NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 7, 2012

URAIS JAMANI NI KAZI NGUMU. KAMA UNABISHA TAZAMA PICHA HIZI MBILI KWA MAKINI

  • Kuna wakati huwa namsikitikia Obama. Akina Rush Limbaugh, Sean Hannity, wagombea uraisi kwa tiketi ya chama cha Republican (Mitt Romney, Newt Gingrich na Rick Santorum) na wahafidhina wengine wanapomwandama kila kona mpaka kufikia hatua ya kumtukana huwa naishia kusikitika. Mpaka katika forum moja kukawa na mjadala mkali kuhusu umuhimu na ulazima wa kuwa rais wa nchi kama Marekani - kazi ngumu kuliko zote, yenye mshahara kidogo na isiyo na shukrani. Halafu nikakumbuka maoni na nadharia za wanasaikolojia kuhusu watu ambao wanaweza kufanya kazi ngumu na zenye misukosuko kama hizi ni watu wa aina gani.
  • Mimi nadhani kwa kiongozi wa nchi za Kiafrika tena anayewapenda na kuwajali watu wake kazi ya uraisi ni ngumu zaidi. Ati, anajisikia vipi anapowaona watu wake wakiwa hawana chakula? Wakiandamwa na magonjwa? Wakiwa katika umasikini wa kutisha? Hawana vituo vya afya, Ufisadi kila kona na matatizo mengineyo? Anajisikiaje?
  • Picha hizi za Mwalimu Nyerere na Mh. Dr. JK zinaonyesha huzuni, fikra nzito na pengine zinawakilisha misukosuko na "mateso" yanayoambatana na kazi ya uraisi barani Afrika. Sijui zilipigwa katika mazingira gani lakini zinatosha kuwaonyesha ugumu wa kazi ya uraisi wale wote ambao wanaunyemelea hapo mwaka 2015. Je, wana majibu (ya vitendo) kwa matatizo mengi yanayoikabili nchi yetu au matumbo na umaarufu ndivyo vinawasukuma? 

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU