NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, August 31, 2011

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA (KUJIVUA MAGAMBA) NA SASA TUNASONGA MBELE !!!

Hii kauli mbiu ya CCM kule Igunga kwa Rostam Aziz imenivutia. Ina maana ile operesheni ya kujivua magamba imeshakamilika? Kama jibu ni ndiyo basi hili ni jambo jema kwa WanaCCM na bila shaka uchaguzi wa Igunga utakuwa pimajoto mojawapo kuona jinsi operesheni hii ilivyopokelewa na wananchi. Tunaomba tu uchaguzi huu mdogo wa Igunga usikumbwe na kashfa zozote za uchakachuaji wa kura na badala yake uwe huru, wa haki na amani!

3 comments:

 1. Kazi ipo!:-(
  MUNGU IBARIKI TANZANIA!

  ReplyDelete
 2. Mtakatifu - Mungu Keshaibariki Tanzania kwa kila kitu. Kazi ni kwetu kupiga akili jinsi ya kuitumia akili hiyo ili kuhakikisha kuwa mibaraka hiyo inatuletea maendeleo ya wengi....

  ReplyDelete
 3. Thank you for the information.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU