NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, December 19, 2011

WANABLOGU WENZANGU NA WAPENZI WOTE WA KWELI WA BLOGU HII: SASA NIMERUDI RASMI !!!


Wapendwa wanablogu wenzangu na wapendwa wote wa blogu hii. 
 • Kwanza nianze kwa kuwaomba msamaha kwa kupotea bila kuaga. Wakati mwingine misukosuko ya maisha, kama vile dhoruba isiyo na soni wala utashi, hutuvamia na kututupa huku na huko mithili ya tiara iliyokatikiwa kamba au mtumbwi hafifu katikati ya dhoruba ya karne! Wasimamao tisti na kupigana kiume (kike?) hubakia na "viburi" vyao na tabasamu la ushindi baada ya dhoruba na misukosuko hii ya maisha. Nami nimepita dhorubani humo, nimeyaona niliyoyaona na kujifunza niliyojifunza, na kama vile chuma kilichopita tanuruni - kikafuliwa na kung'arishwa mithili ya kioo, nimetoka salama. Maisha ni lazima yaendelee ati - tena kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Maisha !!!

 • Na kwa tangazo hili napenda kuwaataarifu rasmi kwamba sasa nimerudi na kuanzia sasa mambo yatakuwa motomoto katika blogu hii. Na jicho na sikio langu sikivu sasa vitaonekana tena katika blogu zenu pendwa - kama kawaida vikiona na kudodosa yanayotokea huko. Tuko pamoja daima !!! 
 • Natumaini mambo yanaendelea vyema huko mliko. Hebu mwaka huu na ukaishe kwa amani na salama; na sote tukaweze kuuona mwaka mpya wa 2012 ingawa sina uhakika sana kama kuna faida yo yote ya kufanya hivyo. Maisha !!!

11 comments:

 1. Maisha! Ni furaha kusikia kutoka kwako ni kweli ulipotea bila kuaga(uliaga bila kupotea) karibu sana tena sana .Maisha

  ReplyDelete
 2. Ndugu Masangu, nimefurahi kuona umerudi kwa kishindo. Tunasubiri kwa hamu zawadi za father christmas, hapa kwetu wafini wanamwita Joulupukki!

  ReplyDelete
 3. Karibu tena katika ulimwengu huu wa mawasiliano

  ReplyDelete
 4. Tumefurahi kukuona tena kaka Matondo,Mungu wa Upendo azidi kuwanansi daima,Karibu sana kaka.PAMOJA!!!

  ReplyDelete
 5. Inaelekea ulikuwa mbali sana...unarudi umeota mvi hata kwenye ndevu???!! Pole sana!


  Lakini sisi tunakukaribisha; na hamna haja ya kuomba msamaha. Kimya yako kwetu ni kama kobe alieyeinama kiHenga... "anatunga sheria" au anawahudumia wengine nao wanaotaka kufaidi mawazo yake!


  Ubarikiwe kwa wakati huu mtakatifu wa Krismas!

  Karibu tena!

  ReplyDelete
 6. Ulipotea kwa kweli Profesa, karibu tena. Mimi sikuachi hadi umenijibu swala langu nililokuwa nauliza tangu umepata mushkeli na gmail, sasa ngoja nikakutumie ujumbe wenyewe kwenye email yako.

  ReplyDelete
 7. Kwanza karibu Santa Kalausi ng'wana wa Paliati.Bwana Matondo umefumba sana. Twambe nini kilikusibu maana kama ni maisha wote tunaishi. Hata hivyo nimefurahi kusikia kuwa umerudi tena jamvini. Ila nakushauri usije kwa kasi mpya nguvu mpya na ari mpya bali kwa mara nyingine. Nimefurahi ulipopita pale kibarazani kwangu ukamwaga "razi" na kuishia.Nami napita nikotoka Libya kumzika Gaddafi. Naelekea Pyongyong kabla ya kuelekea Danganyika kumfariji Kafulia. Karibu tena kilingeni tufungiane nyama sawa na farasi na nyangwa.

  ReplyDelete
 8. Nyote - asanteni sana kwa kunikaribisha. Da Subi...usihangaike. Nitakutafuta mwenyewe na usije ukashangaa nikibisha hodi mlangoni kwako.

  Mwalimu Mhango - kauli mbiu ya kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya ilishachujuka na kutupwa jalalani. Matunda yake hukuyaona/huyaoni?

  Naona una mizunguko mingi. Kampe mikakati mipya Kafulila ili aweze kunusuru ubunge wake. Haiwezekani posho ndo tu ziongezwe halafu wamtose.

  Bwana Matiya - Huyu Joulupukki hana jipya huyu na hahusiani kwa namna yo yote ile na lengo la sikukuu yenyewe. Utamuweza binadamu kwa kugundua mambo yasiyo na maana? Baridi vipi huko, ishaanza? Poleni!

  ReplyDelete
 9. siku nyingine unaaga sio kwenda kimya kimya vinginevyo hutusameheka

  ReplyDelete
 10. mie bado mpotevu kwa hiyo mie nafurahi tu mwenzangu katoka huku msituni na kaja huko mujini kwenye mablogu. inshallah nami nitakuja huko mujini

  john mwaipopo

  ReplyDelete
 11. Heri ya Krismasi na Mwaka mpya wewe pamoja na familia yako. Umenitoa nishai kama waswahili wasemavyo kusema ukweli umevunja rekodi ya mwaka. Santa Clause asilia anapatikana kwenye kibaraza hiki. Vinginevyo ma- Santa Clause wengine ni foto- kopi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU