NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, February 1, 2012

MGOMO WA MADAKTARI: HIVI KWELI TUKO SIRIAZI NA INCHI HII ???

  • Kuna kipindi walimu walitishia kuitisha mgomo wa nchi nzima. Waziri wa elimu wa wakati ule alitoa kauli ya dharau sana akisema kuwa kama kweli walimu wale walikuwa wanataka kugoma, basi kulikuwa hakujaharibika neno kwani angeweza kuokota watu mabarabarani wakaingia madarasani kufundisha bila wasiwasi wo wote
  • Ningali naikumbuka kauli hii kwani, mbali na kuonyesha kiburi na kutojali kwa serikali ya wakati ule, inaonyesha jinsi taaluma ya ualimu na sekta ya elimu kwa ujumla inavyodharauliwa. Walimu wanaweza kuokotwa tu mabarabarani !!! Na wakati huo huo eti hii ndiyo sekta-mama katika maendeleo ya nchi yo yote ile hapa duniani kwani hakuna nchi ambayo imeshawahi kuendelea bila kuimarisha sekta yake ya elimu.
  • Kati ya taaluma zinazoheshimika hapa nchini na duniani kote pengine ni hii ya udaktari. Taaluma hii ni nyeti kwa maana kwamba inahusu uokoaji wa maisha ya watu moja kwa moja na kuwa daktari inakubidi usome kwa miaka mingi (kule Marekani si chini ya miaka 6 katika Chuo Kikuu). Taaluma hii haina mwanya wa kufanya makosa na waipatayo hula kiapo cha kuokoa maisha ya wagonjwa wao na si vinginevyo - popote pale na katika hali yo yote ile.
  • Mgomo wa madaktari unaoendelea unasikitisha sana. Serikali haikujua kuwa madaktari  ni muhimu kuliko walimu na kwamba hawawezi kuokotwa mabarabani? Serikali haikujua kwamba kama madaktari wangegoma basi maisha ya watu wake na hasa masikini yangepotea? Kama serikali ililijua hili, kwa nini haikuchukua hatua kuhakikisha kuwa mgomo huu hautokei. Si tunaambiwa kwamba kinga ni bora kuliko tiba? 
  • Taarifa zinazosema kwamba mpaka sasa wagonjwa wapatao 201 wameshapoteza maisha yao kutokana na mgomo huu zinasikitisha sana. Bila shaka hawa ni wagonjwa masikini ambao hawana uwezo wa kwenda katika hospitali za binafsi ambazo ni ghali sana kwa wananchi wa kawaida. Wangekuwa na uwezo bila shaka wangekuwa wameshakimbilia huko au India kabisa!
  • Ati, ni nani anayepaswa kulaumiwa kutokana vifo hivi? Ni madaktariserikali au wote wawili? Au pengine kwa vile ni vifo vya watu masikini basi haina neno? Kwa wenzetu mkasa kama huu unatosha kuwafanya wahusika wote kujiuzulu, kuchukuliwa hatua za kisheria na kulipa fidia za mamilioni ya dola. Lakini kwetu sisi, ni siasa, utoto na kutojali tu kama kawaida.  Ndiyo maana nikauliza kama kweli tuko siriazi na nchi yetu hii nzuri iliyojaliwa kwa kila kitu na Muumba. 
Katuni kutoka kwa Said Michael
  • Itakuwaje kama siku moja hawa masikini tunaowaacha wakifa kiholela hivi kama wanyama katika makorido ya hospitali zisizo na madaktari wakiamka na kusema sasa yatosha? Jibu bila shaka linapatikana katika historia. Mungu Ibariki Tanzania !!!
Kwa habari mbalimbali kuhusu mgomo huu soma HAPA au HAPA

1 comment:

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU