NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, December 31, 2011

KATI YA HAWA KUNA RAIS WETU MWAKA 2015 !!!

...Wanasiasa vijana wanaotajwa ni pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye.


Katika kundi la umri wa kati wapo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye,  Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro.


Kundi hilo pia linawajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe.

Katika kundi la wenye umri zaidi ya miaka 60 wanaotajwa ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.....

Chanzo: Mwananchi

2 comments:

 1. Kundi la kwanza hakuna hata moja anayefaa. Na hasa Ngeleje kwani bado ana kesi ya kujibu.Nape saizi yake ni udiwani.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Bwana Matiya. Bila shaka mwaka mpya unaendelea vyema huko Ufini....

   Katika siasa kila kitu chawezekana. Kwa maoni yangu wote waliotajwa hapo juu wanaweza kuukwaa urais bila wasiwasi wo wote.

   Umesahau kwamba Nnape alikuwa mkuu wa wilaya (na siyo diwani) kabla hajateuliwa kueneza cheche za CCM nchi nzima?

   Delete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU