NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, June 11, 2012

KWA NINI WASHITAKIWA HAWA WA UFISADI WA UDA WANA FURAHA NAMNA HII ???

Hapa Mshitakiwa anakupa dole !!! 
Ni aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sinza, Salum Mwaking'nda

Huyu ni Mzee Mzima Idd Simba akiwa kafurahiiii....

Siwajahi kuona washitakiwa wenye furaha kama hawa. Ni nini kinachowafanya wawe na furaha namna hii wakati kesi inayowakabili ni kubwa na iliyotuletea hasara ya mabilioni?
  • Ni kweli wangeendelea kutabasamu na kufurahi namna hii kama wangejua kuwa kuna uwezekano wa kupigwa mvua zaidi ya kumi kutokana na ufisadi wao huu?
  • Ni kweli wangeendelea kutabasamu na kufurahi namna hii kama wangejua kuwa kuna uwezekano wa kufilisiwa mali zao ili kufidia mali walizofisadisha?
  • Au wanatabasamu na kufurahi namna hii kwa sababu wanajua kuwa kesi hii, kama zingine zilizotangulia, nayo ni kiini macho tu na itaendelea kwa miaka na miaka, umma utasahau na mwishowe "watashinda" kesi zao. 
Tangu hapo zimwi likujualo halikuli likakumaliza ati !!! 

Hatuko siriazi na bado tuna safari ndefu sana !!! 

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU