Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili

Monday, January 23, 2012

UTAFITI: WAKAZI WA NCHI ZA BARIDI WANA MACHO NA UBONGO MKUBWA KULIKO WAKAZI WA NCHI ZA JOTO

 
Matokeo ya utafiti yaliyochapishwa mwaka jana yanaonyesha kwamba watu wanaoishi katika ukanda wa nchi za baridi juu ya mstari wa Ikweta wana macho na ubongo mkubwa zaidi kuliko wenzao wanaoishi karibu na mstari huo.

Kwa vile nchi nyingi za baridi mbali na mstari wa Ikweta zipo Ulaya, Urusi, Asia na Amerika ya Kaskazini, hii inamaanisha kwamba wakazi wa nchi hizi wana macho na ubongo mkubwa.

Na kwa vile sote tunajua kwamba ubongo mkubwa unahusianishwa moja kwa moja na akili nyingi, swali la muhimu linalozushwa na utafiti huu ni hili: Wakazi wa nchi za baridi (wengi wao ni weupe) wana akili kuliko wakazi wa sehemu zilizo karibu na Ikweta (weusi)? 

Japo watafiti wamekwepa kufanya jumuisho hili, inavyoonekana wamefanya hivyo ili kukwepa mitafaruku tu. Je, ugunduzi huu mpya unaweza kueleza tofauti za kimaendeleo na kisayansi kati ya watu wa “kaskazini” na “kusini”?

Mgunduzi mwenza wa “DNA” mwenyewe alipata matatizo makubwa alipotoa dai kama hili mwaka 2007, dai ambalo lilimfanya afukuzwe au kujiuzulu nyadhifa zake zote za kisayansi na kiuongozi alizokuwa akizishikilia

Kwa maoni ya kutatanisha kuhusu mkondo huu wa mawazo tazama maoni ya binti machachari wa Kichaga aitwaye Aika HAPA. Maoni haya yaliwasha moto mkubwa sana huku wengine wakimshambulia na wengine wakimuunga mkono.

Wewe una maoni gani? Ni kweli watu weusi tuna akili “pungufu” tukilinganishwa na weupe?

2 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Mwalimu Matondo habari za siku nyingi?
    Kaka usitishwe na utafiti huu. Kwanza si kweli kuwa ukubwa wa ubongo ndiyo ukubwa wa akili. Inasemekana kuwa Albert Einstein pamoja na kuwa jiniasi alikuwa na ubongo mdogo tu. Pia si kila utafiti una nia nzuri. Usishangae hawa jamaa siku moja kusema kuwa wasukuma si binadamu kamili. Muhimu ni kwamba kinachoonekana kuwa mafanikio na ujanja wa magharibi vilisababishwa na mazingira yao na roho mbaya ya kuwa tayari kuwanyonya hata kuwaua wenzao ili waishi. Hii ndiyo maana ya dhana nzima ya individualism versus collectivism.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

ASANTE KWA MAONI YAKO

Widget by ReviewOfWeb