Ni kweli mkokoteni huu umemwelemea huyu mama wa shoka? Wananchi wana maoni gani kuhusu mkokoteni huu kuwa "mzito" hivi? Hili ni jambo jema?
Pengine "waheshimiwa" wetu hawa siku moja nao watazipiga kama wenzao HAWA. Kwa habari zaidi soma HAPA, HAPA na HAPA. Katuni ni kutoka Katuni Inasema na Wavuti.
Uchambuzi mpya uliofanya kutokana na data za sensa hapa Marekani unaonyesha kwamba pengo la kipato kati ya walionacho na wasionacho linazidi kupanuka.
Uchambuzi huu umeonyesha kwamba kipato cha wazungu ni mara 20 ya kile cha watu weusi na mara 18 ya kile cha watu wenye asili ya Kilatino. Kipato cha wastani kwa familia za kizungu mwaka 2009 kilikuwa dola 113,149 ikilinganishwa na dola 6,325 katika familia za watu wenye asili ya Kilatino na dola 5,677 familia za watu weusi.
Sote tunajua kwamba Marekani bado inasumbuliwa na ubaguzi wa rangi na kusema kweli watu ambao si wazungu bado wana uwezekano mkubwa zaidi wa kwenda jela, kutokuwa na elimu bora, kutopata kazi nzuri, kuishi katika umasikini na kufariki mapema kuliko wenzao wazungu.
Matabaka haya yana madhara makubwa kijamii kiasi kwamba jamii nzima inaathirika. Marekani ndiyo nchi yenye wafungwa wengi magerezani na katika baadhi ya majimbo bajeti ya kuendesha magereza inazidi, inalingana na au kupungua kidogo tu ile ya elimu. Jamii ya aina hii ni wazi kwamba ina matatizo na hii ni mojawapo ya sababu inayotajwa sana kuwa ni tatizo kubwa la mfumo wa kijamii wa Kimarekani, mfumo ambao pengine utaweza kuchangia katika kuporomoka kwake.
Sisi tunaingiaje katika mtafaruku huu? Tunaendelea kulea matabaka: watu wachache wanajitajirisha sana tena kwa kutumia raslimali za wote wakati wananchi wetu wengi wanazidi kuwa masikini. Kama unabisha nenda huko vijijini ukaone. Bado hatujaweza hata kuwapatia watu wetu huduma za msingi kabisa wakati tunao mafisadi wanaofuja mabilioni ya pesa za umma, pesa ambazo kama tungezitumia vizuri zingeweza kusaidia kuinua hali za maisha za wananchi wetu ambao ni masikini hasa huko vijijini.
Hali hii ikiachiwa kuendelea ni wazi kwamba tunakoelekea si kuzuri kwani binadamu ni mnyama mwenye kujua ukomo wake. Unaweza kumnyonya, kumsikinisha, kumdhulumu na kumtesa lakini siku moja atafikia kikomo na kusema liwalo na liwe. Akifikia hali hii basi jamii inaingia katika misukosuko mikubwa. Historia imejaa mifano mingi ya aina hii.
Ati, mahusiano yetu ya kitabaka leo yangekuwaje kama kweli tungezitumia raslimali zetu kwa faida ya wote?
Wapendwa: Inbox na Sentbox ya Email yangu ya gmail (profesamatondo@gmail.com) zilifutwa na pengine zilijifuta (kama google walivyodai) na imenichukua muda kupata usaidizi wa Google kuzirudisha japo sina uhakika kama meseji zote zimerudishwa. Kwa sasa najibu e-mail za watu polepole hasa zile za muhimu.
Kwa hivyo kama uliniandikia na hukupata jibu, naomba radhi. Naahidi kwamba nitajibu meseji zote za kibinafsi......
Kuhusu kutoonekana hapa kibarazani kwangu na katika vibaraza vya wanablogu wenzangu mara kwa mara ni kutokana na hekaheka za safari na mabadiliko makubwa ya kimaisha na kifamilia ninayokabiliana nayo kwa sasa. Naamini mambo yatatulia na kurudi katika hali yake ya kawaida. Tuko pamoja na kamwe sitakaa niache kublogu na kusoma blogu za wanablogu wenzangu. Kublogu ni mojawapo ya mambo ya muhimu kabisa ambayo nimeshawahi kufanya katika maisha yangu.
Nimesoma habari hii kwa mshangao kidogo. Ni kweli dawa ya babu haitibu na haijawahi kutibu? Vipi kuhusu vigogo waliokuwa wakimimika huko na kuaminisha watu kwamba ilikuwa inatibu? Vipi kuhusu akina Mrema na watu wengine waliothibitisha kwamba ilikuwa imewaponyesha? Vipi kuhusu utafiti wa "wataalamu" ikiwemo ripoti ya awali ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) iliyothibitisha kwamba dawa hiyo ni kinga mathubuti kwa magonjwa mbalimbali?
Hata kama ni kweli kwamba dawa hii haitibu, kisiasa ilikuwa ni "tiba" tosha katika kipindi ambacho taifa lilikuwa linapita katika vuguvugu la kashfa mbalimbali zikiwemo DOWANS na RICHMOND. Badala ya kuripoti kuhusu mambo haya muhimu kisiasa, vyombo vya habari vilitupia hasa macho yao Loliondo na sehemu zingine nchini ambako watoa vikombe walikuwa wakiibuka kila siku. Moto huu uliendelea kuchochewa na viongozi wa serikali na chama waliokuwa wakimiminika huko Loliondo kupata hiyo tiba ingawa wengine walidai kwamba walikuwa wanakwenda huko kwa ajili ya "curiosity" tu na si vinginevyo. Viongozi kadhaa wa upinzani walilalamikia jambo hili na kusema kwamba serikali ilikuwa inashabikia tiba hizi za kiimani ili kujaribu kupoteza mwelekeo wa kesi na kashfa mbalimbali za kifisadi zilizokuwa zikiiandama.
Kama madai haya ni kweli basi si kweli kudai kwamba eti tiba hii ya babu haitibu. Ilikuwa tiba tosha kisiasa na imeshafanya kazi yake; na sasa babu anaweza kuendelea na shughuli zake nyingine. Kuna anayejua sakata la DOWANS lilikoishia? RICHMOND je?
Mimi naendelea kuuliza tena na tena, hili zoezi la kujivua magamba litamalizika lini? Tusipokuwa makini nyoka wetu huyu atabakia na mabakamabaka kila mahali - hapa ngozi mpya na pale kuukuu tena iliyokakawana. Kama kujivua kumeshindikana, pengine tujaribu kuvulishana - hata kama ni kwa "kumwagiana tindikali". Mkanganyiko!
Sakata la Mbunge wangu (Bwn. Chenge) kuhusu ununuzi wa rada ambalo nilianza kulijadili jana linazidi kuchukua sura mpya. Hata baada ya "kusafishwa" rasmi na serikali pamoja na TAKURURU, wakuu wa chama chake bado wanamtaka ajivue gamba.
Dr. Slaa naye tayari ameshawasilisha serikalini uchambuzi wa ushahidi utakaosaidia kumtia hatiani Chenge. Sijui mbunge wangu huyu kama safari hii atasalimika.
Sakata hili pia inaibua swali jingine: Ati, ni kwa nini wanasiasa wa Afrika ni wagumu sana kuwajibika na kujiuzuru hata kama tayari ni matajiri wa kutupwa? Kwa nini wanasiasa wa nchi za Magharibi wakiguswa na ka kashfa tu kadogo basi wanawajibika na kuachia ngazi mara moja?
Ni mbunge wangu bilionea Bwn. Andrew Chenge. Ni kuhusu lile sakata la ununuzi wa ile rada yetu ya bei mbaya. TAKURURU walishamsafisha. Na mwenyewe pia alishajitakasa. Wakati huo huo serikali kupitia kwa waziri wake wa Nchi Ofisi ya Rais, Mathias Chikawe imetangaza rasmi kwamba mbunge wanguhakuhusika kwa namna yo yote ilena sakata hili.
Wakati huo huo timu ya Wabunge waliokwenda Uingereza hivi karibuni kufuatilia malipo ya rada hiyo imependekeza kwamba Bwn. Chenge pamoja na wenzake waliohusika na kashfa hii iliyoliletea taifa hasara kubwa wafikishwe mahakamani. Katika taarifa yao, Chenge anatajwa kuwa ni mtuhumiwa namba mojapamoja na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Dk IdrisaRashid.
Baadhi ya wabunge wa timu hiyo: mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (kulia), mbunge wa Ilala, Idd Zungu (katikati) na mbunge ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai (kushoto).
Kutokana na taarifa hii, mnadhimu Mkuu wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissuamechimba mkwarakwamba Chenge asipofikishwa mahakani basi CHADEMA watafanya maandamano nchi nzima mpaka kieleweke!
Mkanganyiko huu umeniachia maswali mengi. Kama mbunge wangu kweli ana hatia kama inavyodaiwa, kwa nini TAKURURU na serikali wameshamsafisha?Ningetegemea kwamba katika kipindi hiki cha kujivua magamba, chama tawala na serikali yake wangekuwa wakali na kutumia sakata kama hili kuonyesha kwamba kweli wamedhamiria kujisafisha. Je, huu ni mwendelezo wa ile tabia sugu ikerayo sana ya kulindana na kukingiana kifua?
Ndiyo maana imebidi niulize kama mbunge wangu ana hatia ama la kwani siamini kama kweli katika kipindi hiki cha mtandao na upatikanaji huru wa habari, wavua magamba wangali wanategemea kwamba wataweza kweli kuzima na kuifunika kashfa nzito kama hii.
Kunakaribia kupambazuka sasa na anayedhani kwamba kungali bado usiku wa manane anajidanganya. Hebu ubaridi wa alfajiri na ukatusisimue na kutuondolea hofu, matongotongo na fikra zetu za kitwana.
Mwaka huu Sehemu ya nchi yetu, yaani Tanzania Bara itaadhimisha miaka hamsini ya Uhuru wake toka kwa Wakoloni. Uhuru huu uliopatikana miaka hamsini iliyopita ni kazi nzuri na ya Kizalendo iliyofanywa na Chama cha TANU. Chama Cha Mapinduzi katika kukumbuka kazi hii nzuri ya kutafuta Uhuru wa nchi yetu kimeamua kufanya shughuli mbalimbali za kukumbuka kuzaliwa kwa chama kilicholeta Uhuru wa Tanzania Bara yaani TANU.
Itakumbukwa TANU ilizaliwa tarehe 7/7/1954 hapa Dar es salaam katika mtaa wa New street ambao kwa sasa unafahamika kama mtaa wa Lumumba mahali ambapo sasa ni Ofisi Ndogo ya CCM Makao Makuu. Huo ukawa ndio mwanzo wa harakati za kudai Uhuru, Utu na Heshima ya Mwafrika katika nchi yetu.
Kwa kuienzi historia na kazi nzuri na ya Kizalendo iliyofanywa na TANU, Chama Cha Mapinduzi kimeamua katika kuadhimisha miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara kuandaa shughuli mbalimbali za kijamii zikiwa na kauli mbiu Uhuru na Kazi, kauli maarufu katika miaka ya nyuma ambayo Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere aliitoa katika hotuba yake ya kusisimua siku ya mkesha wa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961. Mwalimu Nyerere aliitumia hotuba hiyo kuwaeleza wananchi wajiandae kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea wao wenyewe na nchi maendeleo.
Maadhimisho haya yatafanyika nchi nzima kuanzia ngazi za matawi na kuwashirikisha wanachama wetu na wananchi wote kwa ujumla. Shughuli zitakazofanyika ni kama zifuatavyo:
i. Usiku wa kuamkia tarehe 7/7/2011 Vijana wa CCM nchini watakutana maeneo mbalimbali kufanya shamrashamra za kuzaliwa TANU
ii. Tarehe 7/7/2011 asubuhi wanachama wa CCM na wananchi watakutana kwenye matawi yao na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile, kufanya usafi, kusaidia ujenzi, kupanda miti, kutembelea wagonjwa mahospitalini n.k.
iii. Ikiwezekana kufanya matamasha mbali mbali yatakayowashirikisha vijana,wasomi,wanasiasa na wazee kujadili masuala mbali mbali yenye faida kwa Kata, Wilaya, Mkoa au Taifa kwa ujumla.
iv. Kufanya mikutano ya hadhara na kujikumbusha mafanikio yaliyopatikana kwa kila Mkoa na Wilaya katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru. Kwa Sehemu kubwa tunategemea walezi wa CCM wa Mikoa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa watashiriki shughuli hizo mikoani.
Sherehe hizi zitaanza usiku wa tarehe 6/7/2011 kwa vijana wa CCM sehemu mbalimbali nchini kukutana na kusherehekea ikiwa ni pamoja na kufyatua MAFATAKI saa sita usiku ya siku hiyo, kama ishara ya kuzaliwa TANU.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dr. Jakaya M. Kikwete atashiriki sherehe hizi mkoani Dar es salaam, usiku wa Tarehe 06/07/2011 na tarehe 07/07/2011 asubuhi atakutana na Mabalozi wa Nyumba Kumi Mkoa wa Dar es salaam. Ni mategemeo yangu vyombo vya habari vitashirikiana nasi katika kuuelimisha umma kuhusu historia hii muhimu ya Taifa letu na kutangaza matukio yote yatakayo ambatana na maadhimisho haya. Ahsanteni sana.
Nape M. Nnauye, KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA, ITIKADI NA UENEZI 03/07/2011
*************
Angalizo
Jambo la muhimu linalokosekana katika taarifa hii ni kuhusu matatizo na changamoto ambazo TANU na baadaye CCM i-li/me/mesha/na-pambana nazo. Ningependa sana kusikia, mbali na mafanikio yaliyopatikana, changamoto zinazotukabili kama taifa na la muhimu zaidi - mikakati ya kupambana na changamoto hizo.
Ni nusu karne sasa imepita na japo ni wazi kwamba tumepiga hatua, ni lazima pia tujikumbushe wapi tulipojikwaa na tunachukua hatua gani kuzuia tusijikwae tena. Kama safari yetu haijaenda sawasawa kama tulivyotegemea, ni kwa nini? Zipi ni kero kubwa (na zipo nyingi tu) zinazowakabili watu wetu? Tutazitatuaje?
Kukusanyika ili kusherekea mafanikio pekee ni kujivika kilemba cha ukoka...
Vinginevyo Happy Birthday TANU/CCM. Na pengine si vibaya tukiisikiliza tena sauti hii yenye kuchoma kuhusu zimwi letu kuu angamizi linatotuandama na kukwamisha maendeleo yetu. Mungu Ibariki Tanzania !!!
Jitihada za kukubaliwa rasmi kwa "Tau" zinaendelea na kama zikifanikiwa basi itabidi kuondoa matumizi ya "Pi" katika vitabu na kuanza kutumia "Tau"
Kwa Wataalamu wa Hisabati mnaweza kutufafanulia zaidi faida za hii namba mpya. Kama nilivyowahi kusema HAPA, somo la Hisabati ndiyo somo-mama na ni kosa kubwa kulidharau na kutolifundisha vizuri.
******
Mathematicians Want to Say Goodbye to Pi
"I know it will be called blasphemy by some, but I believe that pi is wrong.
That's the opening line of a watershed essay written in 2001 bymathematician Bob Palais of the University of Utah. In "Pi is Wrong!" Palais argued that, for thousands of years, humans have been focusing their attention and adulation on the wrongmathematical constant.
Two times pi, not pi itself, is the truly sacred number of the circle, Palais contended. We should be celebrating and symbolizing the value that is equal to approximately 6.28 — the ratio of a circle's circumference to its radius — and not to the 3.14'ish ratio of its circumference to its diameter (a largely irrelevant property in geometry).
Last year, Palais' followers gave the new constant, 2pi, a name: tau. Since then, the tau movement has steadily grown, with its members hoping to replace pi as it appears in textbooks and calculators with tau, the true idol of math. Yesterday — 6/28 — they even celebrated Tau Day in math events worldwide.
But is pi really "wrong"? And if it is, why is tau better?
The mathematicians aren't saying that pi has been wrongly calculated. Its value is still approximately 3.14, as it always was. Rather they argue that 3.14 isn't the value that matters most when it comes to circles. Palais originally argued that pi should be changed to equal 6.28 while others prefer giving that number a new name altogether.
Kevin Houston, a mathematician at the University of Leeds in the U.K. who has made a YouTube video to explain all the advantages of tau over pi, said the most compelling argument for tau is that it is a much more natural number to use in the fields of math involving circles, like geometry, trigonometry and even advanced calculus.
"When measuring angles, mathematicians don't use degrees, they use radians," Houston enthusiastically told Life's Little Mysteries, a sister site to LiveScience. "There are 2pi radians in a circle. This means one quarter of a circle corresponds to half of pi. That is, one quarter corresponds to a half. That's crazy. Similarly, three quarters of a circle is three halves of pi. Three quarters corresponds to three halves!" [A Real Pie Chart: America's Favorite Pies]
"Let's now use tau," he continued. "One quarter of a circle is one quarter of tau. One quarter corresponds to one quarter! Isn't that sensible and easy to remember? Similarly, three quarters of a circle is three quarters of tau." Making tau equal to the full angular turn through a circle, he said, is "so easy and would prevent math, physics and engineering students from making silly errors."
A better teaching tool
Aside from preventing errors, as Palais put it in his article, "The opportunity to impress students with a beautiful and natural simplification has turned into an absurd exercise in memorization and dogma."
Indeed, other tau advocates have said they've noticed a significant improvement in the ability of students to learn math, especially geometry and trigonometry where factors of 2pi show up the most, when the students learn with tau rather than pi.
Though 2pi appears much more often in calculations than does pi by itself (in fact, mathematicians often accidentally drop or ad that extra factor of 2 in their calculations), "there is no need for pi to be eradicated," Houston said. "You might say I'm not anti-pi, I'm pro-tau. Hence, anyone could use pi when they had a calculation involving half of tau."
Tau, the 19th letter of the Greek alphabet, was chosen independently as the symbol for 2pi by Michael Hartl, physicist and mathematician and author of "The Tau Manifesto," and Peter Harremoës, a Danish information theorist. In an email, Houston explained their choice: "It looks a bit like pi and is the Greek 't,' so fits well with the idea of turn. (Since tau is used in angles you can talk about one quarter turn and so on.)"
Pi is too ingrained in our culture and our math to succumb to tau overnight, but the movement pushes ever onward. "Change will be incremental," Houston said.
Kwa hali ya sasa nchini mwetu nani ni mla rushwa na yupi ni mwadilifu? Daima ni kweli kwamba mtoto wa nyoka ni nyoka? Ni lazima tuupime uadilifu wa mtu kwa kuzingatia wasifu na dhambi za wazazi wake? Historia inasemaje? Rushwa ni suala la kimfumo lakini utatuzi wake tunauchakura katika jalala la hulka na uadilifu wa mtu mmoja mmoja. Tutafanikiwa?
Samahani kwa maswali mengi yasiyo na maana. Ni hiki kibonzo cha Mpangala kimenifikirisha sana. Ijumaa na Wikiendi njema wadau!