NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 4, 2011

DAWA YA BABU WA LOLIONDO: MARA INATIBU, MARA HAITIBU...


Dawa hiyo iliwahi kufagiliwa na wataalamu kwamba ni kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. Serikali ikatoa tamko (japo kwa kuchelewa sana) kwamba dawa hiyo haifanyi kazi. Utafiti mpya wa Taasisi ya Synovate unasema dawa hiyo inaponyesha na kwamba asilimia 78 ya waliokunywa wamepona. Sasa yupi anasema ukweli?

Hili siyo jambo la mzaha kwa sababu linahusu maisha ya watu; na kule kwetu Unyantuzu wagonjwa wengi wa UKIMWI wameacha kutumia madawa ya kuongeza nguvu baada ya kunywa kikombe cha babu. Kuna ugumu gani kuwapima watu hawa kama wamepona UKIMWI au bado na hivyo kujua kwa uhakika kama dawa hii inaponyesha ama la? Japo kasi imepungua lakini vikombe vipya vingali vikiibuka. Je, vinatibu?

Hii pia inaonyesha kwa uwazi jinsi tunavyoendesha mambo yetu kimparaganyikoparaganyiko tu. Hakuna umakinifu hata kwa mambo ya muhimu kama haya. Halafu tunashangaa eti ni kwa nini mpaka leo bado hatuna umeme wa kuaminika!

2 comments:

  1. "kimparaganyikoparaganyiko"? Hiyo itakuwa mbaya sana kiutaifa wa Mwafrika. Bahati nzuri mimi sijawahi kuisoma ile RIPOTI mbaya kuhusu KIKOMBE CHA BABU, bali nilisoma ile nzuri tu, na hapo nikaanza kuheshimu ndoto zangu kwani BABU anadai alipata "ujumbe" wake pitia ndoto!

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU