NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, January 18, 2012

HEBU ITAZAME VIZURI HII MELI ILIYOLALA. IFIKIRIE KAMA NI NCHI.....

 • Meli kubwa hili la kifahari kwa jina Costa Concordia limelala chali ufukoni mwa bahari ya Tucsan kule Italy. Mpaka sasa watu 11 wameshathibitishwa kuwa wamefariki. Wengine 29 hawajulikani waliko. Lita za mafuta zipatazo 500,000 huenda zikamiminika baharini katika sehemu ambayo imetengwa kuwa mazalia salama ya nyangumi na pomboo (dolphins). Kwa nini ajali hii imetokea?
 • Inavyosemekana ni uzembe wa nahodha. Yeye aliacha kufuata ramani za njia aliyopangiwa na badala yake akaisogeza meli karibu na pwani zaidi ili kujionyesha. Kwa kufanya hivyo meli ikagota kwenye mwamba. Ajali ikatokea. Na kibaya zaidi, nahodha mwenyewe akatimua mbio na kulitelekeza jukumu lake la kuhakikisha kwamba kila abiria ameokolewa. 
 • Ni manahodha wangapi waliwahi kuangusha meli za nchi zao kama huyu nahodha mchovu wa Costa Concordia? Wafikirie akina Mobutu, akina Bokassa, akina Idd Amin, akina Banda, akina ......Afrika ina msururu mrefu wa manahodha wazembe waangusha meli. Tanzania je? Tuna bahati ama? 
 • Pengine maswali ya kujiuliza ni haya: Abiria wanastahili lawama katika uzembe huu wa manahodha wao? Kwa nini mtu mmoja awe na madaraka makubwa ya kusogeza meli karibu na miamba na hakuna mtu wa kumkataza? Wakati unaposoma makala haya mafupi unajua meli ya bara lako na nchi yako inaelekea wapi? Usije ukashangaa sana kama meli hiyo itakuwa inaelekea ufukoni kunako miamba ya hatari. Kama abiria mwema, jukumu lako ni nini?

3 comments:

 1. Tatizo MANAODHA wetu wanatununu hata kwa ubwabwa halafu wanashika hatamu na meli ikianguka wao wanapakukimbilia!:-(

  ReplyDelete
 2. Mungu atulinde Profesa Matondo!!!! Mambo ni mengi sana.

  ReplyDelete
 3. Maumivu ya kichwa huanza polepole!
  Si ajabu kuja kuiona Tanzania ikianguka kama Costa Concordia!
  Viongozi wameiharibu jamii ya watanzania. Nasema hivi kwa sababu wao ndio manahodha (kama ulivyofananisha meli hiyo na nahodha wake).

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU