NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, January 22, 2012

HATIMAYE IMEKUWA: DR. SLAA AKUTANA NA DR. J.K. ANA KWA ANA !!!

Dr. Slaa akisalimiana na Dr. Kikwete ikulu jana. Ni picha ya 
Kihistoria ama?
  • Makala ya Bwn. Ally Ulanga yaliyochapishwa kule Wanabidii nami nikayaweka HAPA yaliwasha moto mkali. Katika makala hayo, Bw. Ulanga alimlalamikia sana Dr. Slaa kutokana na kitendo chake cha "kukwepa" kukutana na Dr. Kikwete katika mazishi ya mbunge wa Chadema, Regia Mtema. Bwana Ulanga aliendelea kubainisha kwamba Dr. Slaa alikuwa hajawahi kukutana na Rais Dr. Kikwete ana kwa ana tangu alipogaragazwa katika uchaguzi mkuu uliopita. 
  • Habari hizi pia ziliripotiwa na gazeti la Mwananchi. Habari za kidaku zikaendelea kusema kwamba Dr. Slaa alimkwepa Dr. Kikwete eti kwa sababu alikatazwa na mkewe kusalimiana na rais. 
  • Nimefurahishwa na taarifa hizi kwamba Dr. Slaa hatimaye ametinga ikulu jana na kusalimiana ana kwa ana na rais Dr. Kikwete. Naamini kwamba jambo lililompeleka ikulu ni kubwa na la muhimu kwa maslahi ya taifa letu. Kwa hili Dr.Slaa na Dr. Kikwete wanastahili pongezi kwa kutuonyesha Watanzania kwamba pamoja na tofauti zao kali za kisiasa bado wanaweza kukaa pamoja na kujadili masuala muhimu yanayohusu taifa letu. 
  • Ni lazima tuendeleze ule utamaduni wa kutatua matatizo na tofauti zetu kwa njia ya mazungumzo. Na kwa hili Dr. Slaa na Dr. Kikwete wameonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa !
Picha zote ni kutoka Jamii Forums

Soma maoni ya Mwanaharakati Mwl. Lwaitama kuhusu suala hili HAPA

1 comment:

  1. Nanukuuu kipengele``.....Ni lazima tuendeleze ule utamaduni wa kutatua matatizo na tofauti zetu kwa njia ya mazungumzo. .....´´

    Umemaliza Mkuu!

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU