NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, September 1, 2011

ATI, "UTALII" NDIYO MAFANIKIO (PEKEE) YA J.K. KWA WATANZANIA ???

Katuni hii ya Said Michael imenifikirisha pamoja na ukweli kwamba pengine imedhamiriwa itazamwe kama kejeli au tashtiti (satire) tu. J.K. ameshaandamwa sana kuhusu safari zake za mara kwa mara na mjadala mkali uliowahi kurindima kuhusu suala hili ni ule ulioanzishwa na Profesa Mbele

Japo sijakisoma kitabu cha Wasifu wa Kisiasa wa J.K na kuona yanayosemwa humo, leo mtu angekuuliza utaje mafanikio na urithi wa J.K. kwa Watanzania ungetaja vitu gani mbali na "utalii" kama katuni hii inavyokejeli?  

5 comments:

 1. Pengine yawezekana utalii ndo sera..

  Ama kilimo kwanza ambayo ni sera ya kujiuza na kujiweka rehani kwa makampuni ya kimarekani na ulaya ya mbolea na mbegu kama syngenta, monsanto nk huku mifumo yetu ya jadi ya kuhifadhi na kupeana mbegu pamoja na mbegu zetu za asili kupotea na kufa kifo chema :-(

  Baada ya hapo tutashuhudia GM seeds bariadi...lol!

  ReplyDelete
 2. Mojawapo ya mafanikio ya JK ni hayo uliyonayo, nalo ni Uhuru wa Kujieleza, au freedom of speech ambavyo wengi wetu tunaona kuwa si lolote si chochote lakini kumbuka himaya ya Ghadafi iliangushwa si kwa watu wake kuwa na maisha ya chini bali kwa kukosa huo uhuru wa kuongea ambao sisi tunao na hatuuoni kama ni wa maana. Labda tukirudishwa kule enzi ile kila mtu alipokuwa anamuogopa jirani yake yaweza kuwa ni shushushu ndio tutaona umuhimu wake.

  Pili kwenye maeneo ambayo yalipendelewa na kuwa na huduma zote muhimu hawawezi kuona lolote la maana lililofanywa na JK lakini kwenye maeneo ambao elimu ilikuwa privilegde ya wachache hata hizo shule za kata zinaonekana za maana. Kwa hiyo uwepo wa shule za kata, na huduma za afya ni mafanikio mengine.

  Tatu demokrasia ya vyama vya siasa ambavyo miaka michache nyuma tu watu hawakuruhusiwa kukutana wala kuandamana wala hawakuwa na uhuru wa kufuata chama wanachokitaka na tukashuhudia wafanyabiashara wakiingia CCM ili kulinda biashara zao na ubabe wa wakubwa. Leo hii CUF, Chadema na vyama vingine na wanachama wao wana uhuru wa kufanya watakalo bila kuogopa virungu mabomu au kuuwawa na polisi kama maujaji ya Pemba na Unguja na maeneo mengine enzi ya Mkapa.

  Kubwa ni kuwaunganisha wazanzibari na kukubali kuundwa serikali ya umoja huko Zanzibar. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni huu mgogoro wa miaka dahari sasa umekwisha.

  Kinachonishangaza kwenye hiyo katuni inaonyesha kuwa Mwinyi hakufanya la maana wakati yeye ndiye baba wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi, na hata Mkapa alipokuta uchumi umeshatoka kwenye umauti ndipo ufisadi ulipoanza, mimi naweza kusema Mkapa ni baba, mwanzilishi na msimamizi wa UFISADI kwani alifanya biashara Ikulu. Kipo kinachowafanya mumuone Mkapa amefanya mazuri tu na Mwinyi na JK wao ni mabaya tu, uzuri kila mmoja wao kaacha alama zake hazifutiki.

  ReplyDelete
 3. kunakitu sikielewi, hivi JK kaleta uhuru wa kujieleza au nykati tunazoishi hizi ni za uhuru wa kujieleza na hamna awezaye kuubana uhuru huo kwa njia yoyote ile?

  ReplyDelete
 4. Nenda kaishi Uganda au Rwanda au unafikiri huko kwa Ghadafi wanagombea nini. Jaribu pia nchi zilizoendelea, kuna cctv na hacking kila mahala, jaribu kusema tofauti kama hujajikuta uko kwenye matatizo. Labda jaribu nchi za middle east kama Bahrain na Saudia au far east kama China, pengine uende Russia au Georgia ukaone uhuru wa kujieleza walionao.

  Au mwambie tu huyo rafiki yako Matondo aanze kuandika against US government kama watarenew visa yake. Kama kuna uhuru hujiulizi kwanini wako busy kuhack simu na computer za watu, na ni juzi juzi tu vijana 2 wamefungwa 4 years kwa walichokiandika kwenye fcbk.

  ReplyDelete
 5. Ng'wanambiti: Pamoja na matatizo yote, ina maana hakuna lolote jema ambalo JK kafanya? Au ni kwa vile wanaCCM - hasa wa kipindi hiki ni wazito kuelezea mafanikio yao. Ni kama vile wanaona aibu. Mimi ni mmoja wa wale wanaoamini kwamba kila kitu kina pande mbili kinzani na pande hizi zinakamilishana. Ndiyo maana huwa nakerwa sana na watu wanaojibana katika upande mmoja tu bila kuangalia upande wa pili...

  Anony wa kwanza. Umeainisha vizuri. Hili la uhuru wa habari na kujieleza nadhani ni mwafaka zaidi kiasi kwamba watu wengine wamefikia hata kusema kwamba pengine linatumiwa vibaya. Uhuru huu umezidi kiasi kwamba hujui ipi ni habari ya maana na ipi ni minong'ono au udaku tu usio na ukweli. Kila mwanasiasa ni fisadi, kila kiongozi ni mbadhirifu, kila kitu kuhusu CCM ni kibaya. Siwatetei mafisadi lakini kama kweli tumefikia hatua ya kuwa na viongozi wote wabovu basi ni wazi tumepotea njia. CCM na serikali yake badala ya kueleza mwelekeo na mafanikio yao wanajikalia kimya tu na kuacha minong'ono na udaku vinaenea. Hata hii operesheni ya kujivua magamba nadhani haikueleweka vizuri na sidhani kama imesaidia sana kujirudishia heshima. Habari za ufisadi na ubadhirifu wa mali zinapotolewa inabidi zikanushwe mara moja kama siyo za kweli na kama ni za kweli na wanaozitoa kama wana ushahidi basi hatua zichukuliwe. Badala yake sasa ni vurugu tupu na huwezi kujua yupi anasema ukweli. Ni sababu hii hii iliyonifanya mpaka nifikie hatua ya kuhoji ufisadi wa mbunge wangu baada ya kumwandama sana(http://matondo.blogspot.com/2011/08/mbunge-wangu-kweli-ni-ngombe-mwenye.html). Niligundua kwamba pengine nami nilikuwa najiingiza katika udaku tu!

  Kamala: Anony wa mwisho ametoa mifano mizuri. Ndiyo - hata katika kipindi hiki cha mtandao, uhuru wa kutoa maoni bado unaweza kubanwa. Hata hapa Marekani, ukianza kuisakama serikali sana usije kushangaa FBI wanakufungulia faili na kuanza kuchunguza nyendo zako. Uhuru upo lakini ni lazima uwe na kikomo.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU