NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 16, 2012

DR. WILBROAD SLAA, KWA HILI UMECHEMSHA


Na Ulanga Ally
Wanabidii (16/1/2012)

Natanguliza pole kwa familia na wanamageuzi kwa msiba wa mpiganaji mwenzetu Bi. Regia Mtema. Hakika msiba huu nipigo kubwa kwa Taifa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi,amina. 

Dr. Slaa ukiwa kiongozi mwenye sura ya kitaifa, utambue kuwa maisha  yako yote yanakuwa mikononi mwa jamii (watanzania).Hii na maana ya kwamba kwa lolote utakalo shughulika nalo lazima litaifikia jamii na kupata fursa ya kulitafakari. Tunatambua kuwa kila mtu anatabia zake binafsi aidha kutokana na malezi, mafundisho ama kuzaliwa. Ni dhahiri pamoja na yote kuna tabia zisizokubalika (mbaya) na zinazokubalika (nzuri) katika jamii. 


Tunatambua uligombea nafasi kubwa ya uongozi wa juu wa Taifa letu (U- Rais) na kwa bahati nzuri ama mbaya ulishindwa na Rais akapatikana naye ni Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. 

Tutambue kuwa kulingana na sheria zetu pamoja na Katiba tuliyo nayo huyu ndiye kiongozi wetu Watanzania na ndio maana kila mtu akimtaja anaanza na "Rais". Katika ushindani kuna kushinda na kushindwa na inapokuwa shida kupinga ushindi wa mtu ki-ushahidi na kimazingira ni busara kukubali kushindwa. 


Hivi vitu kwako vimekuwa ni vigumu kuvikubali na katika hali ya kawaida umeonekana ni mtu mwenye chuki kubwa tena ya wazi kwa Rais wa nchi. Binafsi mwenendo wa tabia yako siupendi kwani umejaaa unafiki,wivu,chuki na majungu ambapo haipaswi kwa kiongozi wa Kitaifa kama wewe na zaidi mtu wa imani (Padri Mstaafu) kuwa nayo. 


Tunatambua kuwa Kikwete kama Rais na kama binafsi ana mapungufu yake lakini hawezi kuwa mbaya kwa yote. Sidhani kwamba imefikia hatua tunajali ya KIJINGA na kuacha MEMA.Kitendo chako cha kumuona Rais wa Nchi kama adui yako namba moja kiasi cha kutosalimiana (nitafafanua chini) hata katika shughuli za kijamii ni aibu kwa taifa, kwako  binafsi, kwa kiongozi wako Mbowe na Chama kwa ujumla. Sikuwa na waza juu ya muendelezo wa tabia yako lakini sasa nimebaini kuwa wewe si muungwana na haufai kuwa kiongozi wa Taifa hili kama hutobadilika. Mifano:- 


1) Ulipinga matokeo ya uchaguzi kupitia vyombo vya habari kwamba si halali na hii ni kwa sababu hukushinda. (Watanzania tulikusikia na kukuona). 

2) Ulikataa kuhudhuria katika mwaliko wa kumtangaza Kiongozi aliyeshinda U-Rais huku na wewe ukiwa mgombea. (Watanzania tulikusikia). 

3) Mchakato wa Katiba hukushiriki kwenda kumuona Rais Ikulu huku ukiwa kiongozi na mratibu Mkuu wa Chama kwa nafasi yako ya Ukatibu Mkuu. (Watanzania tunajua). 

4) Umekataa kuhudhuria Sherehe zote za Kitaifa hasa pindi chama kinapoalikwa na kukuteua wewe kuhudhuria. 

5) Kumkwepa Rais wa Nchi katika Msiba wa kipenzi chetu Bi. Regia Mtema (Hili limenisikitisha kuliko yote) huku ukiwa na taarifa ya ujio wake na baadae kuwasili baada ya kusikia Rais ameondoka. (tunajua waweza sema kuwa ulikuwa na majukumu mengine). 


Picha, Maelezo na Maoni HAPA na HAPA

Hizi tabia zako hazipaswi kuvumilika hata kidogo na ni zaidi ya unyama. Wewe kama Kiongozi unayejiamini ni kwa nini ujifiche ama umkimbie mtu unayemuona kama adui yako? (unapaswa ukabiliane nae) tabia hii inaonyesha mengi huwa unaidanganya jamii juu yake sasa ni AIBU kuonana nae uso kwa uso. Tambua maisha yako na ya viongozi wengine wa vyama vya kisiasa ndani ya Nchi hii yako mikononi mwa Watanzania na si kwao binafsi. Hivi kama ni kuku -assassinate unafikiri TISS wanashindwa? Ukweli ni kwamba wanaweza lakini watawaambia nini Watanzania juu ya kifo chako. Hii nimeisema kama unahisi kuonana na Kikwete ata katika MSIBA maisha yako yatakuwa hatarini. 


Tunajua by implication wewe ni mfuasi wa vegeance policy hasa utakapo pata madaraka (U-rais) , lakini sidhani kusalimia na mtu kutakupunguza hasira na malengo yako ya kutochukua maamuzi unayoyapenda. 

Regia Mtema (Marehemu) -Ametukutanisha hapa msibani kwa sababu ya uungwana wake kwa watu wote pasipo kujali itikadi ya vyama ama dini. Huyu alikuwa binti mdogo sana lakini kwa miaka 32 (umri wake) ameweza kufanya makubwa na kusababisha sote kumpenda. Regia angekuwa mbaguzi, mwenye chuki, asiyekubali kubadilika leo hii pamoja na msiba wake , lakini maneno mengi ya chini chini yangekuwa yakipita juu ya ubaya wake. 

Dr. Slaa tunakuthamini kwa mchango wako wa mageuzi ya kisiasa, changamoto pamoja na umri wako (miaka 64 tarehe 29/10/2012 utatimiza). Hivi kweli kujitenga kwako ama kwa tabia hizi unatufundisha nini sisi vijana tunaokuwa na tegemeo la Taifa? 

Nampongeza sana Mwenyekiti wa Chama Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe hakika ni tofauti kabisa na wewe. Yote ambayo umekwepa kuyatekeleza ata amabayo yamekuwa yakikuhusu , yeye ameweza kuyatekeleza napengine si kwa nafasi yake bali kwa kujali utu na kutambua kuwa SIASA SI VITA (pale demokrasia inapochukua mkondo wake). Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimepata kiongozi bora na mtu wa watu. Mhe. Freeman Mbowe hakika:-

1) Ni mpenda watu 
2) Hana Makuu, majungu wala fitina 
3) Ni binadamu wa kweli anayeishi kulingana na mwenendo wa maisha ulivyo. 
4) Kiongozi bora wa Kisiasa na Kijamii 
5) Hana visasi na mwenye kutambua utu wa mtu 
6) Muungwana na si mgumu wa kusamehe 
7) Mwenye msimamo thabiti wenye kujali haki za wananchi na Wajibu wa Watawala 
8) Mtu wa kujichanganya na wengine pasipo kujali cheo chake, madaraka yake na pesa zake. “Ewe Mwenyezi Mungu tunakuomba umzidishie Umri pamoja na Busara Kiongozi huyu.” 

WITO


Dr. Slaa tunajua ni jinsi gani ilivyo ngumu kubadili tabia yako hasa katika utu uzima ulio nao,lakini hakuna kinachoshindikana mbele ya Mungu. Rudi nyuma utubu na Mwenyezi Mungu atakupa busara ya kutuongoza  vinginevyo "Your leadership can be another disaster to our Nation". 

13 comments:

 1. Kwa nini leo ujumbe huu wakati watu wapo kwenye msiba? Usituchanganye nawe.

  ReplyDelete
 2. slaa kama ni kweli umefikia hatua hiyo hakika si ubinadamu,kwanini usiwe na moyo wa kusamehe?sasa hata ukimwepa kikwete itakusaidia nini?Rais wetu mbona si mtu wa visasi kama wewe,hata msibani slaa?au uzee umeanza kukusumbua?je ukipata urais itakuaje?nimesikitishwa sana na jambo hili,hatutaweza kuunga mkono upuuzi,huo ni msimamo wa kijinga hata kama wewe ni rafiki yangu.Ifikie hatua mweshimu Kiongozi wako,uchaguzi ulishapita.kama huwezi ondoka kwenye nchi yake,unamdharau lakini jeshi lake ndio linakulinda ,yeye si Amiri Jeshi mkuu.usitembee kwenye barabara zinazosimamiwa na serikali yake,lete hizo treni ulizotuahidi,wewe una roho ya ugaidi isiyo na utu.lazima nikuambie padre mwenzangu.tumeambiwa tusamehe lakini wewe unafanya kinyume.tulitegemea kuwa mshauri mzuri kwa vijana sasa kijana Mbowe anakuzidi hekima,please turn back mpatane na Raisi huyu,asiye na visasi,mcheshi,muungwana,anayejali watu,mstarabu,anayejishusha,anayesikiliza watu wa rika lote hata wewe alikuita ikulu ukajifanya kuringa lakini nchi inasonga mbele.Narudia tena nilikupenda tena hata kwenye kampeni zako nilikusaidia hata kukutia moyo,ila kwa hili sitakuvumilia,HUO SIO UUNGWANA WALA USTARABU HATA MISIBANI?KIKWETE MPUUZE HUYU MTU SIO KOSA LAKE UZEE UNAMJIA VIBAYA,NI PADRE MWENZANGU NA MFAHAMU.

  ReplyDelete
 3. Hacha kumchagulia marafiki au kuweka maneno mdomoni mwa Dr. SLAA,Slaa ni mpambanaji na mapambano yana mbinu mbalimbali,why he should cling to a thief who stole food on the table? Slaa is not alone bali tuko wengi tu tusiopenda huyo jamaa yako,sisikilizi hotuba zake,I don't even watch him on any Tv channel,you force that hata kama haibadilishi kitu na kama wewe una mahaba naye si mkanywe naye kahawa huko kwenye vijiwe vyenu?

  ReplyDelete
 4. lazima kuwa na kisasi na m**zi! hivi kweli tunaweza kulinganisha dr slaa wa kusomea huo U- Dr na kwikwetu mwenye U-Dr wa kupewa kwa kuwa ni rais?

  mkosoe tu

  ReplyDelete
 5. mawazo yako uctake kuwa ya watanzania rafiki yangu,kuwa na blog ya kupablish kila unachoweza cyo ujifanye ww ndy msemaji wa watanzania,jisemee mwenyewe kwamba mimi ninafahamu,cyo watanzania wanafahamu mtazamo wako,jiweke wazi labda unasemea kundi fulani la watu lakini cyo watanzania!...
  jirekebishe mambo huwa hayatafakariwi kwa jinsi hyo...

  ReplyDelete
 6. profesa matondo umeweweseka sana. ya wana siasa waachie wanasiasa. ya wanaisimu tutawaachie nyie wana isimu. kuna njia nyingi za kufanikiwa kisiasa ikiwa pamoja na kususia mambo fulani fulani. by the way uchaguzi wa mwaka 2010 haukuwa na miziengwe kwayo inatosha kusema haukuwa huru na wa haki. au nawe unataka kugombea usukumani sasa umeona ujikombekombe

  ReplyDelete
 7. kwanini watanzania mna mawazo finyu, kwanini unafikiri kuna umuhimu wa slaa na kikwete kusalimiana, kwa nini usiangalie maswala chungu nzima yasiyo ya kibinadamu yanayofanywa na unavika salamu ubinadamu.

  ReplyDelete
 8. Mtanzania Mpenda Amani (Sydney Australia)January 18, 2012 at 2:21 AM

  Dr. Wilbroad Slaa = OPIUM OF/TO THE PEOPLE

  Yaani kuna watu utafikiri Huyu Padri feki aliyefukuzwa upadri kwa sababu ya uzinzi ni baba yao. Akisemwa vibaya tu basi

  wataripuka na kuanza mashambulizi. Who the hell is Dr. Slaa?

  Kwa nini ni sawa kumsema na kumtukana Rais Dr. Kikwete lakini kumsema vibaya Dr. Slaa ni mwiko? Ukitazama kule Jamii Forums

  Dr. Kikwete anashambuliwa na kutukanwa sana. And yet this is the president of the republic. Lakini ukimgusa Dr.Slaa uwiii, utakuwa umewasha moto na utaandamwa na kutukanwa sana. Why? Dr. ni nani katika nchi hii?

  Guys, NEVER TRUST A POLITICIAN HATA KAMA NI BABAKO MZAZI. Kawaulize watoto wa Saddam Hussein na Gaddhafi watakwambia. Sasa nyinyi mnaomwabudu huyu padri shauri yenu. Mtu mwenyewe ndo huyo hana subira, uvumilivu na maelewano. Anasusa kuonana na rais wa nchi yake mpaka kwenye MSIBA. I mean MSIBA.....

  Matondo - Huwa napenda blog yako na ingawa kuna wakati unakuwa mzembe wa ku-update, blogs yako ni mojawapo ya blogz chache ambazo ziko independent na hazipendelei, na zimekomaa. Hata CCM umeshaisema sana. Anayebisha aangalie kipengele cha POLITICS. Lakini leo umeweka hii makala ya Mtakatifu Masihi kiongozi wa CULT, makala ambayo you didn't even write, basi unashambuliwa. Pole sana mzee.

  I congratulate mwandishi original wa makala hii Bwn. Ulanga Ally. It is time watu tuanze kusema ukweli kuhusu hii kansa iitwayo Dr. Slaa nchini mwetu. Tusipokuwa makini mtu huyu atatuharibia amani tukiona hivi hivi.

  Na Dr. JK, upole umekuzidi baba. Nchi yako hii na kama ningekuwa wewe mtu kama Slaa ningemfanya aka-disappear au akapata ajali tu. Si unajua tena....ha ha ha!!!


  God Bless my beautiful country Tanzania.

  And by the way, Dr. Slaa will NEVER be a president of my lovely Tanzania. NEVERRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRR !!!!

  Mtanzania Mpenda Amani
  (Sydney Australia)

  ReplyDelete
 9. sasa alimkwepa au alimkuta rais kaishaondoka?mimi nilifikiri labda alipofika alimkuta rais halafu hakumsalimia kila mtu si alikuja kwa wakati wake? na wewe matondo ninakuheshimu klakini hapo umechemka.halafu kama ni uzinzi wa dk kwani yeye rais sio mzinzi au hamumujui mtu wa saigon huyo labda kama hupajui saigon na mambo yake

  ReplyDelete
 10. na wewe wa sydney mbona umeikimbia nchi yako au ndonyie rafikizake david kameruni

  ReplyDelete
 11. Mtani,

  Namuunga mkono dr Slaa.
  Ushindi wa urais hata jumuiya ya ulaya wamekiri kwenye ripoti yao kuwa kura zilipigwa ila majumuisho ya kura yalikuwa na walakini,kama binadamu kwa nini asimdharau mtu au mfumo?

  Hata siye tusiojua kuandika mtatufanya tumtetee.

  Mlewa.
  Morogoro

  ReplyDelete
 12. Jamani utu umepungua sana hapa duniani. Jamani tujirudi na kuanza kusali kwa wote.

  ReplyDelete
 13. Tuwe fair politics is a dirt game na ukiwa na chuki ndio utakufa kabisa!
  Ushauri tu ni kuwa tusiwaamini wanasiasa their parrots who preach what they don't believe huwezi kusema mwenyekiti anakubali katibu anakataa sasa itifaki iko wapi hapo au nini kinaanza chama au mtu?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU