NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, August 19, 2011

FIKRA YA IJUMAA: HIVI LENGO HASA LA ELIMU TUNAYOIPATA VYUONI NI NINI ???

 
Nimejiuliza swali hili baada ya kuona orodha ya shahada 20 ambazo eti hazina faida hapa Marekani. Inawezekana kweli shahada ikawa haina faida kwa "msomi" aliyeipata? Tunaupimaje umuhimu wa elimu tunayoipata? Ni uwezo na uwezekano wake wa kutupatia ajira nzuri baada ya masomo au ni ule umuhimu wa elimu kama nyenzo kombozi inayomkaramsha aipataye na kumwondolea woga wa kupambana na mazingira yake? Ati, katika jamii yetu, elimu tunayowapatia vijana wetu ina lengo gani hasa?

1 comment:

  1. Kama kigezo ni pesa, basi labda hizo degree zinaweza kuwa ni useless. Lakini ujuzi na maarifa ya mtu aliyopata kwenye fani yake hatuwezi kuita ni useless. Kwangu mimi degree inakuwa useless pale ambapo mtu hushindwa kutumia maarifa na ujuzi aliyopata kujikomboa na wala siyo kwa kigezo cha kuangalia kiwango cha mshahara.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU