NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, July 16, 2012

NENO LA KUTIA MOYO ASUBUHI YA LEO: PENGINE INAKULAZIMU UPIGE MBIZI...

  • Pengine umesubiri vya kutosha ili meli ya matumaini yako iweze kutia nanga katika bandari yako bila mafanikio.  Pengine ndoto yako kuu bado haijatimia. Pengine kwa kadri siku zinavyokwenda ndivyo matumaini yako yanazidi kufifia. 
  • Kama una uhakika na mahali meli yako iliko basi nyanyuka. Acha kuendelea kubweteka hapo bandarini kwako. Itakulazimu upige mbizi na kuifuata meli yako huko huko baharini. Kama hujui kuogelea jifunze, lakini kamwe usikae tu na kulalamika. Jifunze hatari na misukosuko ya bahari. Tunakutakia upigaji mbizi mwema !!!

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU