- Mwanzoni ilisemwa, tena kwa vishindo na mihemko tele, kwamba mkakati kabambe wa kujivua magamba ili kuisafisha CCM ungekamilika katika muda wa siku tisini. Muda huo ukaja na kuyoyoma.
- Baadaye lugha ikageuka na kusemekana kwamba kujivua magamba ilikuwa ni mkakati wa hiari na wa polepole.
- Kwa wachambuzi wengi ilikuwa bayana kwamba mkakati huu rahisi na muhimu kwa uhai wa chama hiki kikongwe ama ulikuwa haukuandaliwa vizuri au utekelezaji wake ulikuwa umekwama na kugubikwa na ubabaishaji.
- Wapo wanaouona mkakati huu kama ni kosa na mtego kwa CCM hasa kutokana na ukweli kwamba badala ya kukiunganisha chama, umegeuka na kuwa chanzo cha migogoro na mgawanyiko wa kimakundi.
- Ndiyo maana nimefurahi kusikia kwamba sasa dawa ya mafisadi imeiva ndani ya CCM na hakuna cha msalie mtume; na kwamba mafisadi ni lazima wang'oke mara moja vinginevyo nguvu zitatumika ili kuwang'oa!
- Swali wanalopaswa kujiuliza wanaoitakia mema CCM ni hili: Kwa nini utekelezaji wa mkakati huu umekuwa mgumu? Kwa nini ni vigumu kwa wanasiasa wetu hawa kujivua magamba? Wanaogopa nini? Ni kweli sasa nguvu zitatumika katika kukisafisha chama?
Katuni zote ni kutoka kwa Said Michael.




