NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, April 5, 2012

NINI HASA MAANA YA NENO "KUDADADEKI" ?

 • Kiswahili, kama lugha zingine, ni lugha inayokua na kubadilika kila kukicha. Katika kufanya hivi maneno mapya yanazaliwa na mengine yanakufa au kubadilika. Mabadiliko haya katika lugha yanaakisi mabadiliko yanayotokea katika jamii katika nyanja zake mbalimbali. 
 • Hivi karibuni neno kudadadeki limepata umaarufu mkubwa hasa kutokana na hotuba ya "kihistoria" iliyotolewa na mbunge wa Mtela "Mheshimiwa" Livingstone Lusinde wakati akimnadi mgombea wa chama chake (CCM) aliyeshindwa katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.
 • Katika hotuba hiyo, Bwana Lusinde alitamka neno kudadadeki mara saba. Japo nilisikiliza vizuri hotuba hiyo, neno hili lilinitatanisha na pamoja na kusoma mijadala mbalimbali hapa na pale bado sijaelewa hasa maana ya neno hili na matumizi yake katika jamii.
 • Katika mjadala mmoja ikasemekana kwamba neno hili ni sawa na tusi la Kiingereza "Bullshit". Wengine wakasema linahusiana na vitendo vya kishoga. Yote kwa yote hakukuwa na jibu la jumla mbali na ukweli kwamba siyo neno zuri. 
 • Kuna anayejua kwa uhakika chanzo cha neno hili, maana yake na matumizi yake sahihi katika lugha ya Kiswahili?

5 comments:

 1. Kudadadeki!!!
  Hivi neno KUDADADEKI ni gumu mpaka nawe linakupa utata?
  Hapa nilidhani ni mimi wa kukuuliza wewe.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mzee wa Changamoto:

   Inaonekana maana yangu mimi ina matatizo kidogo. Unajua ukijitenga na jamii-lugha kama sisi tulio huku mbali ughaibuni, umuduji wako wa lugha husika unapungua pole pole.

   Japo najitahidi kujibidisha ili niweze kuendana na mabadiliko halisi yanayotokea katika lugha nizijuazo, siyo jambo la ajabu kujikuta ukipambana na dhana ngeni katika lugha hasa maneno ya mitaani na misemo kama hii ya kudadadeki.

   Ningali nadhani kuwa hili ni neno la mitaani, pengine neno la kihuni na ndiyo maana huyu "Mheshimiwa" akalitumia mara saba katika hotuba yake hii ya Kihistoria.

   Kudadadeki !!!

   Delete
 2. kudadadeki hili neno alikuwa anapenda kulitumia mchekeshaji wa ze komedi badala ya kusema ku......o akawa anakwepesha hapo anasema kudadadeki kwahiyo nineno la kihunihuni hivi lakini ndio hivyo likishazoeleka litaonekana ni rasimi ktk matumizi

  ReplyDelete
 3. Kwanza kulikuwa hakuna neno "KUDADADEKI" neno halisi ni "KUDADEKI" neno hili asili yake ni Mjini Arusha likiwa limeanza miaka ya 1998 pembezoni mwa mji(Matejoo,Ngarenaro ambapo wanapaita sasa Ngaleloo,Majengo pamoja na Ngaramtoni kwa kifupi "NGARA") Neno hili ni neno la mshangao kama vile dah! duh, ama Aisee?. Limekuwa likitumika sana wakati wa michezo ya aina ya Gololi na Mpirani. Hasa kuonyesha msisitizo flani. Wa Chugga hapa. Swallow

  ReplyDelete
 4. HILI NENO NI KAMA KUJIAPIZA KWA KUKOSA KITU HASA KATIKA MOCHEZO AU MASHINDANO. AU KUONYESHA MSISITIZO WA KUTAKA KUMFANYIA MTU KITU KIBAYA

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU