NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, September 6, 2012

BINADAMU TUMEFICHWA YAJAYO !!!

  • Sijui ingekuwaje kama binadamu tungejua siku na saa ya kufa kwetu. Nimelifikiria hili baada ya kuiona picha hii ya Mwangosi - mwandishi wa Channel Ten aliyeuawa na polisi kule Iringa.
  • Inasemekana picha hii hapo juu ilipigwa dakika 20 tu kabla ya kifo chake cha kusikitisha. Hapa anaonekana akiendelea na shughuli zake za kupiga picha za mkutano wa Chadema bila wasiwasi. Kumbe masikini kifo nacho kilikuwa hapo pembeni tu kikimtazama...
  • Pengine badala ya kulalamika na kunyong'onyea, inabidi tuamke na kushukuru kwa kila siku na saa ambayo tuko wazima hapa duniani. Ukweli ni kwamba tunaweza kuondoka wakati wo wote.
  • Hebu na tukawatendee mema binadamu wenzetu ili siku tukiondoka - hata kama ni kwa ghafla na kwa kuonewa kama ndugu yetu Mwangosi, angalau tukaweze kukumbukwa kwa wema na ubinadamu wetu.
  • Kila siku ni lazima tuwakumbatie watoto, ndugu na marafiki zetu na kuwaambia kuwa tunawapenda na kuwathamini. Ni vizuri pia kuweka hati zote za muhimu tayari tayari – urithi, bima, wosia na mengineyo tayari tayari. Safari yetu hapa duniani yaweza kukoma wakati wo wote !!!
  • Pumzika salama ndugu Mwangosi. Yote ni ubatili na waliokutendea hivi nao siku moja watakukuta huko uliko. Japo wameonekana magazetini na kwenye runinga, si ajabu wakakingiwa kifua na walinzi wa mfumo – mfumo ambao hata hivyo umeanza kuonyesha nyufa za kuporomoka !!!

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU