NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, July 25, 2013

JAMANI, NIMERUDI !!!

 • Pengine inabidi niwaombe radhi wapenzi wa blog hii kwa kupotea kwangu bila kuaga. Imepita miezi minane bila kutupia cho chote hapa. Pamoja na kupotea kwangu huku, wapo wadau wa kweli ambao waliendelea kupitapita hapa na kuchungulia. Wengine walidiriki hata kuniandikia na kunilalamika kuhusu ukimya wangu. Kwenu nyote napenda kuwaomba msamaha jamani. Shughuli za kimaisha na misukosuko isiyoepukika vilinifanya nisiisogelee kabisa blog hii kwani sikuwa na nia wala azma ya kublog tena. Moto wa kublog ulikuwa umekaribia kuzimika !!!
 • Baada ya mambo kutulia, sasa najihisi kuwa ningali bado ninayo sauti; na moto ambao ndimize zilikuwa zimeanza kusinzia sinzia gizani sasa umepata pulizo jipya na umeanza kuangaza tena. Nitaendelea kublog tena siyo kwa mtindo wa ku-copy na ku-paste habari za watu wengine kama ambavyo imekuwa kawaida ya wanablog wengi bali kwa kuandika mawazo na fikra zangu mwenyewe (japo kwa kifupi) ili kuendeleza hoja, majadiliano na pengine masuluhisho kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu jamii yetu.   
 • Napenda kuchukua nafasi hii ili kuwakaribisha tena katika mnyukano wa "uppercuts" za hoja na mijadala mbalimbali (mithili ya Mike Tyson enzi zileeee!!!) 
loading

7 comments:

 1. Yaani watu tumeenda mpaka polisi hupatikana ila hatukukata tamaa tulikuwa tulikuombe na lei mungu ametasikua maombi yetu. KARIBU KARIBU KARIBU SANA. BINAFSI NIMEKUMUSS SANA.

  ReplyDelete
 2. Pole kwa yote..Tunashukuru Mungu upo na unaendelea vyema. .Karibu sana.

  ReplyDelete
 3. Makaribu mingeno sana. Tunafurahi kusikia u mzima na umerejea ulingoni. Karibu sana na salamu kwa familia.

  ReplyDelete
 4. Kaka Matondo, pole sana kwa upotevu wako. Nilikuja hadi katika ukuta wako wa Facebook kukuuliza kulikoni. Ninafurahi kuwa umerejea.

  Pia nikupongeze kwa kutotaka kuwa kama wanablog wengine mabingwa wa ku-copy na ku-paste.

  Kila la kheri mkuu.

  ReplyDelete
 5. Ujuo wako ulikuwa mfupi. Where are you?

  ReplyDelete
 6. Mie naona kama Matondo hajarejea bali kachungulia. Arejee tumuone na kumsikia kama zamani. Tueleze kunani ndugu yetu?

  ReplyDelete
 7. Matondo,
  Umenikumbusha mbali juu ya Mwalimu, Mh. Agricola pale Kahororo...sina la kunena Bwana ametwaa..! Tuombe kumaliza vyema maisha haya.
  shaphat

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU