NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, August 23, 2011

ATI, MIHADHARA HII CHOCHEZI INA LENGO GANI HASA ???

Picha hii iko HAPA

Leo wakati natafuta nyimbo za Rose Muhando na Bahati Bukuku katika Youtube, nimekutana na mambo ya ajabu. Watu wameamua kuweka "mihadhara" yenye kutetea dini ya Kiislamu kwa kutumia majina ya waimbaji mashuhuri wa injili kama Rose Muhando, Bahati Bukuku na wengineo (mf. tazama HAPA).

Video ina jina la Rose Muhando lakini ukibofya unapelekwa kwenye video inayoonyesha mihadhara ya kitoto kati ya Uislamu na Ukristo - mihadhara ambayo lengo lake hasa mimi huwa silielewi japo kuna kipindi ilikuwa imejikita sana kule nyumbani.  Kwa kawaida katika mijadala hii Ukristo huwa unashambuliwa sana, Biblia hupotoshwa na kutafsriwa nje ya mandhari na muktadha wake; na Uislamu hushadidiwa kuwa ndiyo dini ya kweli na mwanzilishi wake kuwa ndiye hasa mtume wa mwisho aliyefunga kazi. Daima mwamba ngoma huvutia kwake ati!

Hata hivyo ukisikiliza na kufuatilia vizuri mijadala hii ni wazi kwamba hoja nyingi zinazotolewa zimeegemea katika mihemko, hazina nguvu, zimejaa jazba, hazina umakinifu na hazijachujwa vizuri. Unaweza hata kupata fununu kuhusu kiwango cha elimu-dunia cha watoa mihadhara hawa na wasikilizaji wao ambao wengi wao kazi yao kubwa ni kushangilia tu!

Sina ugomvi na Waislamu na mtume wao wala dini zingine na waanzilishi wao kwani naamini kwamba ni uhuru wa kila mtu kuamini dini yo yote anayotaka. Hata hivyo huwa nakerwa na watu wanaosimama kidete na kuanza kushambulia dini zingine hata ikibidi kwa kutumia matusi (ya kitashtiti) na udogoshaji. Historia inaonyesha kwamba mashambulizi ya aina hii mara nyingi yana madhara makubwa kijamii hasa upande mmoja unapokuwa hauna subira na uvumilivu. Ndiyo maana tukaonywa kwamba kama unaishi katika nyumba yenye vioo basi kamwe usishabikie mchezo wa kurusha mawe. Dini !!!

Ati,  Ukristo ndiyo dini ya kweli? Uislamu ndiyo dini ya kweli? Uhindu je? Dini zingine nazo? Vipi kuhusu dini zetu za Kiafrika tulizokuwa nazo kabla ya ujio wa Waarabu na Wazungu katika mwambao wa Afrika Mashariki? Kwa kuwa dini hizi tumezichanganya na dini tulizoletewa, je hizi nazo ni za kweli?

Ukiona jamii inaanza kubetuana kwa kutumia misingi ya udini, basi jua kwamba jamii hiyo inacheza na moto na inakoelekea si kwema! Na watu wanaoendekeza na kushabikia haya mambo ya udini (wakiwemo hawa watoa mihadhara uchwara) ni watu wa kuogopwa kama ukoma. Mwenye masikio na asikie !!!

14 comments:

 1. eti wewe uko upande gani wa dini hizi? mimi sina upande na hivyo siumiagi, twambie wewe uko upande upi wa hii mikwara ya maisha yajayoyasiyohalisi (illusion)?

  ReplyDelete
 2. huwa namkumbuka sana mwanafalsafa Voltaire aliyepata kunukuliwa kuwa kama dini zote zinamkiri Mwenyezi Mungu huyo huyo mmoja halafu zenyewe kwa zenyewe zinapingana, basi dini ni ubatili mtupu. Ni maneno ya Voltaire hayo.

  ReplyDelete
 3. Mihadhara imekuwa ikiendeshwa na watu wasio na elimu si ya kawaida, uislam wala ukristo. Kimsingi wahuribiri wengi katika mihadhara hii ni watafuta riziki hasa toka kwa matajiri wa kiaribu wanaounga mkono mgawanyiko wetu ili wafanikishe kisasi chao kwa kuwatimua toka nchini mwetu. Kuna majina kama Mazinge, Mwaipopo ambaye sasa ni marehemu, Ringo na wengine wengi ambao ni vihiyo wa kutupwa. Mihadhara ya kidini ilianzishwa na utawala wa awamu ya pii kama ajenda ya siri ya kueneza uislam. Hii pia ilifanyika ili kuridhisha maimla kama Gadaffi na Ayatollah Khomeini ambao walimwaga pesa nyingi kwa vikundi hivi ili kuhatarisha mshikamano wetu. Pesa hii imezaa wahafidhina wanaowafunika wake zao kama maiti waitwao answar sunna. Hii si mihadhara bali ujinga na ufirauni wa kawaida.
  Kwa upande wa pili kuna wahubiri mbwa mwitu kama Kakobe, Gamanywa, Rwakatare na wengine wengi wanaoibuka kila uchao. Kimsingi, tusipokuwa makini taifa letu litaangamia na hii ni kutokana na kuchagua viongozi wapumbavu kama Jakaya Kikwete na Ali Hassan Mwinyi.
  Taifa letu lina matatizo yake hasa ufisadi na usanii, hawa watu wa mihadhara wapuuzwe hata kuchomwa moto ikibidi ili kuokoa taifa letu.

