Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili

Saturday, May 5, 2012

NI KWELI WASUKUMA HATUNA MAADILI YA UONGOZI ???

Ndg. William Ngeleja 

Nimepokea ujumbe huu kutoka kwa mtani wangu mmoja ambaye ni Mhehe. Anasema hivi"

"Pole sana ndugu yangu Matondo. Nimekuwa nikisema mara kwa mara kuwa Nyerere alikuwa sahihi kuwanyima Wasukuma nafasi kubwa kubwa katika serikali yake. Wasukuma mnachojua ni kufuga ng'ombe, chagulaga, ushirikina, kula ugali mgumu na kuoa wake wengi. Mambo ya uongozi bora na maadili hakuna. Pengine ni kiburi chenu. Pengine ni ile kasumba yenu ya kujirundikia ng'ombe wengi kwa kadri iwezekanavyo. Lazima tu kuna sababu"

"Anzia kwa Mzee wa Vijisenti na rada yake. Gamba sugu nambari wani yule. Kisa Msukuma. Angalia William Ngeleja. Pengine waziri mpuuzi na aliyelitia hasara kubwa taifa hili kuliko waziri mwingine ye yote tangu tupate uhuru. Alikuwa anauza madini kama vile masangu a.k.a makande yule. Kisa Msukuma. Halafu mwangalie Bwana mdogo Maige: Huyu amefikia hatua ya kuuza twiga wetu kila mahali. Au aliwa-konfyuzi twiga na ng'ombe? Wasukuma nyie hovyo kabisa. Hata yule Msukuma bosi wa TAKURURU Mh !!! Hivi si hata Balali naye alikuwa Msukuma au nimekosea. Hamfai kuwa viongozi nyinyi !!!"

Ndg. Ezekiel Maige

Nilikuwa safarini nilipoupata ujumbe huu na sijamjibu huyu mtani wangu vizuri. Nilichomwambia tena kwa kwa kifupi sana nikitumia simu yangu ya mkononi ni kwamba "Mbona umemsahau Magufuli, Akina Bomani, Mzee Mapesa na Wasukuma wengine walio(wahi kuwa) na madaraka makubwa serikalini? Mtani, ni lazima kweli tuuangalie ufisadi na ukosefu wa maadili wa mtu kwa jicho jumuishi tena la ukabila? Tukifanya hivyo, ni kabila gani ambalo linaweza kusimama na kujipiga kifua kuwa lenyewe ndilo adilifu kabisa kabisa na halijaguswa na kashfa za ufisadi?"

Ndg. Andrew Chenge

Wasukuma kama mtapita hapa basi jiteteeni. Mtani wangu huyu ni msomi na mchambuzi makini wa masuala ya kijamii na naamini kuwa pengine alikuwa ananitania tu. Hata hivyo utani wake huu umenichangamsha.

Video ni kwa hisani ya Kennedy

11 comments:

  1. Generalization at its best! Huyu jamaa (Ngeleja) na hao wenzie walikuwa na matatizo yao binafsi tu na wala si kwamba wamefanya waliyoyafanya eti kwa sababu ni "wasukuma". Hiyo ni 'nadharia mufilisi' kama mwalimu wangu wa fasihi pale Sengerema High School alivyopenda kusema. Sipendi sana watu wanaopima au kuhukumu wenzao kwa kutumia kigezo cha asili na ukabila badala ya vigezo vya ueledi. Ingawa amesema kiutani, isipokemewa hulka hii itaota mizizi katika jamii ya Kitanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Angalizo zuri Bwana Dennis. Japo huu ulikuwa ni utani lakini nadhani ndanimwe mnapaswa kuwa na ukweli fulani hivi. Sasa siyo enzi za Mwl. Nyerere tena na hizi dhana za ukabila na udini zinaanza kurudi pole pole.

      Kwingineko: Sengerema High School ulisoma mwaka gani. Hata miye nilipita hapo wakati ule wakuu wakifanya jaribio la kuanzisha HGK huku wakijua kuwa hawakuwa na walimu wala vitabu.

      Delete
    2. Labda mtani wetu angetusaidia kabila lenye maadili ya uongozi ili tulinganishe halafu ndio tutaujadili mtazamo wake kimakini zaidi.

      Hata hivyo mtani wewe ni kiboko.., haya twakusubiri..

      Delete
  2. Kimsingi, kama tutaamua kuchoka kufanya utafiti na kutumia hitimisho la jumla basi twaweza kusema watanzania wote si waaminifu. Maana wamekuwa wakifanyiwa huu uchafu nao wameridhika kuonyesha kuwa hata wao wangepata fursa kama hizo wangefanya hivyo. Kwa ufupi ni kwamba taifa letu liko msambweni likipelekwa puta kama kishada cha maua. Tumeharibikiwa kama taifa na si kabila fulani.

    ReplyDelete
  3. Na nyie Wasukuma mmezidi. Geez...!!!

    Halafu mbaya zaidi ninyi kwa ninyi hampendani wala kusaidiana. Ngeleja kapata huo uwaziri basi katutupa sisi marafiki zake wote wakati tumesoma pamoja.

    Angekuwa amepewa Mchaga au Mhaya hizo wizara angeacha Wachaga na Wahaya wengi sana huko. Lakini sasa Wasukuma ni uchawi tu na ubinafsi. Huyo Maige sijui ni utoto. Mtu unakwenda kununua nyumba ya dola 700,000 na kulipa CASH unategemea watu wakueleweje? Ngeleja naye anaporomosha ghorofa huko Mwanza. Ni aibu sana kwa kweli. Wajanja huwa wanajificha angalau kidogo.

    Wasukuma kazi mnayo !!!

    ReplyDelete
  4. hiyo ni 'Case-by-Case' mkuu! Ni sawa na kusema wakurya wote wana Ngeu ilhali mie sina hata kovu la kupigwa na manati!

    ReplyDelete
  5. Mimi nawafahaumu wasukuma wabaya sana kuliko shetani. Pia nawafahamu wasukuma wazuri kuliko malaika. Wengi wao ni marafiki zangu wa karibu kuliko watu wa kabila langu

    ReplyDelete
  6. ndio nyinyi wasuuma si ndio nyinyi mlimpa williamson almasi yeye akawapa shanga?!!!!!!

    ReplyDelete
  7. kweli jamaa aliyepost hii kitu kaenda shule

    ReplyDelete
  8. Hahaha.wsukums.na wanawake.weupe.mmmmm.pia.hawajali.wanahonga.sana.ukimpa.ushauri.wabushi.mpka.wale.nyapu.ndo.wanajuta.bde.tuna.uku.ulaya.wengi.malimbukeni.wamke.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

ASANTE KWA MAONI YAKO

Widget by ReviewOfWeb