NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 16, 2012

UTAFITI: ETI KUANGALIA TV KWA SAA MOJA KUNAPUNGUZA DAKIKA 22 ZA MAISHA YAKO !!!

  • Ukifuata kila linalosemwa na wanasayansi utashindwa kuishi. Leo watasema kunywa kahawa kunapunguza msongo wa mawazo. Kesho watasema kunywa kahawa  huko huko kunaongeza shinikizo la damu na uwezekano wa kupata pigo la kiharusi. Leo watasema hiki na kesho watasema kile ali mradi ni vurugu tupu. Kibaya zaidi ni ukimya wao kuhusu nini cha kufanya hasa pale tafiti zao zinapotoa matokeo yanayokinzana
  • Kwa vile nyingi ya tafiti hizi hufanyika huko Ulaya na Marekani, Waafrika inabidi kuyapokea matokeo ya tafiti hizi kwa uangalifu sana kwani huwa hayazingatii mazingira yetu na mtindo wetu wa maisha (japo sasa tunajitahidi sana kuwaiga kwa kila kitu).  
  • Utafiti uliofanywa mwaka jana na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Queenesland unaonyesha kwamba kuangalia runinga kwa watu wenye umri wa miaka 25 na kuendelea kuna madhara makubwa kiafya na kunapunguza muda wa kuishi. Utafiti huu unaonyesha kwamba kwa kila saa moja unayoitumia ukiangalia runinga basi unajipunguzia dakika 22 katika maisha yako. Hii ni sawa na kuvuta sigara mbili. 
  • Wanasayansi hawa wanasema kwamba tatizo hasa siyo kuangalia tv bali madhara ya kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ambako kunasababisha magonjwa ya moyo, kisukari, kunenepeana na matatizo mengine ya kiafya yanayosababishwa na mtindo wa maisha ya kubweteka (sedentary lifestyle). Kufanya mazoezi, hata kama ni dakika 15 tu kwa siku ni jambo la muhimu na kumeonyeshwa kuwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kuongeza siku tatu katika maisha yako
  • Ati, kwetu sisi Waafrika, kuna ukweli wo wote katika utafiti huu? Utafiti huu unapatikana HAPA.

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU