NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, August 14, 2011

UJUMBE WA LEO: WEWE NDIWE !!!

Kwa hili nakubaliana kabisa na Dr. Seuss. Kuishi kwa kujaribu kuwafurashisha watu wengine ni kazi bure. Mbali na ukweli kwamba jambo hili haliwezekani lakini pia mara nyingi watu hawa unaojaribu kuwafurahisha hata si watu wa muhimu kwako na kusema kweli hawajali. Ati, wawezaje kumfurahisha binadamu mwenzako ambaye mwenyewe hana furaha? 

Wewe ndiwe na hakuna mwingine kama wewe hapa duniani. Itupilie mbali hofu na kawe na furaha Jumapili hii njema.

6 comments:

 1. Nimekubaliana 100% na ujumbe wa leo . mimi ni mimi hakuna mwingine..na wewe ni wewe, yule ni yule na yeye ni yeye hakuna haja ya kufanya kitu kwa kufurahisha wengine...Ahsante sana kwa ujumbe wa jumapili hii.

  ReplyDelete
 2. Ujumbe safi kabisa

  ReplyDelete
 3. Naombea MAFISADI wasisome ujumbe huu!:-(

  ReplyDelete
 4. Da Yasinta - ni kweli. Binadamu tunayo tabia ya kujidogosha na kujifanya tusioweza mambo, kwamba eti kuna wengine ambao ni wa muhimu zaidi yetu pengine kwa ajili ya utajiri, madaraka au umaarufu walionao. Hili si sahihi.

  Tumaini - asante. Ukweli ni kwamba hakuna Tumaini Munale mwingine hapa duniani.

  Kamala - huu si ujumbe wangu. Ni ujumbe wa Dr. Seuss. Unaweza kumsoma zaidi katika link hiyo juu.

  Mtakatifu - Kwa nini unataka mafisadi wasisome ujumbe huu?

  ReplyDelete
 5. @Mkuu Matondo: Ili kwa bahati mbaya wasijiamini sana kwa wafanyayo na wasemayo katika ulaghai kwa walalahoi kutokana na ujumbe huo hapo juu wa Dr.Seuss

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU