NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, March 12, 2012

HAKA NDIKO KABINTI KANGU KA MWISHO. NA LEO KAMEFIKISHA MIAKA MINNE !!!

 • Kanaitwa Johari Long'hwe Matondo (Hilo jina la kati wazungu hawawezi kabisa kulitamka hata uwape nini). Na jana Mungu alikajalia kufikisha miaka minne. Kana afya njema, kana akili shuleni na ni kabinti kanakompenda Mungu sana. Kila siku asubuhi huwa kana tabia ya kusali. Utakasikia kaking'aka: "Hey, we haven't prayed yet!" Basi hapo hata wakubwa huwa tunaona aibu na familia nzima huwa tunakusanyika na kusali pamoja. Furaha na amani iliyoje !!! 
 • Mara nyingi utakasikia kakinitakia mema: "Dad, You are going to have a good day today". Nami hapo huondoka nikiwa na nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya. Ati, ni nini kinachoweza kushindana na sala ya kimalaika cha Mungu kama hichi? Ni uovu gani unaoweza kupambana na sala ya mtoto mdogo asiye na doa bado kama huyu?

 • Tunamuomba Mungu Aendelee kukakaondolea uovu wote na Akazidi kukashushia mibaraka tele na maisha marefu yenye furaha na heri. Amina !!! 

6 comments:

 1. kaka huwa hawasemagi mwa mwisho ..LOL. Nadhani atakuwa sista huyu shangazi yangu.HONGERA SANA kwa kutimiza miaka.

  ReplyDelete
 2. Long'hwe nakutakia afya njema hasa wakati huu wa kuadhimisha siku yako ya kuzaliwa. Happy Birthday to you Long'hwe. Kinehe mayu?
  Matondo umeniacha hoi,yaani binti yako alikosakosa kuzaliwa siku niliyozaliwa.

  ReplyDelete
 3. Hongera sana Shangazi Johari, Mungu azidi kukubariki na kukutumia,uwe na wakati mwema,Hongera pia wazazi Mungu azidi kusimamia malezi yenu!!!!Kamwisho????

  ReplyDelete
 4. Mungu akubariki binti Johari Long'hwe ukue katika hekima yote ukimpendeza Mungu na Wanadamu. Wazazi wako waendelee kuona na kupata faraja kwa kuwa nawe!

  ReplyDelete
 5. Kuna vitu vingi alivyonavyo mwanadamu lakini kamwe hawezi kumfikia mtoto. Watoto hawana hila wala hatia katika mienendo yao bali hukumbana nayo. Na ndivyo wahenga walivyosema "Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo". Hongera sana Johari na hongera sana Profesa Matondo kwa kumwezesha mwanao kuweza kutimiza malengo yake.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU