NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, June 28, 2012

NENO LA KUTIA MOYO ASUBUHI YA LEO - EPUKA NJIA ISIYO NA VIPINGAMIZI !!!

  • Binadamu sisi ni viumbe dhaifu tusio na ukamilifu wo wote. Na mara nyingi, hata kama tukijifanya vipi, huwa hatujui tukitakacho. Sisi ni vigeugeu, walalamikaji, tusioridhika (hata kama tukitendewa wema namna gani), wakorofi na wenye utakatifu wa bandia. Ukweli ni kwamba, pamoja na kujipachika cheo cha u-Homo Sapiens ili kujipambanua na wanyama wengine, binadamu tungali wanyama tu kama wanyama wengine !
  • Ni kutokana na asili yetu hii, hata kama ungekuwa mtu mwema na kufanya wema kiasi gani, daima kuna watu ambao watakuchukia. Hata kama ungekuwa na mawazo mazuri kiasi gani, daima kuna watu ambao watakupinga, kukushambulia, kukuandama na kukuona kuwa hufai. Huwezi kumridhisha binadamu !!!
  • Kama nawe unaandamwa na kupingwa sana na ndugu na jamaa. Kama wafanyakazi wenzio wanakula njama ili kukuangamiza. Kama marafiki zako wamekutenga na kukugeuza kuwa adui yao nambari wani japo hujawakosea cho chote. Kama .....basi usife moyo.
  • Asubuhi ya leo nakutaka uinuke. Nakuomba ukavione vipingamizi vyao kama ishara tu zinazokukumbusha kuwa njia uliyomo ndiyo njia sahihi uliyopaswa kusafiria. Kumbuka kuwa njia isiyo na vipingamizi mara nyingi huwa inaelekea ndiko-siko. Mpendwa, nyanyua kichwa chako kwa maringo na bila aibu. Vitazame vita unavyopigwa na wafanyakazi wenzio ofisini, marafiki zako, ndugu na jamaa; na wengineo kama motisha wa kusonga mbele. Vione vipingamizi hivi kama vithibitisho kuwa upo na kwamba unachofanya ni cha maana. Kamwe usijisaili na kujionea shaka. Barabara hiyo iliyojaa vipigaminzi unayosafiria ndiyo barabara sahihi !!!

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU