NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, August 26, 2011

FIKRA YA IJUMAA: ETI WAJINGA NDIYO WANAJIAMINI !!!

 • Jamani, wenye maarifa na washika kurunzi wetu mashujaa mko wapi? Mbona mmejaa shaka? Ni nini kilichowafanya mpoteze kujiamini kwenu? Kwa nini mmewaachia wajinga waipalilie mimea japo mwajua wazi kwamba si wataalamu wa kilimo? Mnaridhia kweli ngalawa izame nanyi mpo mwakodoa macho tu? Kwa nini???
 • Bofya hapa kusoma wasifu wa Mwanafalsafa na Msomi Bertrand RussellWikiendi njema wadau!

4 comments:

 1. Ahsante kwa fikra ya ijumaa hii. uwe na wakati mzuri nawe pia.

  ReplyDelete
 2. ahsante sana Prof Matondo kwa fikra hii. ama kwa hakika inafikirisha sana

  ReplyDelete
 3. Ukiidadavua fikira hii kwa hali halisi , mfano mimi kama mhasibu, nasita sana kufanya bishara, kwa kuanza kuangalia hali halisi na je nitapata faida au hasara....lakini mwenzangu ambaye hajui uhasibu kajimwaga, sasa yupo juuu, hajali kuwa atapata faida au hasara....
  Mara nyingi werevu, waliosoma wanakuwa na tahadhari, na hio tahdhari ndio inaitwa `kutokujiamini' lakini wale ambao hawajui, hawana habari ya hiyo tahadhari, wanajitosa kwa lolote liwalo(wanajiamini) ni kwa mtizamo wangu tu

  ReplyDelete
 4. Asanteni. Wakati mwingine inabidi kufunga macho na kutenda.

  Emu-three: Una maoni gani kuhusu kuongoza nchi? Nani ajitose? Anayejiamini au asiyejiamini?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU