarejelea ni mambo ya kawaida tu na pengine niseme ni mabadiliko chanya lakini kwa vile ni mabadiliko yanaogofya.

  Kama nilivyomwambia Fadhy hapo juu, nategemea kuanza kuandika kwa kina zaidi. Kuhusu maswali yasiyo na majibu - unamaanisha maswali yanayoulizwa kwenye maoni na wadau au maswali ninayouliza mimi kwenye machapisho yangu? Maswali na maoni ya wadau huwa najaribu sana kuyajibu kila inapowezekana.

  Mimi binafsi huwa napenda sana kuuliza maswali kwani huwa naamini kwamba ni kupitia katika majibu yanayotokana na mitazamo mbalimbali - hasa kinzani - ndiyo hasa tunaweza kupata japo fununu ya ukweli wa kile tukisakacho. Kwa hivyo maswali mengi niyaulizayo hapa kusema kweli hata mimi sina majibu. Au pengine tujiulize tu, ni kweli kuna majibu? Kumbuka kwamba hata kuna watu wanaodai kwamba 3 + 3 siyo lazima iwe sita hasa kama unajumlisha vitu vyenye uwezo wa kujibadili umbo au kujigawa haraka haraka.

  Obeja namhala. Bagishage pye koi. Hangamaga !!!

  ReplyDelete
 5. Namhala, ninakushukuru kwa ahadi uliyoitoa kwa kusema kila ''ukisafiri'' utakuwa unajitahidi kuaga, pia maelezo uliyonipa nimeyaelewa na yametoshereza.
  Nahene nkoi!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU