NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, December 21, 2011

WANAFUNZI HEBU SOMENI UTAFITI HUU: ETI KUTAFUNA BAZOKA DAKIKA TANO KABLA YA MTIHANI HUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU.

 • Tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba kutafuna bazoka (gamu/bigiji/chingamu/ubani wa kutafuna) kuna faida katika kuimarisha afya ya kinywa na hata jitihada za kupunguza uzito wa mwili na msongo wa mawazo. Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la kitaaluma la Appetite unaonyesha kwamba kutafuna bazoka dakika tano kabla ya mtihani kunawasaidia wanafunzi kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao kuliko wenzao ambao hawakufanya hivyo.
 • Utafiti huu unaonyesha kwamba kutafuna bazoka kunachangamsha na kusisimua ubongo na kufanya wanafunzi wakumbuke vitu vizuri na kwa urahisi; na hivyo kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao.
 • Utafiti huu pia unaonyesha kwamba kutafuta bazoka wakati wa mtihani wenyewe kunaweza kuingiliana na shughuli za ubongo za kufikiri na kukumbuka mambo na hivyo kuwafanya wanafunzi kufanya vibaya katika mitihani yao.
 • Wanasayansi hawa pia wanaonya kwamba wanafunzi wasitegemee kutafuna bazoka dakika tano kabla ya mitihani yao ili kufaulu. Wanabainisha wazi kwamba kutafuna bazoka kunasisimua tu kumbukumbu na mambo ambayo mwanafunzi tayari ameshajifunza, kujisomea na kuyahifadhi ubongoni mwake. Kama wanataka kufaulu mitihani yao, wanafunzi ni lazima wajisomee na kujiandaa vizuri kwa ajili ya mitihani yao.
 • Vidokezo vizuri kuhusu jinsi ya kujiandaa kufanya mitihani vinapatikana HAPA. Habari za utafiti huu zimedokezwa HAPA

3 comments:

 1. Kaka Matondo mie ninakubaliana kabisa kabisa na utafiti huo. Mimi mwenyewe nikiwa katika mitihani nimezowea sana kutafuna bazoka. Mimi huwa inanipa kujiamini na kuamsha kumbukumbu kwa kiwango kikubwa sana. Hata wakati naandika riwaya ama mashairi nimezowea kufanya hivyo huku nikitafuna. Si hayo tu, hata nikiwa ninakabiliana na jambo zito linalonipasa kukutana na mtu hupenda kutafuna bazoka. Huwa naitema dakika chache kabla ya kuanza mazungumzo. Ni miaka kumi sasa toka nijifunze tabia hiyo.
  Leo nimefurahi sana kuona hili jambo pia limeelezwa kisayansi na watafiti.

  ReplyDelete
 2. Siku hizi tusiamnini kila kitu chenye "kutolewa na wanasayansi" wa huko ugenini, bali nasi tujifikirie wenyewe, hasa sisi Waafrika ambao mili yetu ni dhaifu (COMPARATIVELY HIGHLY SENSITIVE) kuliko makabila mengine ulimwenguni.

  Mbona zoezi lolote lile lingine (hata mchakamchaka kabla ya mtihani) lazima litakuongeza kiwango cha kufikiri?


  Nani asiejuwa A HEALTHY BODY= A HEALTHY MIND?

  Wanasemaje hawa wanasayansi kuhusu kupumbazwa kwa watoto wa shule juu ya matumizi ya sukari IN GENERAL? Na iko wapi duniani CHEWING GUM isiekuwa na sukari?  Wanasayansi nao wameshaanza kujiuza kwa bidii, siyo? Hao Wrigley's wamewapa mamilioni ngapi wanasayansi hao ili kuwatangazia kwa watoto bidhaa yao hiyo haramu?


  Mimi, Mwanangu (kama wewe ni mtoto unaesoma hapa), sie mwanasayansi lakini nasoma kila siku kuhusu afya na mambo ya biolojia hasa ile yenye kumhusu mtu mweusi. Chagua wewe mwenyewe utawasikiliza hao "wanasayansi" au mimi, uko huru kabisa!

  Lakini nasema:


  Hii sikweli kabisa kwamba ukitafuna uchafu huo ndipo pekee unapata akili...badala yake utapata pia vikohozi na utatembea huku unavuta makamasi bure;


  Utapungukiwa na heshima zako watu wakuone mwehu kutafuna kitu kinachowachafulia viatu vyao kila wakikikanyaga na kama wewe ni msichana wavulana wastaarabu hawakutongozi nikwambie!


  uwezo wako wa mwili kujitetea na magonjwa utadhoofika;


  nguvu za akili yako zitapunguka kitu kama dakika 30 baada ya kupata kila msisimuo au HIGH iliokuja kutokana tu na sukari ndani ya huo ugoro wa ng'ambo;


  na kama wewe kweli ni kijana TEENAGER utazidi kuwashwa na damu za ujana wako (HORMONES) kwa hiyo utakuwa mtundu na kutojielewa (RESTLESS, ANXIOUS AND DEPRESSED) na vilevile kutaka kujihusisha na mambo ya ngono ungali bado mdogo;


  sigara bangi na madawa ya kulevya wewe juwa kabisa uko mbiyoni tayari kutumia;


  utakuwa mgumu kuwasikiliza wazazi ama walimu wako;


  Utapata NA MATATIZO MENGIMENGI TU (tena zaidi ya mia-100)YANAO ONGOZANA NA MATUMIZI YA SUKARI!

  So, whatever little good comes from exercising your chewing muscles pales in contrast to the evil that accompanies the chewing gum sweetened by sugar or artificial sweeteners... CHUNGA SANAAAA!

  ReplyDelete
 3. Fadhy - nyie waandishi na wanafalsafa mna mambo yenu yanayowapa msukumo. Albert Einstein ilikuwa ni kuvuta mtemba na kutembea kimya kimya hasa nyakati za jioni, Pablo Neruda ilikuwa ni kwenda ufukweni na kuangalia mawimbi na ukubwa wa bahari...Hili la kutafuta gamu mimi nilikuwa silijui.

  Manyanya - Huwa napenda kusoma maoni yako kwa sababu daima huwa unakwenda kwa undani sana na kuyaangalia mambo katika upana wake.

  Waafrika ni lazima tuzitathmini hizi tafiti zinazotoka nchi za Kimagharibi kwa jicho la hati hati kwani mara nyingi huwa hazizingatii tamaduni na mazingira yetu. Na kama ulivyogusia hapa, tafiti nyingi zinagharamiwa na makampuni yanayotengeneza bidhaa zao. Kwa hivyo si ajabu kusoma utafiti uliofadhiliwa na kampuni la sigara la Marboro ukionyesha kuwa madhara ya sigara yametiwa chumvi tu ili kuwaogopesha watu. Makampuni ya kutengeneza madawa, kwa mfano, yana tabia hii mbovu ya kuajiri madaktari wazuri kisirisiri ili tu waweze kuandika ripoti nzuri na kuwashauri wagonjwa wao kutumia madawa yanayotengenezwa na makampuni hayo.

  Pamoja na haya yote, hatuwezi kujitenga kabisa na kukataa kila utafiti hasa ukizingatia kuwa kwetu suala hili la kufanya utafiti wa kina bado hatujalitia maanani sana. Ni lazima kujihadhari!

  Na kama wanayosema ni kweli, nadhani sasa kuna gamu ambazo hazina sukari (Sugarless). Hizi zimetengenezwa kwa kutumia vitamuishi mbadala kama vile Splenda. Tatizo ni kwamba vitamuishi hivi mbadala navyo inasemekana vina madhara makubwa ya kiafya kuliko hata hiyo sukari yenyewe!

  Tumwamini nani sasa? Wanasiasa wetu? Wanasayansi wetu? Wasomi wetu? Nani ???

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU