NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, August 8, 2011

HUYU MWANAMZIKI WA KIZAZI KIPYA KUTOKA UGANDA AMENISIKITISHA !!!

Mwana-Fleva Aziz Azion kutoka Uganda

Kwa nini alikubali kutoa hotuba katika lugha asiyoifahamu (vyema)? Kwa nini asitumie lugha yake ya mama au mkalimani kama kulikuwa na ulazima wa kufanya hivyo? Au  naye alitaka kuonekana "msomi" kwa kutema ung'eng'e hata kama umeparaganyika? 

Suala la lugha bado ni tete katika nchi nyingi za Kiafrika na mpaka tutakapoweka mikakati ya kiukombozi na yenye kumakinikia utamaduni wetu, wengi wetu tutaendelea kuadhirika kama huyu msanii mchovu. Ni lazima tujifunze hizi lugha za kigeni lakini tusifikie hali ya kujidhalilisha na kuzidharau lugha zetu za Kiafrika - lugha zilitotukuza na kutuonyesha ulimwengu. Ningefurahi sana kama angetema Kiganda na kuwaacha watu wasiokifahamu wameduwaa. Pengine nao ingewabidi waende wakajifunze Kiganda. Utumwa wa fikra huu sijui utatuisha lini sisi Waafrika. Soma kisa chake hapa chini.

************

Msanii Uganda...Hajui Kiingereza Kabisaaaaaa ...!


Msanii Aziz Azion toka Uganda,aliumbuka alipokua analazimisha kuongea ung'eng'e wakati hajui wakati anatoa speech pande za Serena Hotel kwenye uzinduzi wa Jarida la Black Flavour aka Black Flavour Magazine


Aziz Azion alialikwa kama guest performer na MC alipomuomba atoe speech kidogo kuhusiana na jarida hilo, alikamata mic na kuanza kujiuma uma kidogo apate ugonjwa wa moyo coz aliongea broken english kabla ya kuhamia kwenye lugha yake ya taifa ya Luganda. Artist huyo alifunguka longtime kitambo kuwa ameanza English Course ili ajifunze ung'eng'e....Coz aliripotiwa kuwa hawezi kabisa kuongea lugha hiyo....

Chanzo:  Chini ya Kapeti

*********************
Angalizo Zaidi


Hata hii lugha iliyotumiwa na huyu Chini ya Kapeti hapo juu nayo ni changamoto tupu....

1 comment:

 1. Mkuu, watu wengi tunaamini kuwa "umaarufu" maana yake ni kuwa "Mzungu Mweusi" (na ndio maana, kutoka nje ya tundu kidogo unakuta tunaifia hotelini badala nyumbani kwetu au hospitalini tukiwa na mapesa kidogo).


  Kazi tunayo, maana yake Afrika Kusini hapa zipo nyimbo nyingi zaKiswahili chetu aliyetunga na kuimba Mswahili mmoja kiasi cha kufurahisha hata Malkia Wa Wingereza Elizabeth II.


  Inasemekana, hajawahi mwanamama huyu kufurahia wimbo wa msanii kiasi cha kuacha kiti chake ili ashangilie kwa makofi; lakini ndivyo alivyofanya wakati wa tumbuiza moja ya huyu mwanamziki (naomba nisimtaje jina).


  Hadi siku yake ya kifo, mwanamziki huyo alijigamba kwa Kiswahili chake!


  Tatizo sasa ni hili, kwakuwa sasa kila mwaka Afrika Kusini nyimbo zake zinapata tuzo, huyu mmoja katika wake anakujaga kutoa hotuba ya kushukuru, ndipo anakivunja Kimombo na atatumia mara tatu au zaidi ya muda aliepewa huku mwenyekiti wa shughuli anaogopa kumkatisha kwani ataonekana eti "katili kwa mjane"!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU