NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, June 30, 2011

WANAUME NI WATUMWA WA NGONO ?

Ati, ni kosa kwa huyu mwanafunzi kuwaza haya anayoyawaza?
Inasemekana kwamba Sigmund Freud aliwahi kusema kwamba fikra za mwanaume na karibu kila kitu anachokifanya vimetawaliwa na ngono; na kwamba eti mwanaume huwaza ngono kila baada ya sekunde saba

Japo takwimu hizi zinaonekana zimetiwa chumvi lakini zinatosha kuonyesha jinsi ambavyo ngono imetawala maisha ya mwanaume. Kuhusu utafiti unaotoa fununu juu ya uzinzi wanaume bofya HAPA

Nimemkumbuka Sigmund Freud baada ya kusoma kisa hiki cha Ben kutoka katika gazeti la wanafunzi hapa chuoni. Naogopa kupoteza utamu na hivyo sijakitafsiri.
*******************
A man and his wife are in the shower together when the doorbell rings. The wife puts on a robe and goes down to answer the door. In walks her husband’s friend Ben. The woman tells him that her husband is in the shower and asks if he can come back later.

nstead, Ben steps in and quietly says, “I have $400 in my pocket. I will give it to you if you will open your bathrobe for me.” She is offended, but really needs the money, so she agrees, opens her robe, and lets Ben have a quick peek before doing it up again. Ben gives her the $400, and she opens the door for him to leave, but he says, “I have another $400 in my other pocket. I will give it to you if you let me touch your breasts.” Now she is really mortified, but again, she needs the money, so she undoes her robe and lets him have a quick feel. Taking the other $400 from him, she lets him out of the door.

Going back upstairs, she gets back in the shower with her husband, feeling a little bit guilty.

“Who was that?” the husband asks.

“Oh, that was just Ben,” the wife answers

Ben?” the husband says. “That son of a bitch owes me 800 bucks!”

*******************
Wanaume mpo? Hatuelezwi kilitokea nini kati ya wanandoa hawa. Kama wewe ndiye mume wa huyu mama halafu mama awe na ujasiri wa kukupa stori nzima kumhusu rafikiyo Ben, ungefanya nini? Ni kweli kwamba wanaume sisi ni watumwa wa ngono? Ukiombwa useme ukweli, utajibuje swali hili: Wewe huwaza ngono mara ngapi katika sekunde, dakika, saa, siku, juma, wiki, mwezi, mwaka, muongo, karne, milenia moja?

Wednesday, June 29, 2011

SIMU ZA MKONONI NA KANSA YA UBONGO: BALAA JINGINE KWA AFRIKA?

Picha hii iko HAPA

Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala mkali kuhusu nguvu za mionzi ya mnunurisho inayotolewa na simu za mkononi kama zinaweza kusababisha kansa ya ubongo ama la. Hatimaye Shirika la Afya Duniani limetoa tamko kuhusu utafiti unaoonyesha kwamba simu za mkononi zinaweza kuwa zinasababisha kansa ya ubongo. Hatari hii inasemekana kuwa ni kubwa zaidi kwa watoto wadogo na matineja kwani mafuvu yao bado hayajakomaa sawasawa.

Naomba hii isiwe kweli kwani kama tunavyojua, Afrika ndiyo jalala la bidhaa feki, mbovu na zilizoisha muda wake. Bila shaka nitakuwa sahihi nikisema kwamba simu zinazotoa mionzi hatarishi kwa binadamu na zitakazokuwa zimepigwa marufuku sehemu zingine za dunia ndizo zitarundikana Afrika.

Kama utafiti huu ni wa kweli basi miongo kadhaa tu ijayo Afrika itakumbwa na mripuko wa kansa ya ubongo – mojawapo ya kansa hatari kabisa na inayohitaji tiba ghali sana!

Tunachoweza kufanya kwa sasa ni kufuata mapendekezo yaliyotolewa yakiwemo kununua simu zisizotoa mionzi mikali zaidi, kuweka simu mbali na sikio wakati wa maongezi na kwa wenye uwezo kununua vifaa vinavyosafirisha mawimbi ya sauti kama “Bluetooth”. Vifaa hivi huwekwa sikioni na vinaweza kudaka mawimbi ya sauti ya simu iliyowekwa mfukoni au sehemu nyingine na kuyasafirisha sikioni kwa msikilizaji bila madhara yo yote.

Aina mojawapo ya kifaa cha bluetooth

Hizi simu feki kutoka Uchina zitatufikisha pabaya. Ndiyo maana naomba hili la simu za mkononi kusababisha kansa ya ubongo lisiwe la kweli. Mungu Ibariki Afrika!

Tuesday, June 28, 2011

HARAKATI ZA CCM KUJIVUA GAMBA ZITAMALIZIKA LINI ? NI ZOEZI LA KUDUMU ?

Ili kuepuka kuwa mmezwaji huko mbele ya safari, CCM ilibidi kijivue magamba

Juhudi za CCM kujivua gamba zilipokelewa kwa furaha na matumaini makubwa na wanachama wake pamoja na Watanzania wengine wakipendacho. Japo juhudi hizi zilipondwa na kubezwa na baadhi ya wapinzani pamoja na wachambuzi, kwa wengi zilionwa kama nafasi ya pekee kwa CCM kujaribu kurudisha imani yake kwa wananchi - imani ambayo ilikuwa imeanza kupotea kutokana na tuhuma za ufisadi na makundi ndanimwe; pamoja na kupoteza mwelekeo na malengo yake ya msingi. 

Ilitangazwa kwamba CCM ilikuwa imetoa siku 90 kwa watuhumiwa wote wa ufisadi kujiuzulu uanachama na kama wasingefanya hivyo basi wangewajibishwa. Kauli hii ilionyesha kwamba kweli chama hiki kilikuwa kimedhamiria kujisafisha. 

Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya muda kidogo tu kupita wakuu wapya wa chama hiki walitangaza kwamba hawakuwa na majina ya mafisadi na kwamba ile kauli ya mwanzo ya siku tisini haikuwa ya kweli. Baada ya kigugumizi cha muda mrefu kuhusu mashambulizi ya CHADEMA, hatimaye CCM wameamka na kupitia kwa Katibu wao Mwenezi wanazunguka nchi nzima kujibu hoja za wapinzani wao na kuelezea mafanikio yao. 

Japo kuzunguka kwa CCM nchi nzima ni mkakati mzuri, sina uhakika kuhusu mafanikio yake. Ni kweli kuzunguka huku kunasaidia kurudisha heshima na imani ya CCM kwa wananchi? CCM imefanya tathmini na kujua wananchi wanataka nini? Isije ikawa kwamba juhudi hizi za kijasiri za Katibu Mwenezi zinaonwa na wananchi kama propaganda tu za CCM walizozizoea. 

Kwa maoni yangu naona kuwa CCM inapoteza nafasi ya muhimu sana ya kuonyesha dhamira yake ya kujisafisha mbele ya Watanzania kwa vitendo. Kama kweli ilikuwa imedhamiria kujivua gamba, mbona kazi hii ifanyike nusunusu? Ndiyo maana nimeshangaa kusoma leo katika Gazeti la Chama na Habari Leo CCM ikitoa ahadi nyingine kwamba wasaliti wote ndani ya CCM watawajibishwa na kwamba mafisadi ni lazima wavue gamba. Watawajibishwa na kuvuliwa gamba na nani? Lini?


Badala ya kuwa mkakati wa maana, dhana nzima ya kujivua gamba sasa inaonekana kama kichekesho tu cha kipropaganda. Pengine CCM bado hawajayasoma na kuyaelewa mabadaliko ya kisiasa, kifikra na kimtazamo yanayotokea barani Afrika na nchini mwetu. Kama wangejua, basi wangelichukulia zoezi hili la kujivua gamba kwa dhati na bila kusuasua. 

Na sijui ni kwa nini nafasi nzuri ya kujisafisha na kujirudishia imani yao kwa Watanzania inaachiwa tu ipotee namna hii. Siasa ni mchezo wa kula kuliwa na wakati mwingine inabidi kuchukua maamuzi mazito bila kujali uswahiba, utajiri na uzito wa mtu. Watanzania wanachotaka ni Maisha Bora kwa Kila Mtanzania na siyo propaganda na mikakati isiyo na meno! 

Sunday, June 26, 2011

UTAJIRI WA KUTISHA WA WATUMISHI WA MUNGU

  • Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwasha moto kwa kudai kwamba baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, utajiri wa kutisha wa baadhi ya viongozi hawa wa dini umeanza kutiliwa mashaka. 
  • Habari hizi zinakuja wakati ambapo injili ya utajirisho imepamba moto duniani kote. Injili hii inasisitiza kuhusu upokeaji wa mibaraka ya Mungu kama ilivyoahidiwa katika Biblia. Mara nyingi, hata hivyo, kabla hujapokea mibaraka hii ni lazima "upande mbegu" kwa kutoa - mbali na sadaka ya kawaida iliyoamriwa ya fungu la kumi - kiasi cha fedha kanisani ili kuendeleza shughuli za injili. Kwa hapa Marekani wachungaji wengi wanapendelea upande mbegu ya kuanzia  dola 1,000 na hapo mibaraka ya Mungu itakushukia kama mvua - "guaranteed" !
  • Wapo wanaodai kwamba injili hii ya utajirisho imeweza kutumiwa vibaya na baadhi ya watumishi wa Mungu waroho ambao kwa kutumia bashasha na "miujiza" yao wameweza kuwashawishi waumini wao kuuza kila kitu walichonacho na kutoa sadaka kanisani. Na kwa kufanya hivi, watumishi hawa wa Mungu wameweza kuwa matajiri wa kutupwa wakati waumini wao wakiishi katika umasikini. Watumishi hawa wa Mungu wana majumba ya kifalme, madege binafsi ya kusafiria, helikopita na wanaendesha magari ya gharama kubwa. Hivi karibuni shirika la BBC lilichapisha makala juu ya utajiri wa kutisha wa wahubiri wa Nigeria ambao unazidi hata utajiri wa wafanyabiashara wa mafuta. 
  • Sina ugomvi na watumishi hawa wa Mungu kutajirika lakini kama kweli wanajitajirisha kwa kupitia njia za mkato kama vile kuuza madawa ya kulevya na kuwanyonya waumini wao basi ni wazi kwamba wamesahau lengo lao la kueneza injili na kuwaleta kondoo kwa Bwana. Na kwa maoni yangu, watumishi wa Mungu wa aina hii hawana tofauti na mafisadi wanaoiangamiza jamii. Kila mtu na ashike sana alichonacho!
  • Hebu tumsikilize Mchungaji Munishi na wimbo wake huu niupendao sana wa "Wanamwabudu Nani". 

Kwa picha na habari zaidi bofya HAPA. Tamko la Maaskofu kuhusu sakata la madawa ya kulevya lipo HAPA

Saturday, June 25, 2011

Friday, June 24, 2011

FIKRA YA IJUMAA: NATAMANI KUWA MWAFGHANISTAN !!!

Picha hii iko HAPA

Pamoja na kuwa na silaha bora kutuzidi pamoja na sababu zingine za kimfumo, wapo watu wanaodai kwamba sababu hasa iliyotufanya Waafrika tukauzwa utumwani na hatimaye kutawaliwa (mpaka leo hii) ni kutokuwa na utashi kamili. Wapo wanaokwenda mbali na kudai kwamba pengine Waafrika sisi (na watu weusi kwa ujumla) tuna akili pungufu tukilinganishwa na wakazi wa nchi za Kimagharibi. 

Ati, ni kwa nini tulikubali kuuzwa utumwani tena na wazungu wachache tu wenye bunduki na mizinga? Ni kwa nini tulikubali kutawaliwa na wazungu wakati wa ukoloni? Ni kwa nini tunakubali kutawaliwa hata sasa kupitia ukoloni mamboleo? Ni kwa nini tunakubali kuongozwa na wanasiasa mafisadi wasiotujali? Kwa nini Afrika kuna majanga ya kila aina: vita, magonjwa, umasikini wa kupindukia (japo Mungu katujalia kila kitu). Kwa nini? Narejerea hapa hoja zilizozushwa na Aika - binti machachari wa Kichaga aliyesimama kidete katika mjadala mkali kabisa kuliko yote  iliyowahi kurindima katika blogu hii (Tazama HAPA)

Ninaandika haya baada ya Wamarekani kutangaza kuwa wataanza kuondoka Afghanistan kuanzia mwaka huu. Baada ya kuivamia nchi hiyo kwa mbwembwe nyingi huku wakijidai kuwa na silaha kali na za kila aina, leo wanaondoka bila ushindi wo wote kama Warusi. Warusi pia walijaribu "kuitawala" nchi hiyo lakini baada ya miaka 10 waliondoka kwa aibu wakiwa wameshindwa. Waingereza pia walishajaribu kuitawala Afghanistan miaka ya nyuma lakini wakashindwa. Afghanistan haitawaliki! 



Swali tunalopaswa kujiuliza hapa ni kwamba: Kwa nini wa-Afghanistan hawatawaliki wala kushindika? Pamoja na sababu zingine za kijamii, kitamaduni na kihistoria, jibu rahisi linalotajwa sana ni utashi wao. Hakuna silaha hapa duniani inayoweza kuushinda utashi wa binadamu anayetaka kuwa huru, mtu ambaye yuko tayari kuutoa uhai wake ili kulinda akiaminicho, hadhi yake na watu wake. Majeshi, madege ya hatari yanayojiendesha yenyewe, mabomu ya kiatomiki na satelaiti zenye uwezo mkuu wa uoni kamwe haziwezi kufua dafu mbele ya utashi wa mtu aliyedhamiria kuwa huru. Kama unabisha kamuulize Hosni Mubarak atakwambia.

Natamani sana kama Waafrika tungejifunza kitu kutoka kwa wa-Afghanistan. Ati ingekuwaje kama tungekataa kutawaliwa na wanasiasa madikteta na mafisadi ambao lengo lao ni kushibisha matumbo yao yasiyoshiba? Ingekuwaje kama tungesimama kidete na kukataa kuchezewa na majibwa ya Kimagharibi? Ingekuwaje.....? Leo hii tungekuwa wapi?

Ni kwa sababu hii natamani kuwa m-Afghanistan masikini sana asiyejua kusoma wala kuandika lakini ambaye hataki kutawaliwa.  Na hii ndiyo fikra ya Ijumaa hii. Wikiendi njema! 

Thursday, June 23, 2011

WATUNGA SHERIA WETU NA POSHO ZAO NONO !!!

  • Mjadala wa kufutwa kwa posho nono za wabunge uliowashwa na Mh. Freeman Mbowe unafurahisha na pengine unaakisi mwelekeo hasa wa jamii tunayotaka kuijenga na kuiimarisha, jamii ambayo kupitia kwayo mustakabali wetu mzima kama taifa unategemea. Mbowe ameonyesha azma yake ya kiungwana kwa kurudisha shangingi lake (japo ofisi ya bunge inakana na kutoa masharti), jambo ambalo limepokelewa vyema (kikejeli?) na mpiga mbiu mkuu wa Chama tawala. Kwingineko, mtendaji mkuu wa serikali naye ameonekana kuunga mkono harakati hizi kwa kuamua kuacha kutumia gari lake ghali aina ya Mercedes Benz.
  • Inafurahisha kuona kwamba angalau kwa sasa kuna chama cha upinzani ambacho kusema kweli kinatoa mchango mkubwa katika kuwaamsha Watanzania na kuhakikisha kuwa kinasikilizwa na Watanzania hasa wale wa tabala la chini (ambao ndiyo wengi). Hii inakifanya chama kilichopo madarakani kufungua masikio na kusikiliza (na hata kujivua gamba). Na hili ni jambo jema katika jitihada zetu za kujiletea maendeleo. Jambo la muhimu tu ni kwamba tuendeshe harakati hizi za kuamshana na kupigania maendeleo ya Watanzania wote kwa njia za amani. Tunaelekea kwema !!!

NYOKA AKIVUA GAMBA - NA M.M. MWANAKIJIJI (ONYESHO LA KWANZA)

ATI, ITAKUWAJE SIKU JUA LA KIFIKRA LITAKAPOWAPAMBAZUKIA WALALAHOI ???

  • Wakati masikini walalahoi wanabanikana kama ndafu kwa kukwapuliana simu za mkononi, mikufu, hereni na saa, mafisadi wanaokwapua mabilioni ya shilingi na kudidimiza maendeleo yetu wanafanywa au wanafanyiana nini?
  • Ati, inakuwaje mtu anayekwapua simu anachomwa moto mpaka kufa na yule anayeiba mabilioni ya pesa za umma na kulitia taifa hasara kubwa hafanywi cho chote? Haki iko wapi? Ni kweli vyombo vya dola haviwezi kuikomesha hali hii ya walalahoi kupeana hukumu ya papo kwa papo namna hii? Au vinaiachia hali hii iendelee kwa makusudi kwa vile wanaobanikana ni walalahoi wenyewe kwa wenyewe? Vipi ingetokea siku moja mtu wa tabaka la juu akabanikwa? Vyombo vya dola kweli vingekaa kimya tu na kuacha hali iendelee?
  • Ati itakuwaje siku jua litakapowapambazukia walalahoi hawa na wakaamua kuanza kuwabanika mafisadi badala ya kubanikana wao kwa wao?
  • Japo kwa sasa jambo hili laweza kuonekana kama kichekesho lakini historia imejaa mifano tele ya aina hii; na kujipambanua kwa matabaka kati ya matajiri wa kupindukia kwa upande mmoja na walalahoi kwa upande mwingine tunakokushuhudia kwa sasa hakutoi picha ya kupendeza. Na ishara zote zimeshaanza kuonyesha kwamba walalahoi wa Tanzania tayari wameshaanza kuamka kutoka katika usingizi wao mrefu wa kifikra. 
  • Natumaini kwamba viongozi wetu hawako katika kunguku na wanaliona hili. Kushughulikia kero za walalahoi na kuinua hali zao za maisha (na hivyo kupunguza ufa kati ya matajiri na masikini) ndiyo suluhu pekee ya kukwepa misukosuko mikubwa ya kijamii kama hii.

Kwa habari zaidi kuhusu picha hii bofya HAPA

Wednesday, June 22, 2011

HEBU SIKIA "VITUKO" HIVI VYA WANYANTUZU !!!


(1) Asilimia 24.4 ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wameacha kupata dawa za kupunguza makali ya VVU baada ya kunywa dawa ya Babu Loliondo. (Sehemu zingine hali ikoje?)

(2) Wanaume wanadai kwamba eti matumizi ya vyandarua yanasababisha wasiwe na uwezo wa kupata watoto.

(3) Tohara ya wanaume pia inashutumiwa kusababisha utasa.

**************
  • Ukiachilia mbali hili suala la tiba ya Babu, masuala (2) na (3)  ni mojawapo ya mambo yanayoonyesha changamoto za watunga sera ambao mara nyingi hukurupuka tu na kupitisha maamuzi hata bila ya kuwashirikisha walengwa
  • Fikiria kama mtu umemwaga vyandarua huko Unyantuzu Bariadi bila kwanza kufanya uchunguzi wa kina ili kujua kama hivyo vyandarua vinatumiwa kweli ama la. Basi unatoka hapo na kwenda kujikunja kuandika ripoti nzuri kwamba sera ya kutumia vyandarua ili kujikinga na malaria inaendelea vyema kumbe baadhi ya walengwa wako wanaviogopa ili wasije wakapata utasa. 
  • Badala ya kuwabambikiza sera na maazimio kwa kisingizio cha "ujinga", ukosefu wa elimu na imani potofu kuna umuhimu wa kukaa chini na kuifahamu jamii lengwa; na kuishirikisha katika kupitisha maamuzi. Vinginevyo sera nyingi zitakuwa zinaishia kuonyesha "mafanikio" vitabuni tu. 
**************

Waliokunywa dawa kwa ‘babu’ wasusa ARVs
Imeandikwa na Shangwe Thani, Bariadi; Tarehe: 21 Juni 2011

WATU 1,168 sawa na asilimia 24.4 ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wilayani Bariadi, wameacha kwenda kwenye vituo vya kushauri juu ya matumizi ya dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) baada ya kunywa dawa ya Babu wa Loliondo. 


Kaimu Mratibu wa kudhibiti Ukimwi wa Wilaya ya Bariadi, Faustine Kaliche alisema idadi hiyo ni kati ya watu 5,861 wanaoishi na virusi wilayani humo. 


Alikuwa akizungumza katika mkutano wa Kamati ya Ushauri wa Maendeleo ya Wilaya (DCC) mjini Bariadi. 


Alisema wametoroka vituo vya huduma na tiba vinavyotoa ushauri na vidonge vya ARVs baada ya kupata tiba ya kikombe cha Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile katika kijiji cha Samunge, Kata ya Loliondo wilayani Ngorongoro. 


Kaliche alisema kundi hilo lililoacha huduma ni kubwa na ni hatari kwa afya zao na watu wengine watakaojamiiana nao bila ya kutumia kinga. 


Wakati huo huo akifunga mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Baraka Konisaga aliwataka viongozi wa vyama vya siasa, dini na watendaji wa vijiji na kata kuielimisha jamii iondokane na imani potofu kuwa tohara na matumizi ya vyandarua kwa wanaume vinazuia uzazi


Konisaga alisema, tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa mwanaume aliyefanyiwa tohara ana asilimia 60 ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ikilinganishwa na asilimia 40 kwa mwanaume asiyefanyiwa tohara. 


''Kuna uvumi unaoenezwa na watu wasiowatakia mema watu wa wilaya ya Bariadi kuwa wakitumia vyandarua kujikinga na mbu ili wasiambukizwe malaria hawatazaa tena na wale wanaume wanaofanyiwa tohara hawatazaa tena wakifanyiwa tohara kwa kuwa tohara huzuia wasizae,’’ alisema Konisaga. 


Akiwasilisha taarifa, Kaimu Mratibu wa kudhibiti Ukimwi wilayani Bariadi, Faustine Kaliche alisema kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu, asilimia tisa ya watu waliopima afya wilayani humo wamebainika kuambukizwa virusi vya Ukimwi.


Chanzo: Habari Leo

Sunday, June 19, 2011

"NGAMIA" WA AFRIKA NA TUNDU LAO LA SINDANO

Ati, Afrika tungekuwa wapi kama tungekuwa na viongozi (si wata wala)  makini wanaojali na kupigania maslahi ya Waafrika wenzao badala ya matumbo yao, marafiki na familia zao? 

LEO NI SIKU YETU AKINA BABA....

  • Kwa akina baba wote - waanzilishi na walinzi makini wa mfumo dume. Leo ni siku yenu ya kukumbukwa kwa mchango wenu katika uzazi na malezi ya watoto. Nami nachukua nafasi hii kuwatakia akina baba wote maisha marefu na umakinifu zaidi katika malezi ya watoto.
  • Mimi kwa bahati mbaya (au bahati nzuri sijui!) sikuwahi kumwona baba mzazi kwani aliitwa na Mungu wakati nikiwa na miezi mitatu tu. Jamaa enzi zile wakachoma na picha zake kabisa kwani hawakuona haja ya kutunza picha za mtu aliyetangulia mbele ya hukumu. Leo nami nina watoto na ninajaribu kuwapa upendo wa kweli na kuwafundisha yale niliyojifunza kule Unyantuzu. Akina baba popote mlipo - Happy Father's day!
  • Kwa vile mimi ni mpenzi mkubwa wa "Country music", huyu hapa Keith Urban na Song for dad.

Friday, June 17, 2011

FIKRA YA IJUMAA: NIHIL EX NIHILO. TUTAFAKARI MAENDELEO YETU


Nihil Ex Nihilo ni Msemo kutoka katika falsafa ya Wagriki wa kale unaomaanisha kwamba ombwe daima huzalisha ombwe. Kwa hivyo hakuna cho chote kinachoweza kutokea au kutokana na ombwe. Mtazamo huu baadaye uliathiri mtazamo wa Wanasayansi waliofuatia waliodai kwamba mada, japo inaweza kubadilika umbo moja kwenda jingine, kamwe haiwezi kuundwa wala kuharibiwa. Hata nadharia mashuhuri ya ulinganifu kati ya uzito na nishati ya Albert Einstein (E=mc2) kwa kiasi fulani iliakisi mtazamo huu.

Mtazamo huu wa Nihil ex nihilo hata hivyo ulikuwa na matatizo kwa wanasayansi kwa sababu haukuwawezesha kuelezea chanzo cha dunia yetu, sayari zingine na malimwengu mengine. Hata nadharia yao inayodai kwamba mfumo wetu wa sayari ulitokana na Mtanuko Mkuu wa Ghafla (Big Bang) ulikuwa hauthibitishiki kwa sababu nadharia hii haielezi kuhusu chanzo hasa cha “Big Bang” ni nini. Ati, ni nini kilichotanuka kwa ghafla wakati wa Bing Bang na kilitoka wapi? Kulikuwa na nini kabla ya Big Bang? Kama hakukuwa na kitu (nihil), iweje Big Bang itokee na kuunda mfumo wetu wa sayari na mifumo mingine katika malimwengu mengi ambayo yametapakaa huku na huko?

Nihil ex nihilo iligusa hata dhana nzima ya uumbaji. Wanafalsafa na wanasayansi walianza kuhoji kwamba dunia iliumbwa kutokana na nini? Ni kweli kwamba iliumbwa kutoka katika ombwe (nihil)? Ni kwa sababu hii kwamba mtazamo huu haukupendelewa sana na mamlaka ya kanisa (Katoliki) enzi zile.

Katika miaka ya karibuni nadharia ya Big Bang imepata msukumo mpya baada ya Stephen Hawking – Mwanafizikia na mwandishi mashuhuri wa Uingereza kutoa ushahidi wa kinadharia kwamba inawezekana Big Bang ilitokana na mtanuko wa ghafla wa ‘Black Holes’. Alidai kwamba kinadharia hakuna kitu kinachozuia mada kuumbwa kutokana na ombwe, na pengine tunachodhani ni ombwe pengine ni mada na elementi nyingine ambazo hazionekani kwa macho na bado hatujawa na vifaa vya kisayansi kuweza kuzibaini. Ati, kuna ombwe?

Nimeikumbuka Nihil ex nihilo baada ya kutazama kipindi kimoja katika History Channel ambapo wanasayansi walikuwa wakijaribu kueleza chanzo cha maji hapa duniani; na hasa yale ya baharini. Hitimisho lao ni kwamba maji haya pengine yalitokana na vimondo vilivyokuwa vikidondoka kwa wingi duniani wakati dunia ilipokuwa ingali na umri mdogo (Tazama video hapa chini)

Tukiachana na kizungumkuti hiki cha wanasayansi, mtazamo huu wa Nihil ex nihilo umenikumbusha jitihada zetu za kujiletea maendeleo. Kama jamii ni kweli tuna nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii au tunategemea kupata maendeleo kutoka katika ombwe (nihil)? Cha kushangaza zaidi ni kwamba hata sehemu kubwa ya kile kidogo tunachokizalisha nacho kinaishia katika matumbo ya mafisadi. Kwa mtindo huu tutapata maendeleo ya kweli lini? Bila kuchapa kazi kwa bidii na kuhakikisha kwamba kile kinachozalishwa kinatumika kuleta maendeleo ya wote, tutaendelea kupiga maktaimu ya kimaendeleo na mara moja moja tukienda hatua mbili mbele na kurudi nyuma hatua moja; na au hatua moja mbele na kurudi nyuma hatua mbili. Tukumbuke kwamba Nihil ex nihilo.

Na hii ndiyo Fikra ya Ijumaa hii. Tuonane tena Ijumaa ijayo panapo majaliwa. 

WADAU, SAMAHANI KWA KUPOTEA BILA KUAGA. SASA NIMERUDI RASMI...

Wadau wa blogu hii. Mbali na hekaheka za kubeba maboksi, nilikuwa pia na misukosuko midogo ya kiafya. Ndiyo maana kuonekana kwangu hapa bloguni kulikuwa ni kwa kusuasua sana kwa siku za hivi karibuni.

Napenda kutoa shukrani zangu kwa wote mlioniulizia (Dada Rachel, Mpiganaji Matiya, Mchungaji Arrah, Mchambuzi Meghji, Da Subi na wengineo wengi ambao sikuwataja hapa). Asanteni sana. Tupo pamoja na sasa mtaanza tena kuniona katika blogu zenu. Tuwemo...

Sunday, June 5, 2011

UKIMWI LEO UNATIMIZA MIAKA 30 TANGU UTAMBULIWE RASMI. TUTAFAKARI !!!

  • Tarehe 5/6/1981 Dkt. Michael Gottlieb wa Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA) alichapisha makala ya kihistoria ambayo yalielezea kuhusu ugonjwa wa kushangaza ambao mpaka wakati huu ulikuwa umewakumba wanaume watano mashoga.
  • Katika makala yake ya kihistoria, Dr. Gottlieb alibainisha kwamba wagonjwa wote watano walikuwa wanasumbuliwa na kifua kikuu, pamoja na magonjwa mengine nyemelezi. Ugonjwa huu baadaye ulikuja kugundulika kuwa ndiyo UKIMWI!
    • Jambo la kusikitisha ni kwamba: Kwa vile ugonjwa huu mpya ulikuwa unawaathiri zaidi mashoga  -watu ambao walikuwa hawatakiwi katika jamii hasa kwa maoni ya wahafidhina, serikali ya  Marekani haikuona haja ya kuufanyia uchunguzi mapema na ilijikongoja sana katika juhudi zake za kuweza kuutambua ugonjwa huu kama janga la kijamii. Mpaka wacheza sinema wa Holywood ambao hawakuwa mashoga walipoanza kuteketea ndipo hatimaye raisi wa Marekani wa wakati ule (Ronald Reagan) aliweza kubadilisha mtazamo na kuutambua ugonjwa huu kuwa janga la kijamii. Alikuwa amechelewa sana na ugonjwa huu tayari ulikuwa umeshajitandaza.
    • Baadaye iligundulika kwamba zaidi ya asilimia 70 ya wagonjwa wa Hemophilia – wagonjwa ambao wanahitaji kuongezewa damu ili kupata protini muhimu inayosaidia damu kuganda walikuwa wameambukizwa UKIMWI. Cha kushangaza ni kwamba, hata baada ya ukweli huu kueleweka, makampuni ya madawa ya Marekani yaliendelea kuuza protini hii gandishi iliyokuwa imeambukizwa katika nchi nyingine duniani. Kumbe kwa kufanya hivyo UKIMWI ukapata nafasi ya kujitandaza zaidi ulimwenguni kwa haraka zaidi. Mpaka leo kuna watu ambao wanaamini kwamba jambo hili lilifanyika kwa makusudi ili kujaribu kusaidia kupunguza idadi ya watu duniani na kwamba nchi nyingi zilizolengwa katika "kampeni" hii zilikuwa ni kutoka Afrika na nchi zingine masikini duniani! Mpaka leo inaaminika kwamba UKIMWI umeshaua kati ya watu milioni 28-35 na watu zaidi ya milioni 75 tayari wameshaambukizwa !
    • Nilikuwa Mwanafunzi mdogo UKIMWI ulipoingia Bukoba. Wenyeji waliupachika jina la Juliana – jina la mashati fulani yaliyokuwa yanatoka Uganda. Kwa tuliokuwa wote Shule ya Sekondari ya Kahororo enzi zile nadhani watawakumbuka walimu na wanafunzi wenzetu wapendwa tuliowapoteza kutokana na ugonjwa huu hatari usiokuwa na tiba. Jamani, mnamkumbuka Mwalimu wetu wa Kemia Justin Kaijage? Vipi kuhusu Mwanafunzi mwenzetu William Manhyakenda? Walimu wetu wa Fizikia na Hesabu Mushaija na Mkewe? Vipi kuhusu Mwalimu wetu mpendwa wa Bayolojia Ntamakurilo? Mhasibu Gama, Wapishi wetu wapendwa na baadaye Mkuu wetu wa shule Ishengoma?
    • Kama vile kitambulishi cha ushoga kilichoambatishwa na ugonjwa huu kule Marekani, tulishuhudia unyanyapaa mkubwa kwa wagonjwa wa UKIMWI: Ulikuwa ni ugonjwa wa kuonewa aibu sana. Hili lilikuwa ni kosa na nchi zilizojidamka mapema katika kukabiliana na ugonjwa huu (mf. Uganda) zilipiga hatua kubwa katika kukabiliana nao. Nchi zingine za Kiafrika zikaendelea na unyanyapaa na matokeo yake tumeyaona. Ugonjwa wa UKIMWI umeibuka na kuwa janga kubwa kabisa katika kizazi hiki !
      • Baada ya miaka 30, Leo hii karibu kila familia imeshaguswa na UKIMWI kwa namna moja ama nyingine. Mimi binafsi nilishawapoteza kaka wawili kutokana na ugonjwa huu hatari.
      • Leo hii “tunaposherehekea” miaka 30 ya gonjwa hili hatari tukumbuke tu kwamba bado halina kinga wala tiba na bado linaua (pamoja na Loliondo yetu!). Uzuri sasa ni kwamba tunalifahamu gonjwa hili vizuri na tunaweza kujikinga nalo tukiamua. Wapendwa, tuchukue tahadhari !!!
        Makala ya kihistoria ya Dkt. Michael Gottlieb yanapatikana HAPA

          JIANDIKISHE HAPA

          Enter your email address:

          Delivered by FeedBurner

          BLOGU ZA BURUDANI NA UREMBO