NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, June 28, 2012

WASUKUMA NA NGOMA ZAO !!!

 • Makala haya kuhusu Wasukuma na Ngoma zao inatoka katika jarida la Femina Hip la Julai - Septemba 2006. Sijui kama jarida hili lingali linachapishwa.
 • Makala haya yalinivutia kwa sababu mimi ni mdau mkubwa wa mambo ya kitamaduni hasa ukizingatia kuwa utamaduni wetu kwa sasa unaandamwa na utandawazi. Inafurahisha kuona kuwa Wasukuma wangali wanadumisha ngoma zao za kienyeji. Makabila mengine hali ikoje?

22 comments:

 1. Inasikitisha sana kuona utamaduni wetu unafifishwa na kufuata tamaduni nyingine. Sijui watoto wetu watakuwa vipi kwa kweli. Maana siku hizi kila kitu cha zamani watu wanaona hakifai kabisa. Kuukataa utamaduni ni sawa na kujikataa wewe ni nani. UTAMADUNI WETU NDIO UASILI WETU.

  ReplyDelete
 2. Umenikumbusha ule wimbo au mwimbo kama wasemavyo akina Nkwingwa Mere nenele minzi kuby'ala chawiza. Nimekumbuka michembe na matobolwa kule Lalago na Mwamapalala karibu na Luguru. Upo hapo mwalimu ngw'ana wane? Nahene.

  ReplyDelete
 3. @ NN Mhango.
  Huna ruhusa ya kuvitaja vijiji vyangu. hahahah
  Mwaka gani uliishi au kupatembelea lalago na Mwamapalala.
  Ni kitu cha kushangaza sana kwa sababu umevitaja vijiji vyangu kwa pamoja. Utashangaa nikikuambia nilizaliwa Lalago na maisha yangu ya ujana yote yalikuwa Mwamapalala.
  Kwa kweli umenigusa

  ReplyDelete
 4. @ wanaMwamapalala samahani kwa kutokuomba ruhusa ingawa vijiji hivyo ni mali yangu kuliko wewe. Najua vijiji vingine kama vile Ngeme, Kosori, Nguliati na sehemu nyingine nyingi kuanzia Mwamapalala hadi Malita. Unalikumbuka basi la Ngusa Kitija .Pale Mwamapalala nilipenda sana kumtembea rafiki wa bi mkubwa wangu aitwaye mama Mchele. Hakuna kitu nakumbuka kama miwa mitamu ya Lalago.Mie nilizaliwa Malampaka Hospital ambako mama yangu alikuwa akifanya kazi kama tabibu.

  ReplyDelete
 5. @NN Mhango,
  Sina budi kukubaliana na wewe, Umegusia maeneo ambayo pia yana kumbukumbu nyingi katika maisha yangu. Ninao ndugu na marafiki ambao wametapakaa kwenye maeneo yote uliyoyataja.
  Sijapatembelea kwa muda sasa lakini ninapata habari zake mara kwa mara kwa sababu Bibi yangu(Mzaa Mama) bado anaishi hapo.
  Simkumbuki Mama Mchele lakini basi la Ngusa nalikumbuka sana.
  Baada ya kumaliza elimu yangu ya form iv nilienda kufanya kazi pale Malampaka ginnery kwa muda kabla ya kuelekea Buluba Sec School.
  Nashukulu kwa kumbukumbu zako nzuri ambazo zimenikumbusha mengi.

  ReplyDelete
 6. @NN Mhango,
  Hivi anayemsema ni Mama Mzee au siye. Kwa vile Mama Mzee alikuwa akifanya kazi kama tabibu katika zahanati ya wamishionari Mwamapalala.

  ReplyDelete
 7. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 8. Hapana. Bi mkubwa wangu si mama Mzee. Nimefurahi huenda kuna siku tutagongana kule na kupata mandege na nyama ya kuku au vipi. Kusema ukweli nimekumbuka sehemu nyingi kuanzia Kashishi, Zagayu, Ikindilo, Mbarandwa hadi kuvuka mto Simie kuelekea kule maeneo ya Nyalikungu kwa akina marehemu Silas Mayunga. Siku tukikutana huenda tutajuana. Kwa kisukuma jina Nkwazi waweza kulitafsiri kama Lubala Lutale. Naona leo niishie hapa.

  ReplyDelete
 9. Kama ujuavyo waswahili wanasema Milima haikutani bali binadamu hukutana vilevile ujue kuwa Mwamapalala uliyoiacha kipindi hicho siyo ya sasa. Mwamapalala ya sasa imekumbwa na theory ya Schumpeter's creative gales of destruction.
  Nhahene Lubala Lutale

  ReplyDelete
 10. Nashukuru kunijuza hayo kaka inshallah ipo siku tutagonga kule na kujikumbusha zama zile. Ni ndugyo Noni nt'ale au Lubala Lutale.

  ReplyDelete
 11. Ng'wanaMwamapalala na Lubala Lutale:

  Asanteni sana kwa kunikumbusha nyumbani. Vijiji hivyo navifahamu sana japo sijakaa wala kukulia huko. Baadhi ya vijiji (mf. Ikindilo na Zagayu) nilishawahi kufika mara moja moja tu.

  Nilikwenda kuomba kazi ya kupiga chaki pale Mwamapalala Sekondari baada ya kutoka JKT wakati nikisubiri kwenda Mlimani. Kabla hata hawajanijibu Wasabato wa Bupandagila Sekondari wakanichukua. Nimekumbuka mengi !!!

  Ikitokea tukawa huko basi tutafutane jamani, tuchinje ng'ombe na kula "kibulanga"

  Dwikalagi Mhola Badugu bane !!!

  ReplyDelete
 12. @ Masangu Matondo.

  Ninashukulu kwa kutujuza kama nawe pia ulishawahi kutembelea mitaa yetu na kuomba kutoa mchango wako angalau kidogo wa elimu kwa vijana pale nyumbani (Mwamapalala sekondari).

  Kama nilivyomdokeza Lubala lutale, waswahili wasemavyo, milima huwa haikutani lakini binadamu hukutana.

  Tunaomba ele Welelo ili siku hiyo ifike, ila kwa mfugaji kama mimi kuchinja ng'ombe ni hatua ya juu mno labda michembe na ka mbuzi katatutosha.

  Nhahene

  ReplyDelete
  Replies
  1. Cho! Mimi nilidhani utatukarimu hata mashishanga, wewe unazungumzia michembe. Nikiwepo mimi nitauwa nzagamba tukae tuchome na kula huku tukijikumbusha mambo ya zamani

   Delete
 13. Beng'whe! Makoye ga mbiti! Nangojea siku hiyo kwa kila aina ya bashasha na mshawasha ili tule kibulanga. Tatizo si kuchinja ng'ombe. Kama tungekuwa na mila ya kula tembo basi hata tembo angeangushwa. Kumbuka una-deal na viumbe wa aina gani. Sisi si matajiri wa fedha ila ni matajiri wa ilm.Tutajisanyasanya hivyo hivyo na kufanikisha muungano wetu au siyo? mwabeja gete gete nkwingwa.
  Nkwazi Mhango aka Noni nt'ahle Lubala Lutale

  ReplyDelete
 14. Du! Mmenikumbusha mbali sana japo nyote siwafahamu. Vijiji mlivyovitaja ndio vyangu haswa. Mimi nimesoma Luguru nikamalizia Ngeme. Mwamapalala Misheni nimekaa miezi kadhaa kwaajili ya mafunzo ya dini. Mimi nilitoka huko enzi zile za Bukoboga ambao siku hizi umedorola. Enzi za akina Mwanalukenena, Mwanamagwanje, Mwanalugembe, Mwanamabilika, Mwanankunu nk. Sijui kama yupo hata mmoja wenu anaowajua?

  Suala la kujitolea kufundisha shule zetu za Baliadi nakubaliana nawewe. Mimi niliwahi kufundisha Mwanapalala vipindi vichache tu kwa kujitolea. Mtu kama ataorganise tupo tayari.

  GEORGE JINASA

  ReplyDelete

 15. Mimi Tarafa ya Itilima ni vijiji vichache sana ambavyo sijafika. Ukianzia Nyakabindi, Gangabulili ukarudi Luguru, Inalo, Itubilo, Zagayu, Kabale, Ibendo, Bunamhala, Idoselo, Mwamapalala, Nyamalapa pale kwenye 'lud'ano", unakwenda Mwalushu, Mwanunui, Mwabahabi, Mwabayanda, unarudi Nkololo, unarudi nyuma zaidi kule ntuzu yenyewe kabisa kama Gamboshi, Ukungulyabashashi, Mbiti, Gasoli, Kanade nk. Uk

  ReplyDelete

 16. MADAI YA KWAMA WASUKUMA HATUNA MAADILI YA UONGOZI LABDA NI MANENO YA WATANI WETU WAZARAMO NA WAGOGO. KATIKA AFRIKA MASHARIKI HAMNA MAKABILA YALIYOKUWA NA UONGOZI MZURI NA IMARA KAMA WASUKUMA NA WANYAMWEZI. NDIO MAANA TUNA MANENO KAMA MTEMI KATIKA KISWAHILI AMBAYO ASILI YAKE NI KATIKA MAKABILA HAYA. HATA IKULU INAASILI YA USUKUMANI NA UNYAMWEZINI. PALE KWETU ITILIMA TULIKUWA NA UONGOZI MZURI NA IMARA SANA WA MWANILANG'A.

  ReplyDelete
 17. Ngeme unamkumbuka mwalimu mkuu Madereka Maganga na Tuli siyo? Umenikumbusha zama za dhahabu Jinasa. Nadhani unawakumbuka akina Fakale, Bilia,mzee Dangankulu na wengine waliokuwa maarufu Ngeme.

  ReplyDelete

 18. Hahahahaha! Wote hao nawakumbuka vizuri. Mwalimu Maganga alikuwa ndiye mwalimu mkuu kabla hajapokelewa na Mnegela. Mzee Dangankulu na Fakale aliekuwa na kiduka pale mjini namjua vizuri pia mzee Bilia ambaye alikuwa na mtoto wake anaitwa Maduhu. Mwalimu Tuly yeye alikuwa kama sikosei ana asili ya Pwani. Rafiki yake mkubwa alikuwa Fares Dickson. Unamkumbuka mwalimu Zoi?

  ReplyDelete
 19. Namkumbuka sana. Ungeweka picha yako huenda tungefahamiana vizuri. Nawakumbuka watu wengi kuanzia akina Buthoti Sabuni yule mzee mganga alikuwa na mtoto wake nadhani akiitwa Sebastian na dada zake akina Felista na Vero na wengine wengi. Maduhu Bilia namkumbuka sana. Fares namfahamu pia. Kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba Maduhu sijui baadaye alikuwa mhasibu kama sikosei na vitu kama hivi. Hakuna kitu nakumbuka kama harusi ya Dina Malubalu aliyelipiwa ng'ombe kibao pale kijijini. Kwa ufupi nimekumbuka historia ya maisha yangu. Je huwa unatembelea Ngeme?

  ReplyDelete
 20. daaa mmenukumbusha mipa kishapu saa 9 ikifika naoga kwenda kwenye ngoma ya bununguli kati ya lukondya mabiti na mwanagawa ilikuwa powa sana

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU