NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, December 28, 2011

MAISHA YA KUMBUKONI - WAKUMBUKE WAZAZI (NA KILIMAMBOGO BROTHERS)

 • Nyakati zile kulikuwa na jamaa mmoja pale kijijini kwetu mwenye baisikeli iliyoandikwa "Kaminomino Mpenda Wasichana. Uliza Sababu Yake". Huyu jamaa alikuwa mashuhuri sana na ndiye pekee alikuwa na redio yenye uwezo wa kucheza kanda za kaseti. Ndipo nilipozisikia nyimbo hizi za Kakai Kilonzo na Kilimambogo Brothers kwa mara ya kwanza. 
 • Nashangaa kwamba hata baada ya miaka zaidi ya 20, ujumbe katika nyimbo hizi ungali hai mno. Ni kosa kubwa kukimbilia mijini au huku nje na kuwasahau wazazi waliotulea na kutusomesha hasa kwa sisi tuliotoka vijijini. Tuwakumbuke wazazi !!! 

2 comments:

 1. Mtu kwao, Bwana! Kama wewe unataka kusahau unakotokea basi wewe ni mjinga wa kutupwa! Utaeleweaje unakoelekea kama hujui unakotokea?


  Ila mimi Mkuu ninalo swali kama Msoweto. Kwanini ujumbe kwa wanamama huandikiwa kwenye kanga na kwa wanababa kwenye baiskeli?


  Nani ameanzisha au kushawishi mifumo kama hiyo? Mbona napendekeza apewe udaktareiti kabisa kwamba yeye ni msomi kuliko wasomi wote wa kawaida!!!


  (Kama wewe hapo, Mkuu, usiekuwa na aibu kutueleza chimbuko lako!)

  ReplyDelete
 2. Ahsante kwa ujumbe muruwaa kaka Matondo,wazazi/walezi ni kuwaenzi.Baraka kwako na wote!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU