NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, October 1, 2011

MSIKILIZE MAREHEMU NG'WANAKANUNDO HAPA CHINI - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

  • Mimi ni mkereketwa wa masuala ya kitamaduni hususan lugha zetu za kienyeji ambazo leo hii tumetokea kuzidharau na kuziona kuwa hazina maana wala nafasi hasa katika ulimwengu huu wa "kisasa" . Kumbe kwa kufanya hivyo tunazidi kujididimiza, kujidharau na kuendelea kujitwanisha kwa tamaduni za wenzetu.
  • Tunajipoteza sisi wenyewe na tunapoteza nafasi nzuri sana ya kuweza kuwaelimisha watu wetu hasa katika masuala na kampeni mbalimbali za muhimu kijamii. Kwa wanaofahamu Kisukuma, hebu msikilizeni huyu Manju anavyoonya kwa ufasaha kuhusu gonjwa hatari la UKIMWI na umuhimu wa kupanda mazao yanayohimili ukame kama mtama na mihogo kama mkakati wa kujikinga na balaa la njaa. Mbona tusitumie lugha zetu za kienyeji katika kampeni za kijamii kama hizi za UKIMWI, magonjwa kama kipindupindu, malaria na mengineyo? Kuna ubaya gani?

1 comment:

  1. watungilija,natogwa sana I lyimbo.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU