Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili

Wednesday, June 13, 2012

UNAHITAJI KUJIUNGA NA FREEMASONS ILI UTAJIRIKE? BASI MUONE "DK" CHIPOTEKA !!!

  • Yaani unaambiwa ni utapeli kila mahali. Kuanzia waganga wa kienyeji kama huyu mpaka makanisani kwa "maaskofu" wanaokutaka utoe kila kitu ulichonacho ili upate mibaraka ya Mungu. Kwenye siasa huko sasa ndiyo usiseme...Na yule wa chini kabisa katika mfumo huu wa kitapeli naye akamtapeli nani? Pengine wengine itabidi tujifunze kutapeli familia zetu au kujitapeli sisi wenyewe. 
  • Na hili vuguvugu la Freemasons linalopigwa kila leo hapa Bongo nalo ni nini? Mara Ooh Freemasons wataiangamiza dunia 2012, mara hivi. Mbona huko kwa wenzetu hatuyasikii haya kuhusu hawa Freemasons? Japo ni kweli kwamba Freemasons ni kundi lenye usiri na utata mkubwa - tena lililosheheni memba wenye nguvu kihistoria na hata wakati huu, ni kweli wana uwezo wa kuiangamiza dunia? Kulikoni Bongo? Kwa nini utapelitapeli na kutishana namna hii?  
  • Tazama HAPA kwa mjadala mkali kuhusu hawa Freemasons kwa mtazamo wa Kiafrika. Maelezo ya kina kuhusu hawa Freemasons na imani zao yapo HAPA. Unaweza pia kusoma HAPA kuhusu mashirika mengine yenye nguvu na usiri mkubwa kama hawa Freemasons HAPA

1 comment:

  1. naomba mnisaidie kupata anuani ya freemason, kama email na call zao

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

ASANTE KWA MAONI YAKO

Widget by ReviewOfWeb