  ReplyDelete
 4. Ninapita tu.. Annon naona imekuuma sana. Ila nashukuru Mungu kuna upande mmoja una uvumilivu. NA KILA SIKU NINAOMBA WAENDELEE KULISHAMBULIA KANISA KATOLIKI KWA SABABU WAO WAMEONYESHA UKOMAVU NA KUWA DHARAU.
  Nina wasiwasi wakifika kuyashambulia haya makanisa mapya...

  ReplyDelete
 5. Matondo,
  Hayo ni matokeo ya kuwa na demokrasia ndani ya dimbwi la maadui wakubwa watatu nchini( ujinga, maradhi na umasikini) kama walivyoainishwa na Mwalimu Nyerere. Matokeo yake, Jamii inakuwa kama dodoki, hata uchafu unapokelewa na kuhifadhiwa.
  Demokrasia hai lazima iwe juu ya nguzo na mihimili imara ya nchi(bunge, serikali na mahakama)ambayo haina au haitikiswi na hao maadui watatu. Bila hivyo, matokeo yake ni kuwa na demokrasia isiyo na mipaka ambayo inatumiwa vibaya katika jamii inayoweweseka na ujinga, maradhi na umasikini

  ReplyDelete
 6. Waeleze makafiri hao mpaka waelewe hiyo amamni mpaka lini na huu ni mwaka wa 30 mihadhara inaendelea?

  ReplyDelete
 7. MTOA MADA NA WENGINE WALIOCHANGIA HAPA WANA UBAGUZI WA KIDINI,MAANA NAWAONA DHAILI WANA CHUKI NA UISLAM.HILO LIPO WAZI MAANA HAPA NAONA WANAASHAMBULIA WAISLAM NA MARAIS MINYI NA KIKWETE KAMA WATU WABAYA SABABU YA UISLAM WAO!! EBU TUAMBIENI MKAPA NA NYERERE WANA MAZURI YEPI YA KIMALAIKA? MLAANIWE WANAIKI NYIE

  ReplyDelete
 8. matondo asante yaani hii mihadhara ni tabu kweli,pamoja na mijikanisa ya sasahivi maana mwingine akishaokoka hata kuwatembelea ndugu hataki asiye mlokole yy anamwona anamapepo basitabu tu,mimi pamoja ni mwislam lakini ukiwa msikitini kazi ni kulalamikatu tunatengwa,tunabaguliwa,yaani utoto mtupu

  ReplyDelete
 9. Matondo, naona inalalamika waislama kuweka mihadhara na kutangaza kwamba dini yao ndio ya kweli na dini nyengie ikiwemo ukristo sio za kweli! Lakini hulalamiki mihadhara ya kikristo inayoendeshwa na akina SIMBA ULANGA, inayotukana na kukashifu uislam na kumkashfu mtume Muhammad (saw)! Naona umeamuwa kuonesha rangi yako, but at the sametime unajifanya neutral!

  Ndio kawaida yenu, badala yakujibu hoja kwa hoja, mnaishia kuwashambulia watoa hoja! Hivi alokwambia kusoma sana hiyo elimu ya kikoloni (kama wewe ulivyokaririshwa kiima,kiarifu, tungo tata na tungo tegemezi) ndio kuwa mtambuzi wa mambo ni nani? Maana mkiguswa na uislam au waislam.. mnaanza ooh watu wenyewe elimu zao duni? Hivi huyo YESU alikuwa na degree ngapi? Ungefanya la maana kama ungekwenda hapo kwenye muhadhara ukawasomesha hivyo ilivyo sahihi katika kuitafsiri hiyo bible! Au ungetueleza hapa ni kipi walichokitafsiri sivyo? Wao wanasema Yesu si mungu, wanasoma maandiko, Jee hayo maandiko hayapo kwenye bible? Wanasema ukristo si dini ni cheo...je haijaelezwa hivyo kwenye bible? Sasa Matondo "don't hate the player, hate the game"

  ReplyDelete
 10. hakuana dini sasa wamebaki na aibu mashoga wao ndyoo viongozi wa nyumba zao za ibda sasa wanageuki elimu hahahha
  babu zenu wanawataka mu nyote mashoga

  ReplyDelete
 11. mkristo wa kweli na muislamu wa hawazozani kwa hoja za kizembe ni watu wa amani sana

  ReplyDelete
 12. WATAKACHO AMRISHA WAZUNGU TUTAFANYA TAKE TUSITAKE ZOTE PROGRAMME ZAO HAKUNA LOLOTE MI ACHA NISHIKE NILIPOSHIKILIA.

  ReplyDelete
 13. MNAPOLETA LIGI YA UBISHI MUWEKE USHAHIDI, MBONA MATONDO KAWEKA. UKITUAMBIA TU CC TUTAJUAJE?. HAA MFANYAJE NYINYI NI WAAFRIKA TU.NGOZI NYEUSI YENYE KUFANYA MAMBO MACHECHE HAPA DUNIANI MPAKA LEO.KLA KITU MNAIGA MNACHUKIANA

  LAKINI C VYA KWENI HIVI

  ReplyDelete
 14. ndugu matondo alichoonyesha ni jinsi hii mihadhara inavyoandika majina ya wanakwaya wa kikristo huku ndani yake unakuta ni kuukashifu ukristo.na ameonyesha evidence.sasa huyu simba ulanga hatumjui na hatujaonaa evidence yoyote itakayotuthibitishia kuwa kuna mtu anakashifu uislamu na ana jina hilo. kimsingi matondo yupo sahihi.ni vizuri ukiwa mkweli yaani hata dini yako ikiwa haina maana watu wataiona ina maana. kwasababu dini sio jina ni watu.kwahiyo ni watoa hoja msiache kutoa uthibitisho.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU