NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, February 12, 2012

KIFO KINAPOBISHA HODI: WHITNEY HOUSTON (48) AFARIKI DUNIA.

Whitney Houston akiwa na Clive Davis enzi za uhai wake
  • Whitney Houston ni mwimbaji mmojawapo niliyempenda sana hasa kwa sauti yake yenye utamu wa kushangaza. Ndiyo maana nimesikitishwa na habari za kifo chake cha ghafla. Ingawa matumizi ya madawa ya kulevya yalikuwa yamemdhoofisha kiafya na kuharibu ile sauti yake nyembamba tamu mithili ya chiriku, wengi walikuwa wanaamini kwamba hatimaye alikuwa anakaribia kufanikiwa kuachana na tabia yake hiyo. 
  • Jana tu aliimba wimbo wa Yes, Jessus Loved Me katika hafla ya  Kelly Price & Friends Unplugged: For The Love of R&B Grammy Party na usiku wa leo alikuwa amepangwa kama mmoja wa waimbaji katika hafla ya nguli wa muziki aitwaye Clive Davis. Hebu sikiliza kipaji chake cha kushangaza katika wimbo wake mashuhuri wa Daima Nitakupenda hapa chini. Mungu Ampumzishe salama !!!

2 comments:

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU